Pre GE2025 Rais Samia aagiza mahindi kununuliwa kwa Tsh 700 kwa kilo

Pre GE2025 Rais Samia aagiza mahindi kununuliwa kwa Tsh 700 kwa kilo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ndugu zangu Watanzania,

Tuwe tunaeleweka tunaposema ya kuwa Rais Samia ni mpango wa Mungu Mwenyewe , Ameinuliwa na mkono wa Mungu Mwenyewe, aliandaliwa na Mungu Mwenyewe kuja kuliongoza Taifa letu, amefika hapo alipo kwa mpango wa Mungu na kwamba amekuja na kuletwa kwetu kama zawadi kwa watanzania.

Sasa baada ya kusikiliza maneno pamoja na kiu ya mamilioni ya wakulima kutaka mama awaangalie kwa jicho la huruma na Upendo wakulima kuhusiana na bei ya mahindi kwa kilo.hatimaye Mama huyu mwenye moyo wa upendo,ukarimu ,utu,uungwana na mwenye kuguswa na maisha ya watanzania amesikiliza kilio chao.

Ambapo ametoa maagizo mazito sana yaliyoibua shangwe,nderemo na vifijo kutoka kwa wakulima baada ya kutamka kuwa kuanzia kesho asubuhi mahindi yaanze kununuliwa kwa shilingi Mia 7 yaani 700 kwa kilo moja.ambapo Awali kabisa ilikuwa ni mia tano na baadaye ikaja mia 650 kwa mijini na 600 kwa vijijini.na sasa kwa ujasiri na upendo kwa wakulima bei elekezi ni mia 7 kwa kilo kuanzia kesho asubuhi.

Huo ni upendo mkubwa na usio na kifani alio uonyesha Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan kwa wakulima.hii ni baada ya kutambua gharama wanazotumia wakulima katika uzalishaji, hii ni kwa kujuwa kilimo ndio Secta iliyobeba kundi kubwa la watanzania,hii ni kwa kutambua kuwa kilimo ni biashara na kinapaswa kuwainua watu kiuchumi,hii ni kwa kutaka kuona watu wanaondokana na umaskini kupitia kilimo.

Haya ni maamuzi ya kijasiri ya Rais wetu mpendwa kutaka kila mmoja aone kilimo ni shughuli inayoweza mpatia mtu utajiri na kuishi maisha bora na ya heshima na kupata chochote akitakacho mtu na kupata milo mitatu ya Chakula kwa siku na iliyo bora kabisa.Ni maamuzi ya kumuinua mgongo mkulima ambaye miaka mingi amebeba mzigo wa kulisha Taifa hili na kuhakikishia usalama na utulivu unakuwepo. kwa sababu huwezi kumuongoza wala kusikilizwa na mtu mwenye njaa ya chakula tumboni.

Kikubwa na Rai yangu ni kuwataka na kuwakumbusha wakulima wenzangu kutunza mahindi ya chakula kulingana na ukubwa wa familia.msiuze mahindi na chakula chote mkasahau kuweka hazina ya chakula.njaa ni mbaya sana na inaleta fedheha na unyonge sana ikiingia ndani ya familia au nyumba.tutunze chakula ili kije kitutunze baadaye. Tuuze kulingana na mahitaji na kuacha cha ziada na matumizi ya baadaye.tusiuze chote halafu tukaacha wafanya biashara wakatutunzia nakuja kutuuzia kwa bei ya juu tusiyoweza kuimudu hapo baadaye. Ni bora ukose vyote ndani lakini chakula kiwepo.

Utulivu na Amani ya nyumba ni pamoja na uwepo wa chakula ndani .kama hakuna chakula unaweza kuona hata watoto muda wote ni kama wagonjwa ,kumbe wamezidiwa na njaa.huwezi ukafanya kazi kama kulima ikiwa umeshinda na kulala na njaa.njaa inauma na haivumiliki .View attachment 3044902

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Garama ya kuzalisha 1kg ya mahindi ni Shs ngapi? Ni chini ya bei hiyo? Achana na blabla. Quantify your claim and praises.
 
