Pre GE2025 Rais Samia aagiza mahindi kununuliwa kwa Tsh 700 kwa kilo

Pre GE2025 Rais Samia aagiza mahindi kununuliwa kwa Tsh 700 kwa kilo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Tuwe tunaeleweka tunaposema ya kuwa Rais Samia ni mpango wa Mungu Mwenyewe , Ameinuliwa na mkono wa Mungu Mwenyewe, aliandaliwa na Mungu Mwenyewe kuja kuliongoza Taifa letu, amefika hapo alipo kwa mpango wa Mungu na kwamba amekuja na kuletwa kwetu kama zawadi kwa watanzania.

Sasa baada ya kusikiliza maneno pamoja na kiu ya mamilioni ya wakulima kutaka mama awaangalie kwa jicho la huruma na Upendo wakulima kuhusiana na bei ya mahindi kwa kilo. Hatimaye Mama huyu mwenye moyo wa upendo,ukarimu ,utu,uungwana na mwenye kuguswa na maisha ya Watanzania amesikiliza kilio chao.

Ambapo ametoa maagizo mazito sana yaliyoibua shangwe,nderemo na vifijo kutoka kwa wakulima baada ya kutamka kuwa kuanzia kesho asubuhi mahindi yaanze kununuliwa kwa shilingi Mia 7 yaani 700 kwa kilo moja.ambapo Awali kabisa ilikuwa ni mia tano na baadaye ikaja mia 650 kwa mijini na 600 kwa vijijini.na sasa kwa ujasiri na upendo kwa wakulima bei elekezi ni mia 7 kwa kilo kuanzia kesho asubuhi.

Huo ni upendo mkubwa na usio na kifani alio uonyesha Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan kwa wakulima.hii ni baada ya kutambua gharama wanazotumia wakulima katika uzalishaji, hii ni kwa kujuwa kilimo ndio Secta iliyobeba kundi kubwa la watanzania,hii ni kwa kutambua kuwa kilimo ni biashara na kinapaswa kuwainua watu kiuchumi,hii ni kwa kutaka kuona watu wanaondokana na umaskini kupitia kilimo.

Haya ni maamuzi ya kijasiri ya Rais wetu mpendwa kutaka kila mmoja aone kilimo ni shughuli inayoweza mpatia mtu utajiri na kuishi maisha bora na ya heshima na kupata chochote akitakacho mtu na kupata milo mitatu ya Chakula kwa siku na iliyo bora kabisa. Ni maamuzi ya kumuinua mgongo mkulima ambaye miaka mingi amebeba mzigo wa kulisha Taifa hili na kuhakikishia usalama na utulivu unakuwepo. kwa sababu huwezi kumuongoza wala kusikilizwa na mtu mwenye njaa ya chakula tumboni.

Kikubwa na Rai yangu ni kuwataka na kuwakumbusha wakulima wenzangu kutunza mahindi ya chakula kulingana na ukubwa wa familia.msiuze mahindi na chakula chote mkasahau kuweka hazina ya chakula.njaa ni mbaya sana na inaleta fedheha na unyonge sana ikiingia ndani ya familia au nyumba.tutunze chakula ili kije kitutunze baadaye. Tuuze kulingana na mahitaji na kuacha cha ziada na matumizi ya baadaye.tusiuze chote halafu tukaacha wafanya biashara wakatutunzia nakuja kutuuzia kwa bei ya juu tusiyoweza kuimudu hapo baadaye. Ni bora ukose vyote ndani lakini chakula kiwepo.

Utulivu na Amani ya nyumba ni pamoja na uwepo wa chakula ndani .kama hakuna chakula unaweza kuona hata watoto muda wote ni kama wagonjwa ,kumbe wamezidiwa na njaa.huwezi ukafanya kazi kama kulima ikiwa umeshinda na kulala na njaa.njaa inauma na haivumiliki.

Screenshot_20240717-174351_1.jpg


Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Kama kweli ni mpango wa Mungu atufikirie na sisi tuliouza mahindi yetu sh 500 tuongezewe hiyo miambili basi. Maana nahisi yatafika buku halafu sisi tutapunjika.
Biashara ndio ilivyo .wewe unaweza uza kwa bei hii halafu mwenzako akauza kwa bei ile.Bei hubadilika kila siku na ndio maana wengine huhifadhi ili kusikilizia bei ya soko inakwendaje.
 
Munadagwanywa Tu 😂 kisa Uchaguzi umekaribia, si alikuwa ana msapoti bashe Kwamba awaache wakulima wauze mazao kokote wanakotaka.

SS mbona mnunuzi anampamgia bei ya kununua mazao, AU ndio mnunuzi kashapewa pesa na serikali kuyanunua Kwa kiasi Fulani na kiwango Fulani?.

Tz Bado sana
 
Akihotimisha ziara yake Mkoani Rukwa ,Rais wa JMT Samia S.Hassan ametoa Maelekezo Kwa Wakala.wa Hifadhi ya Taifa NRFA kuanza kununua Mahindi ya Wakulima Kwa bei ya Shilingi 700 Kwa kilo badala ya 500 ya awali baada ya Wakulima kulalamikia bei ndogo.

Aidha Rais amempa amri Waziri wa Kilimo kuanza kutoa Ruzuku ya Mbegu Kwa wakulima wa mahindi kuanzia msimu ujao.👇👇

Rais wa Wananchi anajali mahitaji Hongera Samia hongera 🇹🇿 na kazi iendelee
 
Ni kichaa tu anayeweza kufurahia hiyo bei ya miasaba.kwa maana hiyo gunia la kilo 100 unauza elfusabini?.wakati mwaka Jana watu tuliuza gunia laki na elfuhamsini.mbolea bei juu,mbegu bei juu na kukodisha shamba bei juu halafu unafurahia miasaba?kweli watz kujikomboa utachukua muda mrefu sana.
 
Akihotimisha ziara yake Mkoani Rukwa ,Rais wa JMT Samia S.Hassan ametoa Maelekezo Kwa Wakala.wa Hifadhi ya Taifa NRFA kuanza kununua Mahindi ya Wakulima Kwa bei ya Shilingi 700 Kwa kilo badala ya 500 ya awali baada ya Wakulima kulalamikia bei ndogo.

Aidha Rais amempa amri Waziri wa Kilimo kuanza kutoa Ruzuku ya Mbegu Kwa wakulima wa mahindi kuanzia msimu ujao.👇👇

Rais wa Wananchi anajali mahitaji Hongera Samia hongera 🇹🇿 na kazi iendelee
Kiufupi wateule wanamuangusha!
 
Samia hashiki jembe pengine hajui hata kulima.

Anapangaje bei ya mazao?

Bei ya mazao huamuliwa na uhitaji kwenye soko [demand] .

Hizi cheap politics hazina tija na watazibeba wajinga kuja kumpa sifa asizostahili.
 
Back
Top Bottom