Rais Samia Afanya Mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC)

Rais Samia Afanya Mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC)

Kipande cha Mwanza - Isaka kinajengwa na mchina.
Kama hela ipo ya kukikamilisha hicho kipande, si ajabu kitakuwa tayari kabla ya hiki cha Dar - Morogoro, kwani mchina hacheleweshi kazi.
Kipande hiki kitasafirisha mizigo toka Mombasa nchini Kenya mpaka Isaka Tanzania.
Isaka Tanzania kuelekwa Rwanda.
jamani haya madude yanaendeshwa na umeme, tunajitahidi kuupata umeme toka Nyerere Dam Rufiji
vituo vya kutunzia umeme vinajengwa kwenye station za SGR sasa tukachukue umeme ambao hata kwenye migodi hautoshi, bado mizigo tukapitishia Mombasa, ikaingie Ziwa Nyanza ippakuliwe tena mata mbili hapo Isaka.
Namuomba Makamu wa Rais Bw Mpango aanze na Tabora Kigoma ni karibu kabisa na Makutupora na Burundi na DRC wanategemea Kigoma kuliko hao Rwanda wanaotaka kwa lazima Isaka
tutapoteza pesa nyingi mradi usikamilike hata wa Dar Makutupora
 
Ukweli tuseme, huu mradi ukamilishwe kwanza kutoka Dar to Dom na teen lianze Nazi, sasa kwa mtindo huu mbona kukamilika itachukua awam7
 
Reli sawa tuendelee nayo ila si kwa hela za ndaini...mnawatesa watanzania.!!
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzay Mheshimiwa Samia Suluhu leo Mei 22, 2021 amekutana na kufanya Mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania ( TRC) Masanja Kadogosa

Katika mazungumzo hayo muhimu yaliyofanyika Ikulu pamoja na mambo mengine walijadili maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa ( SGR)

Mkurugenzi Mkuu wa TRC alimshukuru sana Mama Samia kwa kuidhinisha fedha tshs bilion 372 kwa ajili ya ujenzi wa reli ya SGR kipande cha kuanzia Mwanza Hadi Isaka chenye urefu wa kilometa 341

Rais Samia alimueleza Mkurugenzi wa TRC kuwa Serikali itahakikisha kuwa Mradi wa SGR utakaounganisha Bandari ya Dar es salaam na Kanda ya Ziwa, Kanda ya Magharibi na Nchi za Uganda, Rwanda, Burundi na DRC unakamilika kwa wakati
Bye bye Kadogosa...kapumzike salama umetoa yako yote ila wenzako wanayo mengi zaidi yako .....asante kwa utumishi wako....
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzay Mheshimiwa Samia Suluhu leo Mei 22, 2021 amekutana na kufanya Mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania ( TRC) Masanja Kadogosa

Katika mazungumzo hayo muhimu yaliyofanyika Ikulu pamoja na mambo mengine walijadili maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa ( SGR)

Mkurugenzi Mkuu wa TRC alimshukuru sana Mama Samia kwa kuidhinisha fedha tshs bilion 372 kwa ajili ya ujenzi wa reli ya SGR kipande cha kuanzia Mwanza Hadi Isaka chenye urefu wa kilometa 341

Rais Samia alimueleza Mkurugenzi wa TRC kuwa Serikali itahakikisha kuwa Mradi wa SGR utakaounganisha Bandari ya Dar es salaam na Kanda ya Ziwa, Kanda ya Magharibi na Nchi za Uganda, Rwanda, Burundi na DRC unakamilika kwa wakati
Halafu kuna majitu majinga humu eti Legacy ya JPM imekufa! Ukiiua Legacy ya JPM maana yake umeiua Tanzania!
 
Hili likiwezekana katika miaka minne hii litaleta heshima kubwa kwa mama.

Lakini hiki kipande cha Dar hadi Morogoro kinaweka sura mbaya. Ujenzi ukiendelea hivi, hata miaka kumi ijayo hiyo reli itakuwa haijafika popote.
Kuna shida gani hicho kipande mpaka kisikamilike? Vipi kuhusu moro- dodoma kimekamilika?
 
Mkurugenzi Mkuu wa TRC alimshukuru sana Mama Samia kwa kuidhinisha fedha tshs bilion 372 kwa ajili ya ujenzi wa reli ya SGR kipande cha kuanzia Mwanza Hadi Isaka chenye urefu wa kilometa 341

Fedha za huu mradi zinaidhinishwa na Bunge au Ikulu?
 
Ingekuwa jambo la Msingi kupeleka SGR kigoma kuliko mwanza
Kipande cha kigoma ni cha kimkakati kuliko mwanza
Si vizuri kufanya mambo kama mwendazake kwamba kila kitu lazima kiende Mwanza hata kama hakina tija
Kumbe kigoma nayo ni sehemu ya Tanzania!
 
Usimshushe Rais kwa kiwango Cha Mkurugenzi was TRC ...ungeandika ..Dg wa TRC AITWA IKULU KUELEZEA MAENDELEO YA SHIRIKA! Mazungumzo😂😂😂 no kwa watu wanaolingana angalau !
 
Ni wakati muafaka Mama akutane na wakurugenzi wa Africa Development Bank, na World Bank wafanye maamuzi, Mashirika hayo yazisaidie Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia na Congo, wafadhili ujenzi wa SGR kwenye nchi hizo na sisi tutazichangia asilimia 45. Simple ratio iwe.
World Bank 35% Loan
ADB 15% Loan
Each Country 5% Self Finance
Tanzania 45% Grant, Masharti, hasa kwa Rwanda na Uganda, waanze kuboresha mifumo ya kidemocrasia ya Uchaguzi na wavipe uhuru vyama vya siasa kutimiza wajibu wao na kuongeza ushiriki wa wanawake katika shughuri za kiuchumi na kisiasa.
 
Ni wakati muafaka Mama akatane na wakurugenzi wa Africa Development Bank, na World Bank wafanye maamuzi, Mashirika hayo yazisaidie Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia na Congo, wafadhili ujenzi wa SGR kwenye nchi hizo na sisi tutazichangia asilimia 50. Simple ratio iwe.
World Bank 35% Loan
ADB 15% Loan
Each Country 5% Self Finance
Tanzania 45% Grant.
Pumbavu huna akili
 
Back
Top Bottom