Rais Samia aanza kutoa Fedha bilioni 75.98 kwa Vijana na Wanawake kupitia Halmashauri za Wilaya. Hii ni Fursa, tuchangamkie

Rais Samia aanza kutoa Fedha bilioni 75.98 kwa Vijana na Wanawake kupitia Halmashauri za Wilaya. Hii ni Fursa, tuchangamkie

Tatizo urasimu mwingi sana. kupata hizo pesa ni kipengele kizito sana, zinaishiaga kwa wakubwa na wanao fahamiana huko juu
Mkuu National Anthem umeshaenda ukapata changamoto katika mikopo hii? mikopo hii kwa sasa inatolewa kupitia mfumo, hakuna urasimu wala usumbufu wowote, hakuna namna kiongozi yeyote yule anayekula hizo fedha. Maneno ya mtaani hayana ukweli
 
Naenda jumatatu nitaleta mrejesho.. naenda na vitendea kazi ( vinasa sauti na vipiga picha )
 
umetumia uhuru wako kutoa maoni yako, lakini haina sababu kuitana wapuuzi, unaweza jenga hoja na mtu akaelewa bila kumuita mpuuzi
We kaka unakera saaana.Kwanza kusema sa100 katoa fedha ni uchawa wa kiwango cha flyover au sgr.pili nenda mtaani tafuta vijana waloopata ndo ufungue Uzi vinginevyo unajiaibisha na kuiaibisha familia yako.tunajua kila kitu huwezi pata fedha kirahisi hivyo fedha ni ngumu.
 
Hii pesa kuipata ni kazi ngumu hadi haina maana tena. Niliwahi kufuatilia mwisho wa siku nikaona ni upumbavu tu nafanya.
 
Rais Samia Ni mkombozi wa vijana na zawadi kwa watanzania wote aliyedhamilia kubadilisha na kuinua maisha ya mtanzania mnyonge, Hakuna anayeachwa nyuma Wala kusahaulika na juhudi za Rais wetu mpendwa, kazi iendeleee
 
Kijana Execute uwe na Heshima, heshima ni kitu cha bure, mtu aliyestarabika ni yule anayeweza kuheshimu watu huku amejificha nyuma ya keyboard kama wewe, Nimesema Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan.
Jibu swali acha porojo Samia ametoa wapi pesa?
 
Kijana Execute uwe na Heshima, heshima ni kitu cha bure, mtu aliyestarabika ni yule anayeweza kuheshimu watu huku amejificha nyuma ya keyboard kama wewe, Nimesema Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan.
Ungekuwa na akili ungesema ni serikali ila kwa vile wewe ni mpumbavu unasema Sa100 katoa. Huu ni upumbavu mwingine
 
Mkuu Tindo amini kwamba mikopo hii haina usumbufu wowote kwa sasa Serikali imeazisha utaratibu mzuri kuhakikisha hakuna usumbufu wala upendelo wowote katika kutoa, Shauri vijana wenzetu twende kwenye ofisi za Wakurugenzi au hata ofisi za Kata kwa Maafisa Maendeleo Wajamii utapata elimu ya kuazisha kikundi na vijana wenzio na kuwezeshwa mikopo hii, maneno ya vijiweni kuwa kuna usumbufu sio kweli
Wewe umechukua huo mkopo? Ungekuwa umechukua ungekuwa busy na wala usingekuwa unashinda humu kusifu na kuabudu as if utafanya kazi hii ya kusifu na kuabudu miaka yako yote. Serikali zinabadilika, walikuwepo wenzio kina Musiba, sasa yuko wapi?
 
Nimeshawahi kunufaika na huo mkopo. Tatizo mkichukua hamfanikiwi wote. Mfano sisi tulikuwaga watano, tukafanikiwa wawili. Watatu walifeli kwa sababu
  • Walianzisha biashara mpya ambazo hawakuwa na uzoefu nazo
  • Gharama za kuanzisha biashara kama kodi zilitegemea mkopo
  • Licha ya kuwa biashara zilikuwa changa, lakini ndio ziligeuka kuwa chanzo cha mapato ya kuendeshea maisha kwa 100%

MAONI YANGU
Kijana ukiona una uwezo na una biashara hata kama ni ndogo, tafuta vijana wenzako ambao tayari wana vibiashara. Hii itawasaidia ninyi wote kulipa mkopo kwa wakati au kabla ya wakati na hatimaye kupata mkopo mkubwa zaidi tena kwa haraka.
Ivi ningependa niulize mfano mmepewa mkataba wa miaka miwili na muda umepita na deni halijaisha je hatua zipi zinafuata?
 
