Pre GE2025 Rais Samia aagiza mahindi kununuliwa kwa Tsh 700 kwa kilo

Pre GE2025 Rais Samia aagiza mahindi kununuliwa kwa Tsh 700 kwa kilo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Allah amzidishie mama Samia kila la heri, usikivu, utulivu na busara na subra.

Alilolifanya ni kubwa sana tena sana, maana wiki moja kabla aliwaongeza 100, sasa kawaongeza 100 nyingine.
 
Allah amzidishie mama Samia kila la heri, usikivu, utulivu na busara na subra.

Alilolifanya ni kubwa sana tena sana, maana wiki moja kabla aliwaongeza 100, sasa kawaongeza 100 nyingine.

Asiishie kwenye mahindi tu, aongeze na kwenye pamba, korosho
 
Sio sifuri itaongezwa buku kabisa.

Anaeota ni Mimi au wewe? Si ajabu una stress maana hujiamini na huna uhakika na unachokiota 😁😁
images (13).jpeg
 
Allah amzidishie mama Samia kila la heri, usikivu, utulivu na busara na subra.

Alilolifanya ni kubwa sana tena sana, maana wiki moja kabla aliwaongeza 100, sasa kawaongeza 100 nyingine.
Kwa hakika Mwenyezi Mungu aendelee kumtunza na kumbariki sana Rais wetu kwa kazi kubwa na njema anayoifanya katika kugusa Maisha ya mamilioni ya watanzania.
 
Asiishie kwenye mahindi tu, aongeze na kwenye pamba, korosho
Asiishie kwenye mahindi tu, aongeze na kwenye pamba, korosho
[/Q
Kila mtu atafikiwa na mkono wa Mheshimiwa Rais maana Rais wetu ni mwenye upendo na huruma na mwenye kujali maisha ya watanzania.ndio maana anaendelea kuwa msikivu na kujibu kero za kila mtanzania na kwa kila kundi.
 
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
15 July 2024
Kamsamba,
Jimbo la Momba.

Serikali ya CCM imechoka hivyo inahitaji kupumzishwa mfano mahindi WFP wanataka kununua kwa bei ya Tshs. 1,000 kwa kilo

Pamewaka!! CHADEMA WAIVURUGA CCM KAMSAMBA // WANACCM 100 WAHAMIA CHADEMA // WAFUNGUKA BAADA YA KUHAMIA


View: https://m.youtube.com/watch?v=ZTDtjKXVT-o

hotuba nzito za CHADEMA zashawaishi wanaCCM na wananchi.

Wasisitiza nchi kuwa na vijana na raia jeuri wanaoweza kuhoji badala ya kugaragara chini bali tuwahoji viongozi wa serikali

Leo kuna Kamsamba wanaCCM 100 kwa niaba ya wenzao wamejitokeza mbele ya makamu mwenyekiti wa kanda Nyasa CHADEMA..

Dhuluma za stakabadhi ghalani kwa zao la ufuta ni jambo la makosa makubwa wanalofanya serikali ya CCM kwa wananchi wa Kamsamba Momba ... huo ni ubabaishaji mkubwa wananchi walipwe kwa wakati badala ya kupewa risiti kwa mali kauli wakati wananchi wanataka fedha mkononi..

Serikali ya CCM imechoka hivyo inahitaji kupumzishwa mfano mahindi WFP wanataka kununua kwa bei ya Tshs. 1,000 lakini serikali hii ya CCM inataka wakulima wa mahindi walipwe Tshs. 500 kwa kilo ya mahindi.... chama dola kongwe cha kijani kimeshindwa kuwatetea ..


Halafu kwa kuwa 2024 na 2025 CCM wanakuja hapa na kibaba cha chumvi kutaka muwapigie kwa mapipa ya Pombe na T-Shirt, muwakatae hawa CCM.

Wazee wetu wamechoka kwa maji ya kutoka kutekwa mbali leo hii wanamuahidi katika umri huu kuwaletea maji, walikuwa wapi miaka yote hii 60 toka huyu mzee wetu akiwa kijana ... muwakatae hawa CCM kwa ahadi zao hewa miaka nenda rudi ..

