Rais Samia aanza kutoa Fedha bilioni 75.98 kwa Vijana na Wanawake kupitia Halmashauri za Wilaya. Hii ni Fursa, tuchangamkie

Wewe umeleta hii habari kiuchawachawa ndio maana lazima tuwasulubu. Samia hana pesa yoyote ya kumpa mtu isipokuwa sisi wananchi ndio tunamlipa yeye hela.
 
Umeeleweka kaka.
 
Taifa na watu wake lazima wawe na Sera ya kuiheshimu serikali na mamlaka yake. Tuweni wazalendo....Tanzania ni moja na Tanzania ni yetu site.
Uko sahihi Kaka pembe , Watanzania lazima tujifunze kuipenda nchi yetu, Watanzania lazima tujifunze kuheshimu viongozi waliopo madarakani kwa mujibu wa Sheria na Katiba ya nchi, hakuna Tanzania nyingine zaidi ya hii tuliyonayo sasa
Wanamkopesha mwanafunzi wa chuo mpaka milioni 20. Wanashindwa mkopesha Mwanafunzi milioni 5 huyo huyo uraiani akajiajiri.
Chivundu Halmashauri zinakopesha vikundi mpaka milioni 100, nenda Halmashauri utapata elimu kuhusu hili
 
Uko sahaihi kabisa Kaka pembe , lazima watu wajifunze kuheshimu mamlaka, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiye nembo ya Nchi, ndiye utambulisho wa nchi, ndiye alama ya Tanzania. Unapotaja Tanzania unataja Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Arusha kuna Mkurugenzi wa halmashauri alizitafuna hizi pesa mwaka jana wakati Samia na awamu yake ya sita wakiwepo. Huko Temeke pia zilitafunwa.
Ndugu mleta mada hizo pesa zinatafunika kirahisi sana tena kipindi hichi cha huyo Samia wenu ndiyo kabisaaa watu hawaogopi chochote. Ni kama kucheza ngoma na joka kibisa, haling'ati na halina sumu.
 
Ngoja nijaribu kufuatilia, tatizo watendaji halmashaur tangu Magufuli atutoke wananyodo ka miungu watu.

Ukiingia kwenye ofisi zao wanakuona ka nuksi.
 
Nimeshawahi kunufaika na huo mkopo. Tatizo mkichukua hamfanikiwi wote. Mfano sisi tulikuwaga watano, tukafanikiwa wawili. Watatu walifeli kwa sababu
  • Walianzisha biashara mpya ambazo hawakuwa na uzoefu nazo
  • Gharama za kuanzisha biashara kama kodi zilitegemea mkopo
  • Licha ya kuwa biashara zilikuwa changa, lakini ndio ziligeuka kuwa chanzo cha mapato ya kuendeshea maisha kwa 100%

MAONI YANGU
Kijana ukiona una uwezo na una biashara hata kama ni ndogo, tafuta vijana wenzako ambao tayari wana vibiashara. Hii itawasaidia ninyi wote kulipa mkopo kwa wakati au kabla ya wakati na hatimaye kupata mkopo mkubwa zaidi tena kwa haraka.
 
Unatengeneza tatizo halafu ukiliondoa unajiita unazo akili.. nyie lumumba buku saba ni matakataka kabisa.
Hakuna aliyetengeneza tatizo, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha sheria ya bajeti, lakini baada ya kusikia maoni ya watu, na kwa kuwa Serikali ya awamu ya Sita ipo kwa ajili ya Watu,imesikiliza maoni ya watu
 
Hakuna aliyetengeneza tatizo, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha sheria ya bajeti, lakini baada ya kusikia maoni ya watu, na kwa kuwa Serikali ya awamu ya Sita ipo kwa ajili ya Watu,imesikiliza maoni ya watu
Wabunge wale ni wa ccm, hilo wazo walilitoa wapi la kuanzisha tozo?
 
Ngoja nijaribu kufuatilia, tatizo watendaji halmashaur tangu Magufuli atutoke wananyodo ka miungu watu.

Ukiingia kwenye ofisi zao wanakuona ka nuksi.
Mkuu Trinity fuatilia, haya mambo ya kusikia kwa watu hayana ukweli, Mkuu ukifika Halmashauri usipolizika namna ulivyohudumiwa nenda kwa Mkurugenzi au kwa DC jambo lako litatatuliwa, kuna weza kuwa kuna matatizo ya kibinadamu lakini ukweli Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya wanajitahidi saana kuwahudumia Wananchi
 
Si zitakuwa kama zile za Halmashauri ya Temeke waligawana wenyewe viongozi wa CCM na hawajarejesha hata senti!!
 
Wabunge wale ni wa ccm, hilo wazo walilitoa wapi la kuanzisha tozo?
Execute Lile sio bunge la CCM, ni bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Turudi pale Rau Madukani umetoa ushuhuda mzuri saana, ni kweli huwa kuna kuwa na changamoto muda mwingine wakati wa kurejesha mikopo hii hasa pale amabapo baadhi ya wajumbe wanakikundi wanapotumia mikopo hiyo sio kwa malengo waliyoombea, Serikali imeendelea kuwawezesha Maafisa Maendeleo na Maafisa Biashara katika ngazi za Wilaya ili waweze kutoa elimu kwa Wanufaika wa mikopo hii namna bora ya kuweza kuhakikisha mikopo wanayotoa inakuwa na manufaa na hatimaye vikundi viweze kurejesha
 
Jidanganye. Naona unalichuma janga....utalila mwenyewe. Endelea kufikiria Rais ni MTU wa kumtukana hivyo kila ukishiba makande. You not very far nor safe. Trust me.
Tulia we kilaza unamtishia nani mpuuzi mmoja tu huna lolote. Wapi kamtukana Rais?
 
Saizi mikopo hii inatolewa kupitia mfumo wa PPL MIS, hakuna ujanja ujanja wowote unaoweza kufanyika, hakuna mtu anayeweza kupewa mikopo hii kama hana sifa zinazotakiwa.
Si zitakuwa kama zile za Halmashauri ya Temeke waligawana wenyewe viongozi wa CCM na hawajarejesha hata senti!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…