Hoja yako ya ushindani sawa wa ajira ni tofauti na hoja ya watuhumiwa wa kuajiriwa Kwa vyeti deli kisha kufanya kazi katika Serikali au taasisi zake, kulipwa haki zake. Suala la illegality haliondoi ukweli kuwa mhanga alifanya kazi na anastahili kulipwa mara anapoachiwa au kuacha kazi. Serikali ilitakiwa kujitafakari katika ulegevu wa muundo na mifumo yake kiasi cha kuruhusu/kupitisha watu wasiokuwa na vigezo stahiki kuajiriwa. Na kama wahanga waliweza kufanya kazi zao kwa ufanisi, basi hakukuwa na sababu wa kuwekwa kwa vigezo vya ajira Kwa kuwa havihusiani na utendaji kazini. Hapa pia patahitaji review! Hayo yote ni makosa ya Serikali, siyo walioajiriwa na kisha kutimuliwa Kwa hoja ya vyeti fake. Inawezekana kabisa Serikali ilikuwa na uhitaji wa nguvukazi wakati huo inaajiri watumishi wasiokuwa na vyeti stahiki kiasi kwamba hakukuwa na ushindani Kwa walioajiriwa. Katika hili, hoja kwamba kuna watu waliachwa wakiwa most qualified haina mashiko yoyote. Let's be realistic please!