Wana wa Kamsamba hivi kwanini mtembee na jini la CCM katika mfumo wa kadi ndani ya mfuko wako, leo tumechelewa kuwahii kufika ktk mkutano huu kutokana na barabara mbovu ikabidi gari yetu kutumia njia ya ngombe kufika hapa Kamsamba ...

TAKWIMU MUHIMU :
Kata ya Kamsamba wilaya ya Momba katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 23,456 . Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 17,055 walioishi humo.
 
Kwahiyo Dumla ni 2800? Kwa mahindi ya mwaka huu?
Je ya mwaka jana itakua bei gani?
 
Ndugu zangu Watanzania,

Tuwe tunaeleweka tunaposema ya kuwa Rais Samia ni mpango wa Mungu Mwenyewe , Ameinuliwa na mkono wa Mungu Mwenyewe, aliandaliwa na Mungu Mwenyewe kuja kuliongoza Taifa letu, amefika hapo alipo kwa mpango wa Mungu na kwamba amekuja na kuletwa kwetu kama zawadi kwa watanzania.

Sasa baada ya kusikiliza maneno pamoja na kiu ya mamilioni ya wakulima kutaka mama awaangalie kwa jicho la huruma na Upendo wakulima kuhusiana na bei ya mahindi kwa kilo.hatimaye Mama huyu mwenye moyo wa upendo,ukarimu ,utu,uungwana na mwenye kuguswa na maisha ya watanzania amesikiliza kilio chao.

Ambapo ametoa maagizo mazito sana yaliyoibua shangwe,nderemo na vifijo kutoka kwa wakulima baada ya kutamka kuwa kuanzia kesho asubuhi mahindi yaanze kununuliwa kwa shilingi Mia 7 yaani 700 kwa kilo moja.ambapo Awali kabisa ilikuwa ni mia tano na baadaye ikaja mia 650 kwa mijini na 600 kwa vijijini.na sasa kwa ujasiri na upendo kwa wakulima bei elekezi ni mia 7 kwa kilo kuanzia kesho asubuhi.

Huo ni upendo mkubwa na usio na kifani alio uonyesha Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan kwa wakulima.hii ni baada ya kutambua gharama wanazotumia wakulima katika uzalishaji, hii ni kwa kujuwa kilimo ndio Secta iliyobeba kundi kubwa la watanzania,hii ni kwa kutambua kuwa kilimo ni biashara na kinapaswa kuwainua watu kiuchumi,hii ni kwa kutaka kuona watu wanaondokana na umaskini kupitia kilimo.

Haya ni maamuzi ya kijasiri ya Rais wetu mpendwa kutaka kila mmoja aone kilimo ni shughuli inayoweza mpatia mtu utajiri na kuishi maisha bora na ya heshima na kupata chochote akitakacho mtu na kupata milo mitatu ya Chakula kwa siku na iliyo bora kabisa.Ni maamuzi ya kumuinua mgongo mkulima ambaye miaka mingi amebeba mzigo wa kulisha Taifa hili na kuhakikishia usalama na utulivu unakuwepo. kwa sababu huwezi kumuongoza wala kusikilizwa na mtu mwenye njaa ya chakula tumboni.

Kikubwa na Rai yangu ni kuwataka na kuwakumbusha wakulima wenzangu kutunza mahindi ya chakula kulingana na ukubwa wa familia.msiuze mahindi na chakula chote mkasahau kuweka hazina ya chakula.njaa ni mbaya sana na inaleta fedheha na unyonge sana ikiingia ndani ya familia au nyumba.tutunze chakula ili kije kitutunze baadaye. Tuuze kulingana na mahitaji na kuacha cha ziada na matumizi ya baadaye.tusiuze chote halafu tukaacha wafanya biashara wakatutunzia nakuja kutuuzia kwa bei ya juu tusiyoweza kuimudu hapo baadaye. Ni bora ukose vyote ndani lakini chakula kiwepo.

