Rais Samia afanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri. Angellah Kairuki aenda TAMISEMI, Balozi Mulamula atemwa, Bashungwa ahamishwa

Mula mula kakosana na mama wapi tena

Huko TWEETER "Kigogo" kamwaga Habari kwamba Waziri kanunua Nyumba Marekani yenye Dhamani ya Dola 1.7M na kufanya Sherehe Siku 4 Mfululizo. Labda hili nalo limechangia Kumwagwa.
 
Bashungwa anatafutiwa sababu atemwe mazima
Hakuna kitu kama hicho Raisi akiamua anaweza kumtengea waziri yoyote muda wowote alijisikia bila kushauriana na mtu yoyote katiba imempa nguvu Raisi, ata leo anaweza kumteua Makonda kuwa mbunge na kumpa uwaziri au anaweza kunichagua mimi kuwa mkuu wa mkoa na hakuna atakaye hoji.
 
Kuteua na kutengua ni jadi yetu Tanzania.

MulaMula alikuwa anafuatilia sana swala la uraia pacha, nadhani hilo ni moja ya yaliyomponza ingawa yanaweza kuwapo mengine.
Mzee mkubwa hebu fafanua kidogo hapo kwenye uraia pacha.
Kuna siri gani mpaka serikali iogope huo mchakato kiasi cha kutimua waziri?
 
Haya mabadiko huwa yanafanywa sijawahi kuona chochote chamaana
 
Pongezi kwa wote walio endelea kubaki.

Jambo la msingi wafanye kazi kwa bidii na kwa maarifa.

Wasijisahau kuwa Mama hufoka kwa KALAMU.........

Chapeni kazi, tatueni kero za wananchi kwani utendaji kazi kwa nia ya dhati bila unafiki ndio utakao wabeba, unafiki na uzandiki hauwezi kuwasaidia.
 
Siku Mwigulu na Makamba aakiondoka nitampongeza Rais kwa kupiga kitimoto roast kilo mbili na Wind hoek bariiiid nne.

Hawa watu wamejaa kiburi na dharau huku utendaji wao ukiwa ni dhaifu, dhaifu mno sijui wamempa nini mama
 
Badala ya kumtumia mwizi Mwigulu, anamtambua mwanamme mwenzake. Huenda Mulamula alikuwa hansifii kama wenzake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…