Rais Samia afanya uteuzi: Masauni aondolewa Wizara ya Mambo ya ndani, Kabudi apelekwa Wizara ya Habari na Michezo, Janabi kuwa mshauri wa Rais

Rais Samia afanya uteuzi: Masauni aondolewa Wizara ya Mambo ya ndani, Kabudi apelekwa Wizara ya Habari na Michezo, Janabi kuwa mshauri wa Rais

Suala la wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kupewa nafasi za kisiasa linachochea sana uvunjifu wa amani wakati wa uchaguzi ili kuwafurahisha wanasiasa na kujipendekeza ili wapate uteuzi.
Rais aache kabisa kuwateua na awaache watumike kwenye majukumu yao ya msingi bila kujiingiza kwenye siasa.
kweli haijakaa vizuri..bora marufuku iwekwe kwenye katiba kabisa
 
Nawaza tu maana waliosikiliza Askari Magereza Walivyosikitikia Matendo ya Polisi kwamba waliwafuata na " mabunduki na Mabomu" kama majambazi, hawatashangaa Masauni kuhamishwa

Vinginevyo lingejengeka Bifu la kutisha
 
Huyu atatuulia Rais wetu,hivi kweli mh.Rais anywe maji asubuhi,ale mchana kidogo na usiku asile kitu anywe maji peke yake.....
Lucas Mwashambwa alitakiwa kuupinga huu uteuzi kwa nguvu zake zote. Maana Mama anaenda kushindia maji na viubwabwa kiduchu tu kila siku eti kwa lengo la kulinda afya!!

Hivi ilikuwaje adui wa chakula akateuliwa kwenye hiyo nafasi!!
 
Nawaza tu maana waliosikiliza Askari Magereza Walivyosikitikia Matendo ya Polisi kwamba waliwafuata na " mabunduki na Mabomu" kama majambazi, hawatashangaa Masauni kuhamishwa

Vinginevyo lingejengeka Bifu la kutisha
Hilo sakata ni la Mtwara ambapo alikamatwa askari Magereza akiendesha pikipiki bila helmet.... ndo mkasa mzima
 
Wewe Mzee Mgaya ndiyo hamna kitu kabisa!! Na hao wengine wamehamishwa sababu gani? Usikute mkeka ulishakuwepo kitambo tu! Halafu unatuletea visababu vyako visivyo na kichwa, wala miguu!
 
Wakuu,

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na mabadiliko ya Viongozi mbalimbali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi na mabadiliko ya viongozi hao ni kama ifuatavyo:-

(i) Mhe. Rais Dkt. Samia amehamisha majukumu ya sekta ya habari kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwenda Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ambapo Mhe. Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo;

(ii) Mhe. Jerry William Silaa (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

(iii) Mhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbaro (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria

(iv) Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira);

(v) Mhe. Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi;

(vi) Mhe. Abdallah Hamis Ulega (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi;

(vii) Mhe. Innocent Lugha Bashungwa (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi;

(viii) Bw. Gerson Msigwa ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali;

(ix) Dkt. James Henry Kilabuko ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu)

(x) Dkt. Stephen Justice Nindi ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo anayeshughulikia masuala ya ushirika na umwagiliaji;

(xi) Dkt. Suleiman Hassan Serera amehamishwa kutoka Wizara ya Kilimo kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara.Aidha, Balozi Dkt. John Stephen Simbachawene atapangiwa kituo cha kazi;

(xii) Prof Mohamed Yakub Janabi ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais Masuala ya Afya na Tiba. Aidha, pamoja na nafasi hiyo Prof. Janabi ataendelea kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili

(xiii) Bw. Anderson Gukwi Mutatembwa ameteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa kituo cha kazi;(xiv) Bw. Mobhare Matinyi ameteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa kituo cha kazi;

(xv) Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. Hamad Khamis Hamad ameteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa kituo cha kazi;

(xvi) Kamishna wa Polisi CP. Suzan Kaganda ameteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa kituo cha kazi;

(xvii) Bw. Thobias Makoba aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali ameteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa kituo cha kazi.

Uapisho wa Viongozi walioteuliwa utafanyika Ikulu Ndogo, Tunguu Zanzibar tarehe 10 Desemba, 2024 kuanzia saa 5.00 asubuhi.


Isinge kuwa hii kuangaliana usoni, Masauni alitakiwa aende zake Zanzibar.
Huyu jamaa ame haribu sana jeshi la polisi.
Kila kitu simu ya maagizo.
Polisi hawakuwa waki fanya kazi zao kwa mujibu wa PGO bali kwa maagizo.
Rais ame chelewa sana kumuondoa huyu jamaa.
 
Kama uliamua kusoma ili uwe mwanasiasa juwa kabisa kuwa unaenda kuua kipaji chako,leo utamaduni,kesho sheria,kesho kutwa mambo ya nje,hapo hakuna kitu kabisa,utabakia tu kugangaa njaa ili familia yako iishi...
Hata Prof. Sarungi waliwahi mfanyia hivyo hivyo.

Mtaalmu wa mifupa, akala wizara ya michezo.
 
Back
Top Bottom