Rais Samia afanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri. Angellah Kairuki aenda TAMISEMI, Balozi Mulamula atemwa, Bashungwa ahamishwa

Rais Samia afanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri. Angellah Kairuki aenda TAMISEMI, Balozi Mulamula atemwa, Bashungwa ahamishwa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri Kama ifuatavyo:

Amemteua Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Awali Mhe. Dkt.Tax alikuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Aidha, Mhe. Tax anachukua nafasi ya Mhe. Balozi Liberata Mulamula.

Amemteua Mhe. Innocent Lugha Bashungwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Awali Mhe. Bashungwa alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Amemteua Angellah Jasmine Kairuki kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia amemteua kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Mawaziri wote hao walioteuliwa wataapishwa tarehe 03 Oktoba, 2022 saa 3:00 asubuhi Ikulu Jijini Dares Salaam.

View attachment 2375256
Mganga wa Dk. Mwigulu Nchemba si wa mchezo mchezo kwani Kaupiga mwingi kwa Ndumba na Mama Kamsahau kabisa Kumtumbua.
 
TAMISEMI kaamua kuwabadilishia mzembe mwingine tu wakuruhusu uwizi zaidi.

Maana yake wizi unao endelea TAMISEMI una baraka zote wa ‘Bi Tozo‘ sote tunajua uwezo wa Angela Kairuki sasa kumuweka hapo ni sawa na kusema ibeni zaidi.

Huo ndio ukweli wenyewe
 
sjui ni kwanini ila tangu enzi za jpm sielewi mantiki ya hizi teuzi za miezi sita sita. ukikaa ukitazama kwa umakini zimekaa kama nafasi ya kumtega mtu kimahaba kisha mkichukizana umuweke pemebni upate marafiki wengine wa kuwatega
 
Na hizo kucha tunyofolewe lini atatangaza agombei 2025 tupate nafasi za kuwapima wanayoitaka hiyo nafasi.

Atutaki tena biashara ya kuuziwa mbuzi kwenye gunia.
 
sjui ni kwanini ila tangu enzi za jpm sielewi mantiki ya hizi teuzi za miezi sita sita. ukikaa ukitazama kwa umakini zimekaa kama nafasi ya kumtega mtu kimahaba kisha mkichukizana umuweke pemebni upate marafiki wengine wa kuwatega
Uteuzi wa mama ni wa hovyo hovyo sana.
Mawaziri wenye nafuu ni;
1. Maji
2. Kilimo
Basi wengine sijui wanafanya kitu gani.
Tunaibiwa sana kwani wanalipwa kodi zetu
 
Huyo Dr TAX katokea huko huko Civil Services ni mtu wao; Wala hakuna shida kuwa waziri wa mambo nje ni njagu wa zamani.

Wizara ya ulinzi huyu mtu ata hatujui shughuli yake haswa, ila Bashungwa kasomeshwa na serikali nje ya nchi na kurudi kapewa kazi serikalini sasa kama hujui hawa watu huwa ni wa aina gani kazi kwako (tatizo labda wapewe wizara ngumu).

Hila huyu Kairuki TAMISEMI ni maza kutuletea utani tena watanzania.

Huyu Kairuki wa kumpa TAMISEMI hizi sasa dharau.
 
Hivi mbunge akiteuliwa si anatakiwa kula kwanza kiapo cha ubunge?

Halafu, hadi sasa idadi ya wabunge wa kuteuliwa imefikia ngapi? Ukijumlisha wale wa JPM + 19 (Halima mdee et al)

Je, Mulamula anaendelea kuwa mbunge na kupokea posho za ubunge au anarudi kwenye nafasi yake ya hapo awali kabla ya uteuzi?

Tz hakuna kiongozi anayefuata katiba ,kikatiba ni 10 ila anaweza akateua hata 20 hakuna mtu atakayemzuia.
 
Huyo mama Mulamula alikuwa hawashi kiukweli. Yule mama sio mwanasiasa wala sio mwanadiplomasia anafaa kuwa mwanazuo (Academician).
 
Back
Top Bottom