Ule mkopo mkataba wake ni mwaka mmoja tu. Inabidi mchaguane vijana mnaoaminiana ili mmalize kwa muda husika. Mkifanya hivyo mkopo wa pili mnapewa haraka. Kuna baadhi huwa wanakopeshwa hadi bajaji. Shida ya baadhi ya watanzania kile kipato cha siku anachukulia kama faida, anakula chote anaacha ya mafuta tu.
Mwisho wa siku chombo kinaharibika, unakuta mhusika hana hela ya matengenezo na marejesho yanahitajika.
 
Hizo fedha zinatolewa kwa UVCCM na siyo vijana wote nchi hii.
Nilishashuhudia wana-CCM wakiitana serikali ya mtaa Salasala,Dar es salaam wakimwita jamaa yangu akachukue pesa japo hana Biashara yoyote.
 
Ule mkopo mkataba wake ni mwaka mmoja tu. Inabidi mchaguane vijana mnaoaminiana ili mmalize kwa muda husika. Mkifanya hivyo mkopo wa pili mnapewa haraka. Kuna baadhi huwa wanakopeshwa hadi bajaji. Shida ya baadhi ya watanzania kile kipato cha siku anachukulia kama faida, anakula chote anaacha ya mafuta tu.
Mwisho wa siku chombo kinaharibika, unakuta mhusika hana hela ya matengenezo na marejesho yanahitajika.
ndo maana mkuu nimeuliza je ikiwa upo nje ya mkataba halmashauri wanachukua hatua gani kwa wana kikundi?
 
Kusema kweli tatizo ni viongozi wa juu wanatia masharti ya ajabu kuchukua mikopo hasahasa afisa maendeleo kata ya segerea, yaani mtu unaunda kikundi unahangaika zaidi ya miezi 3 mpaka unakataa Tama kuomba mkopo.
System ni mbovu mno, bila connection au rushwa, sidhani kama unaweza pata mkopo.
Mi nimeghairi kabisa
 
Tatizo la ajira kwa Vijana ni tatizo la dunia nzima kwa sasa, tatizo hili linachangiwa pia na hali ya uchumi wa dunia kwa sasa, licha ya jitihada za Serikali inayoongozwa na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuhakikisha uchumi unaimarika bado tatizo la ajira ni changamoto ya dunia nzima.

Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa mwaka wa fedha 2022/2023 amepanga kutoa mikopo isiyo na riba kwa Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu jumla ya shilingi bilion 75.98 kupitia Halmashauri za Wilaya, fedha hizi zitasaidia saana Vijana kuazisha miradi ili kujikwamua na kuoongeza fursa mbalimbali, Vijana watakaopata fedha hizi wanaweza kuajiri vijana wenzao na kuchangia kwenye pato la nchi.

Fedha hizi za mikopo zimeshaanza kutolewa kwenyebHalmashauri zote kupitia Maafisa Maendeleo wa Halmashauri husika katika Ofisi za Wakurugenzi. Vijana twende tukapate mikopo hii isiyo na masharti magumu na haina riba. Vijana wenzangu tukipata mikopo hii tukumbuke kurejesha ili kuwezesha Vijana wenzetu pia waweze kunufaika na Mikopo hii.

Kwa mwaka wa fedha uliopita (2021/2022) Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitoa jumla ya shilingi bilioni 59,236,353,909.00 kama Mikopo isiyo na riba kwa Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu,. Kupitia fedha hizo tumeshuhudia Vikundi vingi vikifanikiwa kuazisha miradi mbali mbali na kuweza kutoa ajira kwa vijana wenzao ikiwa ni pamoja na kuchangia katika pato la nchi,

Kuna kikundi cha vijana Dar Es Salaam kilipata mkopo na kufanikiwa kuazisha Kituo cha Afya/ Zahanati ambacho kwa sasa sio kinasaidia tu kutoa huduma kwa Watanzania bali kimetoa ajira kwa Vijana hao na wenzao.

