Rais Samia aanza kutoa Fedha bilioni 75.98 kwa Vijana na Wanawake kupitia Halmashauri za Wilaya. Hii ni Fursa, tuchangamkie

Rais Samia aanza kutoa Fedha bilioni 75.98 kwa Vijana na Wanawake kupitia Halmashauri za Wilaya. Hii ni Fursa, tuchangamkie

masai dada Mikopo hii inatolewa kupitia Halmashauri zote nchini, na unapitia kwa Mafisa Maendeleo waliopo katika kata na ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri, mikopo hii haina riba na inatolewa kwa vikundi vya Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu.
Fika ofisi ya Halmashauri ulipo au ofisi ya Kata uonane na Afisa Maendeleo wao ndio watakupa muongozo, Mikopo hii haina usumbufu na wala haina riba, Washauri Wanawake pamoja na Vijana wachangamkie fursa hii.
Special requirements
Tufanye general tu.
Hao vijana katika kundi wawe na vingezo gani?
Au kila halimashauri na jambo lake
 
Tatizo urasimu mwingi sana. kupata hizo pesa ni kipengele kizito sana, zinaishiaga kwa wakubwa na wanao fahamiana huko juu
National Anthem mikopo hii kwa sasa inasimamiwa vizuri, utaratibu mpya wa kutoa mikopo hii umeanza toka mwaka wa fedha uliopita, mikopo hii inatolewa bila upendeleo wowote, hakuna mkubwa wala nani anayeweza kula fedha hizi, nenda ofisi ya Halmashauri ulipo, utapewa utaratibu na utakuja hapa kushuhudia ukweli.
 
Mkuu Tindo amini kwamba mikopo hii haina usumbufu wowote kwa sasa Serikali imeazisha utaratibu mzuri kuhakikisha hakuna usumbufu wala upendelo wowote katika kutoa, Shauri vijana wenzetu twende kwenye ofisi za Wakurugenzi au hata ofisi za Kata kwa Maafisa Maendeleo Wajamii utapata elimu ya kuazisha kikundi na vijana wenzio na kuwezeshwa mikopo hii, maneno ya vijiweni kuwa kuna usumbufu sio kweli

Ni kweli mimi sijaenda na wala sina hamu ya kwenda maana huo usumbufu huwa naufahamu. Isitoshe sina card ya ccm. Ngoja niwajulishe vijana wa CCM wakachukue hizo hela. Acha mimi niendelee kutafuta zangu za halali.
 
Special requirements
Tufanye general tu.
Hao vijana katika kundi wawe na vingezo gani?
Au kila halimashauri na jambo lake

Special requirements
Tufanye general tu.
Hao vijana katika kundi wawe na vingezo gani?
Au kila halimashauri na jambo lake
Ni mnajiunga kwenye kikundi kisichopungua watu watano (Kama sio watu wenye ulemavu), kisha mnajisajili katika mfumo wa PPL MIS, then mtapata cheti cha usajili na baada ya hapo mnaweza fanya maombi ya mkopo kwenye mfumo, ni rahisi hakuna ubabaishaji, kikubwa ni mkopo mnao omba uwe ni kwa ajili ya ujasiliamali, fedha hizi ni mkopo usio na riba hivyo lazima zirudishwe ili waweze kunufaika na vijana wengine.
 
Ni kweli mimi sijaenda na wala sina hamu ya kwenda maana huo usumbufu huwa naufahamu. Isitoshe sina card ya ccm. Ngoja niwajulishe vijana wa CCM wakachukue hizo hela. Acha mimi niendelee kutafuta zangu za halali.
Tindo mikopo hii haina uhusiano na mambo ya chama wala siasa, hakuna kigezo cha kadi ya chama wala hayo mambo yenu, kama hujaenda wala hujawahi kwenda unasemaje kuna usumbufu, lets be positive, tuache kuamini mambo ya mtaani yasiyo na ukweli
 
National Anthem mikopo hii kwa sasa inasimamiwa vizuri, utaratibu mpya wa kutoa mikopo hii umeanza toka mwaka wa fedha uliopita, mikopo hii inatolewa bila upendeleo wowote, hakuna mkubwa wala nani anayeweza kula fedha hizi, nenda ofisi ya Halmashauri ulipo, utapewa utaratibu na utakuja hapa kushuhudia ukweli.
sawa acha nifike nione
 
Tindo mikopo hii haina uhusiano na mambo ya chama wala siasa, hakuna kigezo cha kadi ya chama wala hayo mambo yenu, kama hujaenda wala hujawahi kwenda unasemaje kuna usumbufu, lets be positive, tuache kuamini mambo ya mtaani yasiyo na ukweli

Mimi sihitaji hiyo mikopo ya serikali, sijui CCM au ya mama Samia. Ngoja niwajulishe wenye uhitaji wa hiyo mikopo boss, ambao wengi ni wanaccm.
 
Wanamkopesha mwanafunzi wa chuo mpaka milioni 20. Wanashindwa mkopesha Mwanafunzi milioni 5 huyo huyo uraiani akajiajiri.
 
Kwahiyo ametoa huyo Samia au ni fedha za serikali zinazotolewa kwa kufuata bajeti iliyopitishwa na bunge?
Heshimu mamlaka. Samia ni Amiri jeshi mkuu na ndiye kiongozi wa serikali. Ikitoa serikali,ametoa yeye. Tumempa majukumu hayo kikatiba.
Usiandike upuuzi kwa kumkashifu Rais wa nchi ukadhani jf ni mbinguni.
By the way baadhi ya mods humu JF ni watu wa deep state....utachomolewa kama jino bovu na hutarudi kuja kumnanga Mh.Rais humu. Watch out
 
Wewe kichaa hivi vitisho umevitoa kwenye sheria ipi? Shwain pumbavu.
 
