Rais Samia aambiwe Makamu wa Rais ni Mkubwa kwa Rais wa Zanzibar, au anafanya makusudi!?

Tulimponda na kumkosoa sana Hayati JPM kwa style hii ya kuamua tu mambo aonavyo kichwani mwake.
Kuweni wazi pia kwa Mama.
Nilimsikiliza Bungeni, na leo.
AMEKOSEA SANA. FULL STOP. Semeni ukweli, hata kama akiwa ni wa upande wenu.
 
Zanzibar ni nchi?
 
Wakumbushe banaa, naona wamejisahaulisha wakati hata miezi miwili haijaipita
 
Umenikumbusha kitu
Mwaka 1994 Nyerere (aliona mbali sana huyu mzee) kupima nguvu ya Maalim kisiwani, ingewezekana 1995 angeukwaa urais wa smz, sasa kikatiba raisi wa smz ni makamo wa rais wa JMT kumaanisha in absence of Rais wa JMT (akiwa safarini, akifa) makamo wake anashika nchi. Hili wahafidhina wa ccm hawakulipenda yakafanyika marekebisho kumuondoa rais wa smz kama makamo.
Kichekesho ni kuwa maalim hakushinda (hakutangazwa) na wazanzibar hawakuidai nafasi yao tena tukawa na makamo asiye na kazi.
Maalim jabali la siasa Tanzania katiba ilibasilishwa kumzibiti mtu mmoja.
 

1. Na wewe unakosea, hakuna nchi inaitwa Tanzania...

Tuna nchi inatwa JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ama kwa kiingereza THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA..

2. Kwa muktadha huu, Makamu wa Rais wa JMT is truly bigger than The president of Zanzibar. Kwa hiyo kiprotokali hilo linapaswa kuzingatiwa...

3. Nakubaliana na wewe kuwa Rais hukosea kiprotokali anapompa nafasi ya kwanza Rais wa Zanzibar kabla ya VP wa JMT...
 
Umeandika ugoro!
 
Wewe nawe ni zero brain. Mmoja anaitwa Rais na mwingine makamu wa rais bado huoni tofauti?
Makamu wa rais analinganishwa na makamu mwenzake.
Makamo wa rais wa jamuhuri ya muungano wa tanzania
Rais wa serikali ya mapinduzi zanzibar
 
Hivi nani huwa anawapotosha kuwa mbara huruhusiwi kununua uwanja Zanzibar?

Taarifa umesema pesa za sherehe ya muungano zigawanywe haijasema zigawanywe Kwa uwiano gani.

Hata ikiwa nusu Kwa nusu sawa tu maana muungano ni wa nchi mbili zilizokuwa na hadhi Sawa.
 
Ili kupata maelezo sahihi kwanza ni lazima kujibu swali je Zanziba NI NCHI? Jibu la swali hilo ndo linaamua protocol iweje.
 
Muulize mbunge wako uliyemchagua hayo maswali. na kwa Maneno ya Kiswahili Raisi ni Mkubwa kuliko makamo wa raisi hata ukubadilisha kwa lugha za kigeni, hata kwenye hafla za kimataifa ndio utaratibu
Tunajadili Rais wa nchi na Makamu wa Rais wa nchi. Zanzibar siyo nchi bali ni sehemu ya nchi ya Tanzania. Tofauti ya Rais wa Zanzibar na wakuu wa mikoa wengine wa Tanzania Bara (Tanganyika) ni kuwa Rais wa Zanzibar ana mamlaka ya ndani ya Zanzibar wakati wakuu wa mikoa hawana mamlaka hayo.
 
Mama anajua sana sema ana mapenzi tu na Zenji. Wakati analengwa na wanasiasa wa Zanzibar kuwa anataka kugombea Urais wa 2020, ilibidi atoe kauli "Mimi sina mpango wa kugombea Zanzibar kwa Muundo wa serikali Mimi ni namba mbili itakuaje nije nigombee cheo cha chini kuliko nilicho nacho?
 

Hili mbona ni dogo, natamani huyo mama achote pesa tena za Tanganyika akajenge miradi ya nguvu huko Zanzibar. Na kwenye kuchota hizo pesa asijadiliane chochote na wapuuzi wa huku Bara. Na huyo mama akifanya hivyo tutamuita mzalendo na kutaka aongezewe muda wa kukaa madarakani.
 
Hamna cha protocol bali upuuzi mtupu. Magufuli alikuwa anafanya anachotaka na alikuwa anaonekana wa maana. Ni hivi, kila zama na kitabu chake, huyo mama afanye atakalo maana tumeacha katiba yetu kufanyiwa chochote na rais.
 
Waache watanganyika waendelee kulala fofofo wakiendelea kupingana wao wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…