Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Leo amesikika Rais Samia akisema kuwa aliruhusu mikutano ya vyama vya siasa. Hiyo sentensi moja tu inamaanisha Rais Samia hajui katiba inasema nini juu ya mikutano ya vyama vya siasa?
Mikutano ya vyama vya siasa kwa vyama vyote vya siasa ni haki ya kikatiba, na wala siyo hisani ya Rais au CCM.
Tunachojua ni kuwa ofisi ya Rais ilikengeuka na kukiuka katiba ya nchi kwa kuzuia mikutano ya vyama vya siasa, baadaye ofisi hiyo ya Rais ilerejewa na ufahamu na kufuta amri batili.
Kama anaamini ana mamlaka ya kufuta haki za kikatiba, afute, afanye kila kitu kwa matakwa na utashi wake. Watu nao wapambane kwa namna wanazojua dhidi ya mkiukaji wa katiba.
Rais anasema kuwa eti wenzake ndani ya CCM walimshauri asiruhusu mikutano ya vyama vya siasa. Kama kweli kuna majitu ya namna hiyo ndani ya CCM basi hayo ni majuha na maadui wakubwa wa Taifa. Kila mzalendo, bila ya kujali ni wa chama gani au hana chama, ni lazima apiganie utekelezaji wa haki za kikatiba.
Kama Rais anaona kweli anatukanwa kupitia mikutano ya vyama vya siasa, sheria zipo. Kwa nini wanaomtukana wasishtakiwe? Lakini kamwe asiseme kuwa eti yeye ndiye ameruhusu mikutano ya vyama vya kisiasa. Mikutano ya kisiasa imeruhusiwa na katiba, haijaruhusiwa na Rais. Marehemu kwa ubabe tu aliamua kukiuka katiba, na Samia alipochukua madaraka akaendeleza ukiukaji wa katiba kwa muda.
Labda kwa sababu Rais alisema kuwa katiba ni kajitabu tu, ndiyo maana anaona yupo juu ya katiba.
Tukikubali kauli potofu kama aliyoitoa leo Rais Samia, kuna siku tutaweza hata kuambiwa kuwa, nimewaruhusu muendelee kuishi, lakini mnanikosoa!!