Rais Samia aagiza Darasa la Saba waliofutwa kazi walipwe stahiki zao

Rais Samia aagiza Darasa la Saba waliofutwa kazi walipwe stahiki zao

Miaka yote hiyo mwajiri anakuwa wapi kufanya verification ya credentials za huyo mwajiriwa...ina maana kama umemwacha aendelee kukufanyia kazi ina maana amekidhi vigezo na matarajio yako, hivyo huna sababu ya kumnyima chochote anachostahili.
Yaani umeniibia na kunidanganya halafu unasema nilikuwa wapi! Muda haubadili kosa mkuu, ukibambwa lazima upelekwe kwenye vyombo vya sheria.
 
Ndo unyama unaomaanisha, limekuchoma.
Sheria zifuatwe over.
Limenichoma ndio lugha gani?
Jikite kwenye hoja, sawa sheria zifuatwe... wakipewa hizo stahiki, wakafunguliwa mashtaka, wakahukumiea kisha wakapewa msamaha na Rais una tatizo na hilo?
 
Hoja yako ya ushindani sawa wa ajira ni tofauti na hoja ya watuhumiwa wa kuajiriwa Kwa vyeti deli kisha kufanya kazi katika Serikali au taasisi zake, kulipwa haki zake. Suala la illegality haliondoi ukweli kuwa mhanga alifanya kazi na anastahili kulipwa mara anapoachiwa au kuacha kazi. Serikali ilitakiwa kujitafakari katika ulegevu wa muundo na mifumo yake kiasi cha kuruhusu/kupitisha watu wasiokuwa na vigezo stahiki kuajiriwa. Na kama wahanga waliweza kufanya kazi zao kwa ufanisi, basi hakukuwa na sababu wa kuwekwa kwa vigezo vya ajira Kwa kuwa havihusiani na utendaji kazini. Hapa pia patahitaji review! Hayo yote ni makosa ya Serikali, siyo walioajiriwa na kisha kutimuliwa Kwa hoja ya vyeti fake. Inawezekana kabisa Serikali ilikuwa na uhitaji wa nguvukazi wakati huo inaajiri watumishi wasiokuwa na vyeti stahiki kiasi kwamba hakukuwa na ushindani Kwa walioajiriwa. Katika hili, hoja kwamba kuna watu waliachwa wakiwa most qualified haina mashiko yoyote. Let's be realistic please!
Mwizi kufanikiwa kuiba haihalalishi umiliki halali wa kile alichokiiba.....

Tatizo linaanzia pale walipotumia udanganyifu kupata hiyo ajira ndio inawaondolea uhalali wa wao kupata mafao......chanzo cha pato lao ni haramu na mafao yao ambayo ni sehemu ya mshahara huo haramu pia ni haramu
 
amejipatia fedha kwa njia ya udanganyifu wakati amefanya kazi ya halali?!...kwani serikali ilishindwa kuwagundua tangu mwanzo?!...unasubiri mtu afanye kazi miaka 40 ndo unamfukuza eti ana vyeti feki wewe unaona ni maamuzi ya busara hayo!?....mtu katumikia taifa alipwe stahiki zake kisha serikali iwe makini isiajiri tena watu wa aina hiyo wakati mwingine.....acheni roho mbaya kisa tu tangazo la rais limeenda kinyume na msimamo wa rais aliyekufa....kauli yake haikuwa neno la mungu..
Hawa waabudu Mtu jiwe hawataki madudu yake yaibuliwe na kupanguliwa, lakini itawabidi waishi tu na maumivu, au wamfuate huko jamuhuri ya malaika!
 
Yaani umeniibia na kunifanganya halafu unasema nilikuwa wapi!Muda haubadili kosa mkuu,ukibambwa lazima upelekwe kwenye vyombo vya sheria.
Wengi tatizo inaonekana si sheria kufatwa bali ni msamaha...
Nikuulize, wakipewa stahiki, wakashtakiwa kisha wakahukumiwa kwa sheria halafu Rais akawapa msamaha kwa mujibu wa sheria una tatizo na hilo?
 
Limenichoma ndo lugha gani?
Jikite kwenye hoja, sawa sheria zifuatwe... wakipewa hizo stahiki, wakafunguliwa mashtaka, wakahukumiea kisha wakapewa msamaha na raisi una tatizo na hilo?
Washitakiwe kwanza kwa kugushi, baadae mahakama itaamua.
Siyo mtuhumiwa alipwe then ashitakiwe.
Big No.
 
She is looking for cheap popularity,weledi hapo hakuna kabisa.Na hii inapeleka message gani kwa wengine:unaweza kugushi chetu na as long as hujagundulika after time t unapewa haki zako.Very bad precedent.
Tanzania tunapitia nyakati ngumu kiutawala
 
Washitakiwe kwanza kwa kugushi, baadae mahakama itaamua.
Siyo mtuhumiwa alipwe then ashitakiwe.
Big No.
Sasa hapo unapingana na utaratibu wa sheria. Kumnyima haki mwajiriwa ni kinyume cha sheria. Sheria ni kwamba mfanyakazi alipwe haki zake. Kama alitapeli ashtakiwe kisha ahukumiwe kwa mujibu wa sheria. Mahakama iseme ni kweli ana makosa kisha hukumu. Kusema usimlipe ni kuvunja sheria maana anayethibitisha kuwa ni tapeli wa vyeti ni mahakama. Kiwango cha adhabu pia mahakama ndiyo inaelewa.
 