Ukienda Wilaya ya Rufiji maeneo ya Ikwiriri kuna kikundi kilinufaika na mikopo hii kinajihusisha na uselemala, kimekuwa kikundi kikubwa kwa sasa, wanatengeneza fanicha kama pale keko, nimeshuhudia si mara moja Wafanyabiashara wa keko wa fanicha wakienda kuchukua vitanda na fanicha nyingine bora kabisa pale ikwiriri kutoka kwenye kikundi hiki, kikundi hiki kimeweza kutoa ajira kwa vijana wengi (sina takwimu halisi) lakini ukifika kwenye eneo la kazi yao utakuta zaidi ya vijana 100 wakiwa wamejiajiri kutoka na uwezeshwaji wa mikopo hii isiyo na riba.

Niliwahi kuona pia kikundi cha Vijana waliojiajiri na kilimo cha umwagiliaji hapo Rufiji, Vijana hao ni Wasomi kabisa na wanafanya vizuri, wamepata elimu nzuri kutoka kwa Watalaamu kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji, sio rahisi kutaja vikundi vyote lakini ni wazi mikopo hii imekuwa mkombozi kwa Vijana wengi.

Kuna kijiji nilienda huko Rufiji kila kijana ana piki piki anayotumia kwa shughuli zake za kilimo na wengine wanatumia kwa shughuli za biashara, lakini nilipouliza nini kipo nyuma ya mafanikio haya nikaambiwa ni kutokana na uwezeshaji wa kiuchumi kwa Wananchi unaofanywa na Serikali kupitia mikopo isiyo na riba, vijana wanamashamaba ya korosho na ufuta.

Huko kusini, kuna kikundi cha Mazingira kupitia mikopo hii Wameweza kununua mpaka gari (Scania) la zaidi ya milioni 120 kutokana na mikopo hii ya kuwezesha Wananchi kiuchumi.

Manufaa ya mikopo hii ni mengi, Vijana twende Halmashauri tukapate Elimu, Halmashauri zina Watalaamu wa kila nyanja, Halmashauri zinaweza saidia kupata vifaa kama vya kuazishia viwanda vya tofali etc..

Vijana tutoke kwenye mitandao kwenye kutukana watu na kukejeli, wale wanaokejeli na kupinga kila jitihada za Serikali msiwasikilize wana watu wanaowalipa kwa kazi hizo, Serikali iko macho, inaona.

Mungu ibariki Tanzania.

Mungu mbariki Raisi wa Jamhuri wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan.
Kusema kweli tatizo ni viongozi wa juu wanatia masharti ya ajabu kuchukua mikopo hasahasa afisa maendeleo kata ya segerea, yaani mtu unaunda kikundi unahangaika zaidi ya miezi 3 mpaka unakataa Tama kuomba mkopo.
System ni mbovu mno, bila connection au rushwa, sidhani kama unaweza pata mkopo.
Mi nimeghairi kabisa
 
We kaka unakera saaana.Kwanza kusema sa100 katoa fedha ni uchawa wa kiwango cha flyover au sgr.pili nenda mtaani tafuta vijana waloopata ndo ufungue Uzi vinginevyo unajiaibisha na kuiaibisha familia yako.tunajua kila kitu huwezi pata fedha kirahisi hivyo fedha ni ngumu.
@Unitman Huo ni mtazamo wako, Vijana wako mtaani huko wengi wamepata mikopo hii na Wanafanya mambo makubwa, acha kusikiliza maneno yasiyo na ukweli.
 
Hii pesa kuipata ni kazi ngumu hadi haina maana tena. Niliwahi kufuatilia mwisho wa siku nikaona ni upumbavu tu nafanya.
@Mgeni wa Jiji ya juzi siyo ya jana , mambo yamebadilika, saizi unaomba kwenye mfumo , hakuna ubabaishaji,
 
Back
Top Bottom