Rais Samia afanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri. Angellah Kairuki aenda TAMISEMI, Balozi Mulamula atemwa, Bashungwa ahamishwa

Rais Samia afanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri. Angellah Kairuki aenda TAMISEMI, Balozi Mulamula atemwa, Bashungwa ahamishwa

Kwa hiyo hajamuona mtu yeyote wa kuimudu TAMISEMI ndani ya bunge hadi akamchukue mtu wa nje?

BTW: Kipindi huyo Mulamula anateuliwa alipambwa humu na akina Kabudi wakaonekana walikuwa amateurs tu kwenye nafasi ile.

Kulikoni mwanadiplomasia mbobevu katemwa ilhali "diplomasia yetu imeimalika kuliko wakati wowote".😁
 
Bashungwa !!


Wizara ya Ulinzi, ikashikwaje na Mwanamke ??? Daaahhh
We jamaa, kwani mbona raisi ni mwanamke. Huwa siwaelewi wanaume wanaolalamika wanawake kuwa viongozi wakati wanaume wengi siku hizi ni mchele mchele wengi hufikiria ngono tu, wengine wanakuwa na ushoga, wengine wanalawiti, wengine waizi tu na mapanya road, wengine kukesha kwenye masupu ya pweza na wengine kuzalisha na kuacha masingle mama mtaani yaani kila mahsli ni vurugu za wanaume. Wacha wanawake wachukue nafasi mlizoshindwa kusimamia. Kaeni kwa kutulia mnyolewe dizaini yenu!
 
Kwa hiyo hajamuona mtu yeyote wa kuimudu TAMISEMI ndani ya bunge hadi akamchukue mtu wa nje?

BTW: Kipindi huyo Mulamula anateuliwa alipambwa humu na akina Kabudi wakaonekana walikuwa amateurs tu kwenye nafasi ile.

Kulikoni mwanadiplomasia mbobevu katemwa ilhali "diplomasia yetu imeimalika kuliko wakati wowote".😁
Ya ngoswe muachie ngoswe, hata leo hii ikitokea la kutokea mama akaanguka chali, hizi sifa zote anazopewa zitageuka na kuwa fimbo za kumchapia.

Kwa ufupi hakuna kiumbe mnafiki kama mtanganyika, ndugu zetu wazanzibari kidogo wamestaarabika tofouti na watu wa bara.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri Kama ifuatavyo:

Amemteua Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Awali Mhe. Dkt.Tax alikuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Aidha, Mhe. Tax anachukua nafasi ya Mhe. Balozi Liberata Mulamula.

Amemteua Mhe. Innocent Lugha Bashungwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Awali Mhe. Bashungwa alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Amemteua Angellah Jasmine Kairuki kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia amemteua kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Mawaziri wote hao walioteuliwa wataapishwa tarehe 03 Oktoba, 2022 saa 3:00 asubuhi Ikulu Jijini Dares Salaam.

View attachment 2375256
Kump bashungwa hiyo wizara ni wazi rais hajitambui...
 
Mula mula kakosana na mama wapi tena
Siku nilipomuona Dorothy Gwajima kaanza kuvaa kiremba/ushungi na wanawake wengi kuanzia wakuu wa wilaya nk kuanza kuvaa hii code, nikawaza hivi: "......Mulamula asipojitune kuendana na mdundo wa ngoma hii ataliwa kichwa....." Hahaha mawazo yangu yametimia!
 
Kwani Mula Mula ndio alimlazimisha apande basi kule Wingereza?
 
Back
Top Bottom