Tunaona kuwa Rais wa Zanzibar ana mamlaka ya kuwateua maofisa wa TPDF / JWTZ kuongoza vikosi maalum vya usalama, ulinzi na valantia. Makamu wa Rais wa Muungano hana nafasi hiyo bila kukasimiwa na Rais wa Muungano

Toggle navigation
President's Office and Chairman of Revolutionary Council, Zanzibar
MEDIA » NEWS AND EVENTS
Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka Makamanda wapya aliowateua waende wakajenge na kurudisha nidhamu katika vikosi hivyo

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Commodore Azana Hassan Msingiri kuwa Mkuu wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM) hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka Makamanda wapya aliowateua kuwa Wakuu wa Vikosi Maalum vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,waende wakajenge na kurudisha nidhamu katika vikosi hivyo.Hafla hiyo ilifanyika Ikulu Jijini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamo wa Kwanza wa Rais Othman Masoud, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar Othman Makungu, Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama, viongozi wa dini, watendaji wa Serikali na wanafamilia.
Alisema kwamba Jeshi ni nidhamu na ikikosekana nidhamu hakuna Jeshi, hivyo, nidhamu ilitetereka katika vikosi na ndipo alipoamua kuwachangua Makamanda hao ili walete uzoefu wao wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania.Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa aliona haja na sababu ya kuwatumia Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania ili waweze kuiweka nidhamu katika vikosi vya SMZ.
Aliwapongeza Wakuu wote wa Vikosi aliowaapisha hivi leo na kutaka wakafanye kazi kwa bidii na kuwataka askari na Maafisa wote wa vikosi vya SMZ kutokuwa na wasiwasi kwani lengo lake ni kujenga ili vikosi viwe madhubuti, vilivyowezeshwa na kuwa na mafunzo ya kutosha.Mapema Rais Dk. Mwinyi ambaye pia, ni Mkuu wa Vikosi hivyo kabla ya kuwaapisha Wakuu hao kwa mujibu wa Sheria aliwapaindisha vyeo vya Ukuu wa Vikosi hivyo ya SMZ.
Pia, alitumia fusra hiyo kumshukuru Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi Kamanda Simon Siro kwa kukubali pendekezo lake la kuwateua Makamanda hao na kusisitiza kwamba yeye alikuwa na lengo la kutafuta viongozi na sio wataalamu kwani anachotaka ni viongozi na si fani zao.
Walioapishwa katika hafla hiyo ni Kanali Azana Hassan Msingiri kuwa Mkuu wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM), Kanali Makame Abdallah Daima kuwa Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU), Kanali Rashid Mzee Abdallah kuwa Kamishna wa Kikosi cha Zimamoto na Ukozi.
Wengine ni Luteni Kanali Khamis Bakari Khamis kuwa Kamishna wa Vyuo vya Mafunzo, Luteni Kanali Burhani Zubeir Nassoro kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Uratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya pamoja na ACP Ahmed Hamis Makarani kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi (ZAECA)
Source :
Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka Makamanda wapya aliowateua waende wakajenge na kurudisha nidhamu katika vikosi hivyo | Presidents Office Zanzibar