Utulivu na Amani ya nyumba ni pamoja na uwepo wa chakula ndani .kama hakuna chakula unaweza kuona hata watoto muda wote ni kama wagonjwa ,kumbe wamezidiwa na njaa.huwezi ukafanya kazi kama kulima ikiwa umeshinda na kulala na njaa.njaa inauma na haivumiliki .View attachment 3044902

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Umekosea kuandika, Rais hajasema hivyo! "Mia 700" uliyoandika ni sawa na elfu 7, yaani mia zikiwa 700 inakuwa 7,000. Ungeandika mia 7 yaani mia zikiwa 7 inakuwa 700.
 
mfano mahindi WFP wanataka kununua kwa bei ya Tshs. 1,000 lakini serikali hii ya CCM inataka wakulima wa mahindi walipwe Tshs. 500 kwa kilo ya mahindi....

Zambia kununua mahindi

TANZANIA YASAINI MAKUBALIANO NA ZAMBIA KUIUZIA TANI 650,000 ZA MAHINDI, KAULI YA BASHE NA MWIGULU


View: https://m.youtube.com/watch?v=pfunGatK8CM
Zambia imekumbwa na hali ya hewa ya El Nino, ambayo ni hali ya hewa inayohusishwa na mabadiliko ya mifumo ya upepo, ambayo inamaanisha halijoto ya joto ya juu ya uso wa bahari katika maeneo ya mashariki na kati ya Pasifiki na kusababisha ukame kwa nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.

Picha: Philimon Bulawayo/REUTERS
Zambia inapanga kuagiza tani 650,000 za mahindi meupe kutoka Tanzania baada ya ukame kupunguza uzalishaji kwa zaidi ya asilimia 50, waziri wa habari Cornelius Mweetwa alisema Jumatano.

Uzalishaji wa mahindi nchini Zambia katika msimu wa mazao wa 2023/24 unatarajiwa kupungua hadi tani milioni 1.5 kutoka tani milioni 3.2 msimu uliopita, kulingana na utafiti wa utabiri wa mazao.

"Serikali imefikia makubaliano ya awali na serikali ya Tanzania kuagiza tani 650,000 za mahindi meupe kutoka nje," Mweetwa alisema katika taarifa yake akitangaza maamuzi ya baraza la mawaziri.

Waziri wa Kilimo Mtolo Phiri alisema bungeni Jumanne kwamba nchi ilisitisha uuzaji wa mahindi nje ya nchi kufuatia upungufu wa tani milioni 2.1 na itaagiza nafaka hiyo kuu kutoka nje.

Zambia plans to import 650,000 tons white maize from Tanzania​

BY REUTERS - 19 June 2024 - 18:11

El Nino is a weather phenomenon associated with a disruption of wind patterns, which means warmer ocean surface temperatures in the eastern and central Pacific.

Image: Philimon Bulawayo/REUTERS

Zambia plans to import 650,000 metric tons of white maize from Tanzania after drought cut production by more than 50%, information minister Cornelius Mweetwa said on Wednesday.

Zambia's maize production in the 2023/24 crop season is expected to decrease to 1.5-million tons from 3.2-million tons the previous season, according to a crop forecasting survey.

"The government has reached an initial agreement with the Tanzanian government to import 650,000 tons of white maize," Mweetwa said in a statement announcing cabinet decisions.

Agriculture minister Mtolo Phiri said in parliament on Tuesday the country suspended maize exports following a deficit of 2.1-million tons and would import the staple grain.

Source: thesowetan newspaper
 
N

Nikuulize swali, kwa trending hiyo kufika mwezi wa 10, mahindi yanaweza fika 1000 kwa kilo?...maana mimi nilinunua 600 kwa kilo na nina gunia kama 150, nafikiri niziuze au nisikilizie?
Endelea kuzitunza .ila hakikisha umepiga dawa vizuri ili yasije yakapechwa halafu ukaingia hasara itakayo kububujisha machozi ya uchungu na majuto.
 
Back
Top Bottom