Rais Samia afanya Uteuzi na Mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Makatibu Tawala na Kaimu Kamishna (TANAPA)

Rais Samia afanya Uteuzi na Mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Makatibu Tawala na Kaimu Kamishna (TANAPA)

Hivi kwanini lakini ndg yetu na kipenzi chetu Pascal Mayalla hawampi nafasi ktk teuzi zote hizi?!!

Mkuu Pascal Mayalla uliwafanya nini watu wa system? kwanini wanakunyanyapaa ndg yangu?
Jifunze kuwa chawa. Badilika, jishushe na uchague kujipendekeza na kusifia. Ikiwezekana waone wazee wakutambikie. Halafu waganga nao wana nafasi yao ktk safari yako ya kufukuzia teuzi. Hivyo usiwaache sana.

Inshaalah ipo siku jina litatokelezea tu...
Huyo alishavuka hizo level za uDC,yeye anapambania jimbo,japo wajumbe hawajaridhia
 
Rais Samia ameteua na kufanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Makatibu Tawala na Kaimu Kamishna (TANAPA).

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemhamisha kituo cha kazi Sixtus Raphael Mapunda kutoka Wilaya ya Sumbawanga kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke akichukua nafasi ya Mobhare Holmes Matinyi ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari - Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali.

Rais Samia pia amemhamisha kituo cha kazi Mkuu wa Wilaya ya Urambo, Kenan Laban Kihongosi kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba Mkoani Songwe akichukua nafasi ya Fakii Raphael Lulandala ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa UVCCM.

Amemteua pia Elibariki Bajuta, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro kuwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora akichukua nafasi ya Kihongosi ambaye amehamishiwa Momba.

Amemteua Nyakia Ally Chirukile kuwa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga ambapo akichukua nafasi ya Sixtus Raphael Mapunda aliyehamishiwa Wilaya ya Temeke, kabla ya uteuzi huu Ndugu Nyakia alikuwa Katibu Tawala wa Ngorongoro.

Kilasiku teuzi tu kwani hakuna kingine cha kufanya
 
Hii nchi kwa hapa tulipofikia, tunahitaji haraka Katiba Mpya iliyotokana na wananchi, kabla mambo hayajaharibika kabisa.
 
Hivi kwanini lakini ndg yetu na kipenzi chetu Pascal Mayalla hawampi nafasi ktk teuzi zote hizi?!!

Mkuu Pascal Mayalla uliwafanya nini watu wa system? kwanini wanakunyanyapaa ndg yangu?
Jifunze kuwa chawa. Badilika, jishushe na uchague kujipendekeza na kusifia. Ikiwezekana waone wazee wakutambikie. Halafu waganga nao wana nafasi yao ktk safari yako ya kufukuzia teuzi. Hivyo usiwaache sana.

Inshaalah ipo siku jina litatokelezea tu...
Pascal Mayalla yupo kwenye list ya wanaofanya vetting, au unataka ajiteue? Hiyo kazi ya kuwafanyia vetting wengine inamtosha sana...make ina marupurupu na takrima kibao kuliko hizo teuzi zenyewe.
 
kuna mapungufu kadhaa kwenye hiyo taarifa. mfano hakuna halmashauri ya Tanga Mjini bali Halmashauri ya Jiji la Tanga'
hakuna cheo cha Katibu Tarafa bali Afisa Tarafa
pia cheo cha DED (district Eecutive Director) hutumika kwa wakurugenzi wa halmashuri za wilaya tu. Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji, Manispaa na Jiji haitwi DED
 
Hizi teuzi za uDED naona sasa zinawaendea ma DAS......wakuu wengine wa idara kwenye halmashauri na kwingineko naona mambo yanazidi kuwadodea...
 
Back
Top Bottom