Kwa hili nadhani mama Samia ameliwazia kisiasa zaidi badala ya kiweledi.....

Mtu aliyeghushi vyeti vya kitaaluma ni mhalifu na angetakiwa awe jela......wanasiasa wetu wana akili ndogo sana, daima wanawaza kutoa kauli na matamko yatayowafurahisha wapiga kura ili waendelee kubakia utawalani........

Mtu anayekalia nafasi ambayo ametumia njia za udanganyifu kuipata anazuia nafasi kwa wengine waliovuja jasho kwa ajili ya nafasi hiyo.......
Sasa kwanini serikali ilivyowaondoa vyeti feki haikuwapeleka mahakamani kama ni jinai? Hujui kuna watu waliondolewa kazini kwa visasi kisa vyeti feki?
 
Kwa hiyo malipo hayo, ulitaka alipwe nani, ambayo huyu ameyafanyia kazi? Kila Mtu anakuwa paid for their service, nataka ufafanue upande huu wa kazi ya huyu mwenye cheti feki!
Kazi aliyofanya ni feki

Kazi inatangazwa kuendana na elimu

Mfano inatangazwa kabisa kuwa kazi ya ualimu inataka mtu awe na cheti cha form four na diploma mfano

Wewe huna vyote cha form four huna na cha diploma huna.Unaenda internet cafe kuchonga cheti feki

Wewe DARASA la saba sifa zote huna una ualimu gani uliokuwa ukifanya hapo zaidi ya utapeli kufundisha kiubabaishaji babaishaji tu maana elimu huna.Ukatapeli hadi wazazi wanakuita mwalimu mwalimu wakati ni tapeli tu la mtaani

Mishahara yote uliyolipwa ni pato la utapeli na pensheni uliyopeleka ni sehemu ya mshahara wa utapeli uliotapeli sababu hukutoa mfukoni mwako kupeleka hayo makato yalitoka kwenye mshahara uliotapeli serikali

Hivyo hiyo pension ni mali ya serikali sio yako rudisha na pesa zingine zote ulizolipwa tapeli
 
Kwa hili nadhani mama Samia ameliwazia kisiasa zaidi badala ya kiweledi.....

Mtu aliyeghushi vyeti vya kitaaluma ni mhalifu na angetakiwa awe jela......wanasiasa wetu wana akili ndogo sana, daima wanawaza kutoa kauli na matamko yatayowafurahisha wapiga kura ili waendelee kubakia utawalani........

Mtu anayekalia nafasi ambayo ametumia njia za udanganyifu kuipata anazuia nafasi kwa wengine waliovuja jasho kwa ajili ya nafasi hiyo.......
Kama serikali haikuwapeleka mahakamani basi imeamua kuhalalisha jinai.
 
Sasa kwanini serikali iliyowaondoa vyeti feki haikuwapeleka mahakamani kama ni jinai? Hujui kuna watu waliondolewa kazini kwa visasi kisa vyeti feki?
Ambaye anaona ameonewa apeleke malalamiko yake mahakamani ili apate haki yake......
 
Hivi adui wa chadema hasa ni Magufuli, Polepole na Bashiru au ccm?
CCM ni jina tu ila waliopo humo baadhi yao ndo hawafai kwa kauli zao. Mbona wapo wengi tu ndani ya ccm lakini ni watendaji wazuri au unataka mtu achukue chama kizima kisa wajinga wachache wanaokiharibu?
 
Mwizi kufanikiwa kuiba haihalalishi umiliki halali wa kile alichokiiba.....

Tatizo linaanzia pale walipotumia udanganyifu kupata hiyo ajira ndio inawaondolea uhalali wa wao kupata mafao......chanzo cha pato lao ni haramu na mafao yao ambayo ni sehemu ya mshahara huo haramu pia ni haramu
Uhalali wa kutokupewa mafao ulitakiwa kufata utaratibu upi? Twende taratibu bila mihemko, tujadili tu kwa hoja.
 
Sasa hapo unapingana na utaratibu wa sheria. Kumnyima haki mwajiriwa ni kinyume cha sheria.


Kitendo cha wenye vyeti feki kuajiriwa kiliwanyima haki wenye vyeti halisi wakakaa bila ajira na familia zao kuteseka kisa mwanga mwenye cheti feki kakalia nafasi zao

Pia kitendo cha cheti feki kuajiriwa kiliwanyima haki wananchi kupata huduma stahiki kutoka kwenye mwenye cheti original wakapewa na mwenye feki
 
Back
Top Bottom