Pre GE2025 Rais Samia aagiza mahindi kununuliwa kwa Tsh 700 kwa kilo

Pre GE2025 Rais Samia aagiza mahindi kununuliwa kwa Tsh 700 kwa kilo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wewe ni Msemaji wao au? 😁😁😁

Umpe au usimpe atakuwa Rais
Labda muongeze sifuri, endelea kuota ndoto nyevu
FB_IMG_1697801575410~2.jpg
 
Ndugu zangu Watanzania,

Tuwe tunaeleweka tunaposema ya kuwa Rais Samia ni mpango wa Mungu Mwenyewe , Ameinuliwa na mkono wa Mungu Mwenyewe, aliandaliwa na Mungu Mwenyewe kuja kuliongoza Taifa letu, amefika hapo alipo kwa mpango wa Mungu na kwamba amekuja na kuletwa kwetu kama zawadi kwa watanzania.

Sasa baada ya kusikiliza maneno pamoja na kiu ya mamilioni ya wakulima kutaka mama awaangalie kwa jicho la huruma na Upendo wakulima kuhusiana na bei ya mahindi kwa kilo.hatimaye Mama huyu mwenye moyo wa upendo,ukarimu ,utu,uungwana na mwenye kuguswa na maisha ya watanzania amesikiliza kilio chao.

Ambapo ametoa maagizo mazito sana yaliyoibua shangwe,nderemo na vifijo kutoka kwa wakulima baada ya kutamka kuwa kuanzia kesho asubuhi mahindi yaanze kununuliwa kwa shilingi Mia 7 yaani 700 kwa kilo moja.ambapo Awali kabisa ilikuwa ni mia tano na baadaye ikaja mia 650 kwa mijini na 600 kwa vijijini.na sasa kwa ujasiri na upendo kwa wakulima bei elekezi ni mia 7 kwa kilo kuanzia kesho asubuhi.

Huo ni upendo mkubwa na usio na kifani alio uonyesha Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan kwa wakulima.hii ni baada ya kutambua gharama wanazotumia wakulima katika uzalishaji, hii ni kwa kujuwa kilimo ndio Secta iliyobeba kundi kubwa la watanzania,hii ni kwa kutambua kuwa kilimo ni biashara na kinapaswa kuwainua watu kiuchumi,hii ni kwa kutaka kuona watu wanaondokana na umaskini kupitia kilimo.

Haya ni maamuzi ya kijasiri ya Rais wetu mpendwa kutaka kila mmoja aone kilimo ni shughuli inayoweza mpatia mtu utajiri na kuishi maisha bora na ya heshima na kupata chochote akitakacho mtu na kupata milo mitatu ya Chakula kwa siku na iliyo bora kabisa.Ni maamuzi ya kumuinua mgongo mkulima ambaye miaka mingi amebeba mzigo wa kulisha Taifa hili na kuhakikishia usalama na utulivu unakuwepo. kwa sababu huwezi kumuongoza wala kusikilizwa na mtu mwenye njaa ya chakula tumboni.

Kikubwa na Rai yangu ni kuwataka na kuwakumbusha wakulima wenzangu kutunza mahindi ya chakula kulingana na ukubwa wa familia.msiuze mahindi na chakula chote mkasahau kuweka hazina ya chakula.njaa ni mbaya sana na inaleta fedheha na unyonge sana ikiingia ndani ya familia au nyumba.tutunze chakula ili kije kitutunze baadaye. Tuuze kulingana na mahitaji na kuacha cha ziada na matumizi ya baadaye.tusiuze chote halafu tukaacha wafanya biashara wakatutunzia nakuja kutuuzia kwa bei ya juu tusiyoweza kuimudu hapo baadaye. Ni bora ukose vyote ndani lakini chakula kiwepo.

Utulivu na Amani ya nyumba ni pamoja na uwepo wa chakula ndani .kama hakuna chakula unaweza kuona hata watoto muda wote ni kama wagonjwa ,kumbe wamezidiwa na njaa.huwezi ukafanya kazi kama kulima ikiwa umeshinda na kulala na njaa.njaa inauma na haivumiliki .View attachment 3044902

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Mia 700 ndio nini?
 
Very wrong , kama mahindi yapo mengi kuliko watumiaji bei ilitakiwa kushuka sio kuongezeka,

Okay now ni msimu wa mavuno bei 700 kwa kg sasa msimu wa masika ukifika hali itakuwaje?

Mwakani watakao lima mahindi wata_yapeleka wapi? Kama 700 ni bei ya ndani unadhani hii itavutia wanunuzi kutoka nje?
Nani atavutiwa kuja kununua mahindi yetu?

Demand and supply ni kama laws of gravity huwezi kufanya janja janja ukawa Sawa, matokeo ya hii bei tutayaona mwakani mpaka mwaka keshokutwa.

Solution ilikua ni kufungua mipaka watu wauze nje ndani kuwe na equilibrium.
 
Kwanini soko lisiamue bei ya mahindi?
Kwani wakulima wanailimia serikali?
Yaani wakulima walime kwa nguvu zao halafu bei ipangwe kwa huruma za Rais! Huu ni uwendawazimu wa kiwango cha SGR.
 
Wewe hujui taabu wanayopata wakulima, kilo 1 ilitakiwa kuuzwa 1,000

cc Lucas Mwashambwa
 
Very wrong , kama mahindi yapo mengi kuliko watumiaji bei ilitakiwa kushuka sio kuongezeka,

Okay now ni msimu wa mavuno bei 700 kwa kg sasa msimu wa masika ukifika hali itakuwaje?

Mwakani watakao lima mahindi wata_yapeleka wapi? Kama 700 ni bei ya ndani unadhani hii itavutia wanunuzi kutoka nje?
Nani atavutiwa kuja kununua mahindi yetu?

Demand and supply ni kama laws of gravity huwezi kufanya janja janja ukawa Sawa, matokeo ya hii bei tutayaona mwakani mpaka mwaka keshokutwa.

Solution ilikua ni kufungua mipaka watu wauze nje ndani kuwe na equilibrium.
Naona wivu umekushika baada ya kuona wakulima wanakwenda kufaidika na jasho lao.nakushauri kuwa na wewe nenda ukalime ufaidike
 
Kwanini soko lisiamue bei ya mahindi?
Kwani wakulima wanailimia serikali?
Yaani wakulima walime kwa nguvu zao halafu bei ipangwe kwa huruma za Rais! Huu ni uwendawazimu wa kiwango cha SGR.
Naona huelewi kitu chochote kile.unafahamu wafanyabiashara walikuwa wananunua shilingi ngapi mahindi huku mitaani? Hujuwi kuwa bei hiyo iliyotangazwa na Mheshimiwa Rais imekuwa neema kubwa sana kwa wakulima waliokuwa wameanza kunyonywa na wafanyabishara waliokuwa wananunua kwa bei ndogo?
 
Naona wivu umekushika baada ya kuona wakulima wanakwenda kufaidika na jasho lao.nakushauri kuwa na wewe nenda ukalime ufaidike
Nalima na nafanya biashara ya mazao ,by the way uelewa wako ni finyu kijana.

Siandiki siasa nazungumzia uchumi kuku wewe.
 
Back
Top Bottom