Rais Samia afanya Uteuzi na Mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Makatibu Tawala na Kaimu Kamishna (TANAPA)

Rais Samia afanya Uteuzi na Mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Makatibu Tawala na Kaimu Kamishna (TANAPA)

Rais Samia ameteua na kufanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Makatibu Tawala na Kaimu Kamishna (TANAPA).

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemhamisha kituo cha kazi Sixtus Raphael Mapunda kutoka Wilaya ya Sumbawanga kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke akichukua nafasi ya Mobhare Holmes Matinyi ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari - Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali.

Rais Samia pia amemhamisha kituo cha kazi Mkuu wa Wilaya ya Urambo, Kenan Laban Kihongosi kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba Mkoani Songwe akichukua nafasi ya Fakii Raphael Lulandala ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa UVCCM.

Amemteua pia Elibariki Bajuta, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro kuwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora akichukua nafasi ya Kihongosi ambaye amehamishiwa Momba.

Amemteua Nyakia Ally Chirukile kuwa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga ambapo akichukua nafasi ya Sixtus Raphael Mapunda aliyehamishiwa Wilaya ya Temeke, kabla ya uteuzi huu Ndugu Nyakia alikuwa Katibu Tawala wa Ngorongoro.

Hatimaye nimelamba Uteuzi 😁😁
 
Ngorongoro imefumuliwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiki ndio anchoweza KIZIMKAZI anatamani iwe kila wiki. Mm na family yangu pamoja na ukoo wangu tunaona ni Aibu tu. Mambo mazito analeta maneno tu mkeka hatoi. Pole kwa watanganyika
 
Siku hz wanatambulika kama Afisa tarafa
Kwenye taarifa hii kutoka Ikulu kuna sehemu imetaja 'Afisa tarafa' na sehemu nyingine 'katibu tarafa'.

Inamaana hata ikulu haielewi umuhimu wa kutambua cheo/nafasi ya Uongozi?
 
Hivi kwanini lakini ndg yetu na kipenzi chetu Pascal Mayalla hawampi nafasi ktk teuzi zote hizi?!!

Mkuu Pascal Mayalla uliwafanya nini watu wa system? kwanini wanakunyanyapaa ndg yangu?
Jifunze kuwa chawa. Badilika, jishushe na uchague kujipendekeza na kusifia. Ikiwezekana waone wazee wakutambikie. Halafu waganga nao wana nafasi yao ktk safari yako ya kufukuzia teuzi. Hivyo usiwaache sana.

Inshaalah ipo siku jina litatokelezea tu...
Si alisema ataki teuzi alipo panamtosha
 
Hivi kwanini lakini ndg yetu na kipenzi chetu Pascal Mayalla hawampi nafasi ktk teuzi zote hizi?!!

Mkuu Pascal Mayalla uliwafanya nini watu wa system? kwanini wanakunyanyapaa ndg yangu?
Mkuu Kisima , sijawahi kuwafanya kitu chochote, kinachofanyika kwenye vetting, kitu cha kwanza ni kufungua file lako, kitu wanachokutana nacho ni bandiko hili kuwahusu TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!, hata ungekuwa wewe, jina kama hili ungeli forward?.

Kwenye sehemu ya mwenendo wa maisha binafsi, wanakuta taarifa Pasco ni mtu wa viti virefu kwa mwendo wa Joni Mtembezi. Anapenda sana kula, Uliwahi kula vyakula gani kutoka sehemu mbalimbali Duniani ukafaidi? sijui chakula gani hajawahi kula!. Enzi akiwa kijana ni foleni mpaka Feri!, hata ungekuwa wewe, ungefowarward jina kama hili?.

Na wanapozidi kupekua file wanakutana na nyuzi kama hizi Pongezi Zangu ni Bonafide-Genuine! Sisaki Teuzi, Sitaki Teuzi, Niko Naye Mbeya, Nitamweza! wanafunga kabisa faili!.
Jifunze kuwa chawa.
Duh...!, mtu hajawahi kuwa chawa, sasa anelekea 60 ndio aanze kujifunza uchawa!
Badilika, jishushe na uchague kujipendekeza na kusifia.
Ukiwa sio kujipendekeza type ni kutojipendekeza, mimi niko down to earth, kosa langu ni mkweli too much na sijaweza kujigunza kunyamaza.
Ikiwezekana waone wazee wakutambikie. Halafu waganga nao wana nafasi yao
It's very unfortunately, I'm not a believer!
ktk safari yako ya kufukuzia teuzi.
Sijawahi kufukuzia teuzi!. Mfano sasa, macho yote ni 2025 watu wasio na jicho la 3, wanajua 2025 ni Mama, mtu anayefukuzia teuzi anaweza kupandisha bandiko kama hili Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke

Mimi hivi hivi nilivyo kwa capacity yangu kama mwandishi wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea, naweza kumsaidia sana Rais Samia na kulisaidia sana taifa letu bila position yoyote ya uteuzi!.

P
 
Kwa juhudi zako za huku unastahili sasa sijui kama unaifaa nchi au inafaa maslahi binafsi😆
Kuitumikia Nchi sio lazima uteuliwe japo ukiteuliwa ni vyema zaidi na maslahi ya Umma na ya binafsi yote yanatumikiwa Kwa pamoja🔥🔥

Kama bro Pascal
 
Huyo hamza anapelekwa ngorongoro kwenda kuwabeba waarabu na kuwafukuza wamasai
 
Back
Top Bottom