Tindo mikopo hii haina uhusiano na mambo ya chama wala siasa, hakuna kigezo cha kadi ya chama wala hayo mambo yenu, kama hujaenda wala hujawahi kwenda unasemaje kuna usumbufu, lets be positive, tuache kuamini mambo ya mtaani yasiyo na ukweli
Je, hao vijana wanatakiwa wawe tayari na shughuli ya ujasiriamali wanayoifanya au hata kama hawana shughuli watapewa tu hizo hela..?
 
Wewe kichaa hivi vitisho umevitoa kwenye sheria ipi? Shwain pumbavu.
Jidanganye. Naona unalichuma janga....utalila mwenyewe. Endelea kufikiria Rais ni MTU wa kumtukana hivyo kila ukishiba makande. You not very far nor safe. Trust me.
 
Jidanganye. Naona unalichuma janga....utalila mwenyewe. Endelea kufikiria Rais ni MTU wa kumtukana hivyo kila ukishiba makande. You not very far nor safe. Trust me.
Wewe mpumbavu nioneshe sehemu nimemtukana Samia.
 
Tatizo la ajira kwa Vijana ni tatizo la dunia nzima kwa sasa, tatizo hili linachangiwa pia na hali ya uchumi wa dunia kwa sasa, licha ya jitihada za Serikali inayoongozwa na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuhakikisha uchumi unaimarika bado tatizo la ajira ni changamoto ya dunia nzima.

Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa mwaka wa fedha 2022/2023 amepanga kutoa mikopo isiyo na riba kwa Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu jumla ya shilingi bilion 75.98 kupitia Halmashauri za Wilaya, fedha hizi zitasaidia saana Vijana kuazisha miradi ili kujikwamua na kuoongeza fursa mbalimbali, Vijana watakaopata fedha hizi wanaweza kuajiri vijana wenzao na kuchangia kwenye pato la nchi.

Fedha hizi za mikopo zimeshaanza kutolewa kwenyebHalmashauri zote kupitia Maafisa Maendeleo wa Halmashauri husika katika Ofisi za Wakurugenzi. Vijana twende tukapate mikopo hii isiyo na masharti magumu na haina riba. Vijana wenzangu tukipata mikopo hii tukumbuke kurejesha ili kuwezesha Vijana wenzetu pia waweze kunufaika na Mikopo hii.

Kwa mwaka wa fedha uliopita (2021/2022) Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitoa jumla ya shilingi bilioni 59,236,353,909.00 kama Mikopo isiyo na riba kwa Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu,. Kupitia fedha hizo tumeshuhudia Vikundi vingi vikifanikiwa kuazisha miradi mbali mbali na kuweza kutoa ajira kwa vijana wenzao ikiwa ni pamoja na kuchangia katika pato la nchi,

Kuna kikundi cha vijana Dar Es Salaam kilipata mkopo na kufanikiwa kuazisha Kituo cha Afya/ Zahanati ambacho kwa sasa sio kinasaidia tu kutoa huduma kwa Watanzania bali kimetoa ajira kwa Vijana hao na wenzao.

Ukienda Wilaya ya Rufiji maeneo ya Ikwiriri kuna kikundi kilinufaika na mikopo hii kinajihusisha na uselemala, kimekuwa kikundi kikubwa kwa sasa, wanatengeneza fanicha kama pale keko, nimeshuhudia si mara moja Wafanyabiashara wa keko wa fanicha wakienda kuchukua vitanda na fanicha nyingine bora kabisa pale ikwiriri kutoka kwenye kikundi hiki, kikundi hiki kimeweza kutoa ajira kwa vijana wengi (sina takwimu halisi) lakini ukifika kwenye eneo la kazi yao utakuta zaidi ya vijana 100 wakiwa wamejiajiri kutoka na uwezeshwaji wa mikopo hii isiyo na riba.

Niliwahi kuona pia kikundi cha Vijana waliojiajiri na kilimo cha umwagiliaji hapo Rufiji, Vijana hao ni Wasomi kabisa na wanafanya vizuri, wamepata elimu nzuri kutoka kwa Watalaamu kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji, sio rahisi kutaja vikundi vyote lakini ni wazi mikopo hii imekuwa mkombozi kwa Vijana wengi.

Kuna kijiji nilienda huko Rufiji kila kijana ana piki piki anayotumia kwa shughuli zake za kilimo na wengine wanatumia kwa shughuli za biashara, lakini nilipouliza nini kipo nyuma ya mafanikio haya nikaambiwa ni kutokana na uwezeshaji wa kiuchumi kwa Wananchi unaofanywa na Serikali kupitia mikopo isiyo na riba, vijana wanamashamaba ya korosho na ufuta.

Huko kusini, kuna kikundi cha Mazingira kupitia mikopo hii Wameweza kununua mpaka gari (Scania) la zaidi ya milioni 120 kutokana na mikopo hii ya kuwezesha Wananchi kiuchumi.

Manufaa ya mikopo hii ni mengi, Vijana twende Halmashauri tukapate Elimu, Halmashauri zina Watalaamu wa kila nyanja, Halmashauri zinaweza saidia kupata vifaa kama vya kuazishia viwanda vya tofali etc..

Vijana tutoke kwenye mitandao kwenye kutukana watu na kukejeli, wale wanaokejeli na kupinga kila jitihada za Serikali msiwasikilize wana watu wanaowalipa kwa kazi hizo, Serikali iko macho, inaona.

Mungu ibariki Tanzania.

Mungu mbariki Raisi wa Jamhuri wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan.
Chawa wa kizungu wewe, ametoa kwenye mshahara wake?
 
Back
Top Bottom