Rais Samia afanya uteuzi, Kafulila awa Kamishna wa Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP)

Rais Samia afanya uteuzi, Kafulila awa Kamishna wa Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP)

Mwaikibaki

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2015
Posts
3,004
Reaction score
3,695
Wadau,
Mkeka wa teuzi zingine huu hapa na Mstaafu Kafulila amekumbukwa!
3aaa5ad7-012a-468c-ba37-3017b9dd9a14.jpg

962380b7-7173-442f-84d8-22edd6b1dc3b.jpg


=====

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi kama ifuatavyo:-

Amemteua Dkt. Ellen Mkondya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa - Muhimbili. Dkt. Mkondya ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.

Amemteua Bw. Justine Peter Mwandu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Bima la Taifa (NIC). Bw. Mwandu ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Tanzania Reinsurance (TANRE).

Amemteua Prof. Verdiana Grace Masanja kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI). Masanja ni Profesa wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela.

Amemteua Bw. Griffin Venance Mwakapeje kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania. Bw. Mwakapeje alikuwa Mkurugenzi, Idara ya Huduma za Kisheria kwa Umma, Wizara ya Katiba na Sheria. Bw. Mwakapeje anachukua nafasi ya Bw. Casmir S. Kyuki ambaye atamaliza kipindi chake tarehe 07 Januari, 2023.

Amemteua Bi. Fatma Mohamed Abdallah kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Puma Energy Tanzania. Bi. Abdallah ni Meneja wa Kampuni ya Puma Energy nchini Geneva. Aidha, Bi. Abdallah anachukua nafasi ya Dominic Dhanah ambaye amemaliza muda wake.

Amemteua Bw. David Zacharia Kafulila kuwa Kamishna wa Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP). Bw. Kafulila ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mstaafu.

Teuzi hizi zinaanza mara moja.

Pia, soma: Rais Samia Suluhu Hassan afanya uteuzi wake wa kwanza Ikulu. Gerson Msigwa atolewa Ikulu, Dotto James ahamishwa. TPA, TCRA na TRA zapata wakuu wapya
 
Hizi teua tumbua zinazoendelea zitatuletea matatizo. Maana machawa na waimba mapambio wataongezeka sasa ili wateuliwe.
Wale walio na nafasi bado madarakani watakesha wakisifia mpaka mvua kuletwa na mama ili kibarua kisiote nyasi.

Kipindi hiki Magufuli atatukanwa sana ili tu watu waonekane ni watiifu kwa mama.

Kina Ally Hapi wataibuka sasa hivi kusifia hata visivyosifika vya mama ili waonekane na wao.
 
Humu jukwaani walikua wanamponda kua akalime pilipili na nyanya, bora aende huko akakusanye mtaji. Nna uhakika sasa hv hatafanya makosa tena maana fedheha ya kupigwa chini ilikua kubwa
 
Back
Top Bottom