Rais Samia aendelea kuifungua Tanzania, kuanza ziara ya kikazi Nchini India

Rais Samia aendelea kuifungua Tanzania, kuanza ziara ya kikazi Nchini India

Rais Samia aendelea kuifungua Tanzania, kuanza ziara ya kikazi Nchini India​


Atakaye niwekea kilichoifanya Tanzania kufungiwa, nani aliyoifungia[tusichoshanye, weka sheria iliotamka Tanzania imefungiwa]Tarehe au Siku ilipotangazwa, na kwanini au sababu gani ilifungiwa, nitaweka picha ya Vibwengo wakiendesha Lori.

Haya matamshi yakuwa Tanzania imefunguliwa yanatoka wapi, yanaashiria kitu gani na yana lengo la kutaka nini haswa?

Je, yapo matamshi kuwa Tanzania "imefungwa" au "kufungiwa" mahali popote pale?

e.g Gazeti la Serikali, Waraka wa Bunge, Hukumu ya Mahakama, tamko la Raisi au kitu chochote kile kinachofanana na hayo, kuashiria Tanzania imefungwa?

Kusema Raisi Samia aendelea kuifungua Tanzania ina maana gani haswa kama sio kunyanyasa Wananchi?

Naombeni jibu, tafadhali.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu mpendwa kipenzi cha Watanzania, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi nchini India kuanzia Tarehe 6-11 mwezi huu wa October kwa mualiko maalumu wa Rais wa nchi hiyo. Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Rais ameambatana na wafanyabiashara wakubwa mbalimbali wa Kitanzania, ambao watapata fursa ya kukutana na wafanyabiashara wakubwa kutoka nchi ya India. Pamoja, watafanya mazungumzo ya kibiashara na kuangalia fursa za kibiashara na uwekezaji baina ya nchi zetu hizi mbili.

Mheshimiwa Rais wetu atapata fursa ya kufanya mazungumzo pia na Waziri Mkuu wa India, lakini pia kuzungumza na wafanyabiashara wakubwa kutoka India, katika jitihada ya kuwavutia kufanya biashara na uwekezaji nchini mwetu katika nyanja na sekta mbalimbali. Ikumbukwe kuwa Tanzania na India zimekuwa na mahusiano ya kidiplomasia ya kihistoria na ya muda mrefu sana. India ni miongoni mwa nchi za kwanza kabisa kufungua ubalozi wake hapa nchini katika miaka ya mwanzoni kabisa baada ya kupata uhuru wetu.

Watanzania, tutegemee kupata fursa mbalimbali za ajira kutokana na uwekezaji mkubwa kutoka kwa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka nchini India.

Rais Samia anaendelea kuifungua nchi yetu na kuifungulia fursa mbalimbali za kiuchumi. Tunaendelea kuzoa fursa za kibiashara na uwekezaji kutoka kila kona ya dunia. Tanzania inaendelea kuwa chaguo namba moja la wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa kutoka mataifa mbalimbali. Tuendelee kuchangamkia fursa hizi ambazo zinaletwa na Mheshimiwa Rais wetu, ambaye anakesha akitafuta fursa kwa ajili ya Taifa letu.

Ni kupitia uwekezaji na biashara na wafanyabiashara wakubwa kutoka mataifa mbalimbali ambapo tutapata fursa za ajira, ongezeko la mapato, mapinduzi ya viwanda, kilimo, miundombinu, teknolojia, mapinduzi ya kifikra, na kupaa kiuchumi na kimaendeleo kwa Taifa letu.

Kazi iendelee. Mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana Mzalendo na Mpenda Nchi Yangu.

Simu: 0742-676627
Una elimu gani?

Sent from my Infinix X663 using JamiiForums mobile app
 
Tanzania inashirikiana na India katika mambo mbalimbali sana .India pia limekuwa soko kubwa sana kwa baadhi ya mazao yetu yanayodhalishwa hapa nchini.
Mbona sijawahi kusikia Kiongozi yeyote kutoka bara lingine akija hapa nchini Na kufanya mikutano na wafanyabiashara wetu Wa ndani kwa nia ya kuwavutia kwao?! Tatizo ni nini?; Sisi tumeumbwa kuwavutia wawekezaji kutoka nje lkn sisi siyo wa kuvutiwa huko nje?
Halafu linakuja lipumbavu moja hapa JF kifua mbele kusifia tabia ya kunadinadi nchi yetu
 
Back
Top Bottom