Nitakufa, lakini siabudu Mtu wala falfasa za Mtu! Matatizo ya elimu na vyeti yapo tele Tanzania, mfano mzuri ni sakata la Bashite, ambaye mwendazake alimkumbatia kama Luba, alafu Wewe unashangilia watu kupokwa stahiki zao, kisa makaratasi?!
Kuna udanganyifu wa vyeti kwa watu ambao hawajasoma wanatumia ujuzi na elimu ya Mtu, hao ni wadanyanyifu! Lakini Kwanini huzingatii watu kama madereva ambao hawakuwa na cheti cha form 4 tu lakini ameendesha gari miaka 30, leo unamnyima mafao aliyo fanyia kazi, kisa kikatarasi? Kwani ni cheti kinacho endesha gari? Na unajua pia kuna wenye vyeti halali kabisa lakini walifaulu kwa rushwa?! Na kuna wenye vyeti wazembe kazini?