Pre GE2025 Rais Samia aagiza mahindi kununuliwa kwa Tsh 700 kwa kilo

Pre GE2025 Rais Samia aagiza mahindi kununuliwa kwa Tsh 700 kwa kilo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Endelea kuyahifadhi..ila uwe unapita mara moja moja kuangalia hali yake ipoje hususan kama umepiga dawa ya maji .maana wengine wanaweka vidonge badala ya kupiga dawa.kwa hiyo aliyeweka kidonge hatakiwi kufungua fungua mlango mahali alipohifadhia mazao yake.
Nilioweka ni ya kidonge mkuu,
 
Endelea kuyahifadhi..ila uwe unapita mara moja moja kuangalia hali yake ipoje hususan kama umepiga dawa ya maji .maana wengine wanaweka vidonge badala ya kupiga dawa.kwa hiyo aliyeweka kidonge hatakiwi kufungua fungua mlango mahali alipohifadhia mazao yake.
Kwa hiyo vidonge si miezi mitatu ndio inabidi uuze?
 
Ukiona serikali inaingilia mpaka biashara za kufanya wanainchi wa kawaida jua kibubu Kina Hari mbaya
 
Ukiona serikali inaingilia mpaka biashara za kufanya wanainchi wa kawaida jua kibubu Kina Hari mbaya
Dhamira ya serikali yetu ni kumuinua mkulima. Ndio maana inaweka bei nzuri.lakini hujalazimishwa kuuza mahindi yako serikali.uza unapotaka Mwenyewe
 
Mimi nilishawahi kuwa na mahindi, nilikuwa nauza gunia kuanzia TZS 90,000 hadi 110,000. Maana yake kg ni 900 mpaka 1100. Ni gunia la kg 100.
 
Ni kichaa tu anayeweza kufurahia hiyo bei ya miasaba.kwa maana hiyo gunia la kilo 100 unauza elfusabini?.wakati mwaka Jana watu tuliuza gunia laki na elfuhamsini.mbolea bei juu,mbegu bei juu na kukodisha shamba bei juu halafu unafurahia miasaba?kweli watz kujikomboa utachukua muda mrefu sana.
Watu wapo Dar hawajui chochote kuhusu kilimo. Aisee, nimeshangaa sana watu kufurahia bei ya TZS 700 kwa kg!
 
Mama anaupiga mwingi.
Kwani siku hivi Wakenya wameacha kununua mahindi!? Kwa uzoefu wenu ni miezi gani ambayo bei ya mahindi inakuwa juu na ni ipi inakuwa chini na kwa sababu gani?
 
Back
Top Bottom