Chini ya huyu mama neema zinazidi kimiminika Kila uchwao

Uzuri Kwa Sasa mahindi ni ya kutosha kazi imebali kidogo tuh Kwa Kila mtanzania kutafuta mboga ambayo ki uwalisia ni kama nayo mama katushika mkono
Kwa hakika wakulima chini ya uongozi wa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan wamekuwa na furaha sana na kufaidika na jasho lao. Ndio maana wanasubiri uchaguzi kwa hakika sana ili wampigie kura za ndio kwa kishindoo kikuu kitakacho itetemesha Dunia nzima
 
Machozi yamenitoka mpaka nimejaza bwawa sasa hv nafugia samaki kwa kutumia machozi
Fuga tu hao samaki maana hata soko la samaki nalo lipo tu zuri kwa juhudi za Mheshimiwa Rais wetu mpendwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan
 
Garama ya kuzalisha 1kg ya mahindi ni Shs ngapi? Ni chini ya bei hiyo? Achana na blabla. Quantify your claim and praises.
Acha kupiga porojo kwa vitu usivyo na uelewa navyo .mimi ni mkulima na ninafahamu vyema kabisa faida ya bei hiyo iliyotangazwa na Mama yetu mpendwa Daktari Mama Samia
 
Hakuna kitu chochote hapo cha kuniliza chawa , hilo gazeti lako peleka kwenyr vikundi vyenu vya WhatsAapp ili mumsifie mama yenu vizuri.
Wivu utakuuwa mwaka huu na roho yako hiyo ya kwanini.Mama anaendelea kuchanja mbuga katika mioyo ya mamilioni ya watanzania
 
Avha
Wewe mpuuzi hauna tangible data zaidi ya uchawa kwa huyo ajuza wenu hivyo sina sababu ya kuengage na wewe.

Na hii thread pia imeanzishwa na mtu wa kundi lako hivyo lazima mpeane support.
Acha ujinga wako hapa wewe
 
Wanamuangushaje? Kwenye hili wamemuangushaje?
Kama wateuliwa wangeyasikiliza malalamiko ya wakulima leo hii raisi asingekuwa na muda wa kusikiliza malalamiko ya wakulima labda angekua anatoa suluhu kwenye mambo mengine lakini wateule wamejaa vibri wanampa kazi raisi mara mbili akatafute mikopo ya maendeleo halafu pia aje atatue suala la bei je hapo wateule aliowaamini hawaja muangusha?!
 
Luca toa maelezo yanayoeleweka punguza mahaba hata unashindwa kufikisha ujumbe ipasavyo,hata pale ujumbe unapokuwa ni mzuri na ungeweza wanufaisha wengi,jitahidi kutokuwa mbinafsi kwa viwango hivi,utaweza kuwasaidia wengine.
Maelezo yangu mbona yapo wazi na yamenyooka kabisa ndugu yangu mtanzania.nimeambatanisha hadi maelezo ya ziada kutoka kwa waziri akimnukuu Mheshimiwa Rais
 
Lucas unaumwa?

Kuna mkulima mwenye mahindi mwezi huu July wa kuuza NFRA?

Mtaani hakuna mahindi ilhali Serikali inayauza yaliyoko NFRA nje ya Nchi, Zambia na Malawi🤔
Kweli nimeamini wewe ni mgonjwa au umeandika ukiwa na usingizi .napenda kukupa tu taarifa kuwa mimi ni mkulima na kwa sasa kuna watu wengine bado hata hawajapukuchua mahindi yao. Acheni kukaa huko mijini mpaka hamuelewi kinachoendelea hapa Nchini.
 
Kama wateuliwa wangeyasikiliza malalamiko ya wakulima leo hii raisi asingekuwa na muda wa kusikiliza malalamiko ya wakulima labda angekua anatoa suluhu kwenye mambo mengine lakini wateule wamejaa vibri wanampa kazi raisi mara mbili akatafute mikopo ya maendeleo halafu pia aje atatue suala la bei je hapo wateule aliowaamini hawaja muangusha?!
Sijaona Cha maana umeandika ,basi sawa
 
Sina neno wacha nile buyu nisubiri 2: pongezi za wakulima wanaopangiwa bei
 
Back
Top Bottom