Rais Samia afanya Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa na Taasisi: Hamduni-TAKUKURU, Makala-Dar, Kafulila-Arusha, Chalamila-Mwanza, Sendiga-Iringa, Makongoro...

Rais Samia afanya Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa na Taasisi: Hamduni-TAKUKURU, Makala-Dar, Kafulila-Arusha, Chalamila-Mwanza, Sendiga-Iringa, Makongoro...

Kwanini Tabora iwe yellow kadi? Unaichukulisje Tabora?!
Sioni tatizo la Hapi Mimi binafsi...huyu dogo atafika mbali Sana...anaweza hata akawa PM baadaye...
Tabora ni moja ya mikoa maskini sana Tanzania na maendeleo kama hakuna kwa hiyo mchango wake katika uchumi ni mdogo sana. Mimi sina tatizo na huyu kijana ila mdogo na atajifunza kama alikosa huko nyuma zile kauli za kupanda mabega "unanijuwa mimi wewe" na kunyoshea watu vidole wewe umeteuliwa tu fanya kazi unaweza kuwa mkali huku ukawa na adabu. Nakuambia hiyo yellow card chance ya kufanya makosa Tabora ndogo ila akiharibu na huko anaenda Red card one way, Tabora shule kwake itakuwa.
 
everything anafanya rais ni kupinga. kama angekuwa mtu wa kufanya ili apate sifa..angesha teua safu ya mpya muda mrefu sana.
lakin hakurupuka kachukua muda kafanya maamuzi.
Wengine hatuna tabia ya kusifia maamuzi yasiyo stahili kusifiwa.
 
Amos Makalla ni mtu mzuri aliondolea kwa misimamo yake tu history ya mtu inakufuata unakoenda alifanyiwa fitna nyingi lakini alikaa kimyaa tu.
Jamaa ni mtu poa. Kuna ishu tu nina mashaka nae ya Sugu kufungwa maana wakati ule alikuwa RC Mbeya
 
Tabora njaa.. labda atakula tumbaku.
Kwanini Tabora iwe yellow kadi? Unaichukulisje Tabora?!
Sioni tatizo la Hapi Mimi binafsi...huyu dogo atafika mbali Sana...anaweza hata akawa PM baadaye...
 
Rais SSH - baadhi ameangalia weledi - Mtaka n.k, wengine amakumbuka watoto wa Viongozi- Makongoro Nyerere, Joseph Sokoine, Utashi na uthubutu kwa kuwapa wapinzani Mikoa ya Kimkakati -Iringa - Queen Sendiga, Kafulila - Arusha, amemrudisha Jijini A. Makalla.
Pia amepeleka Haki na Umakini Takukuru - Kamishna Hamduni, Amemuondoa Br. Jen. Ibuge kutoka Foreign kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma- mwana diplomasia nguli wa mambo ya kusini mwa Afrika, Amempeleka Br. Jen. Gaguti Mtwara kusimamia usalama wa mpaka, Amemtoa Brig Jen. Mbuge toka MK-JKT kwenda Kagera, anapanga ofisi za Bunge na DPP..
 
tulieni dawa iingie, km inauma sana mseme mama ataelewa tu
 
Tunakwenda kuishuhudia dodoma ikipanda kielimu vya kutosha, mtaka yupo smart sana kwenye elimu.
Agwe na elimu wapi na wapi, waache wagogo waendelee kuomba gwala
 
Mama ilimradi tu afanye lolote aongolewe kwa miaka watu walikuwa wanalalama kubadilisha badilisha wakuu wa mikoa na wilaya kunaondoa consistencies ndio maana Magufuli aliwaacha.

Hao watu kwa muda waliokaa wanafahamu changamoto za maeneo yao, plan zilizokuwepo na changamoto za watendaji wao.

Kingine Magufuli for once alijitahidi kuweka wakuu wa mikoa kutokana na maeneo wanayoyafahamu au skills zao ili watatue changamoto kutokana priority wanazozifahamu wao.
Mfano alifanya vizuri kumleta Morogoro yule Masai maana anajua matatizo ya wakulima na wafugaji
 
Hana jipya.. umemsikia lini anaongelea mambo serious kama miradi ya maengeleo na diplomasia ya kiuchumi.

Binafsi naona anasafiri tuu na air Tanzania.
Huyu aendelee kuwatukana wastaafu. Samia nimeanza kuwa na mashaka naye. Huyu kumbe bure, tumeliwa kabisa
 
Mfano alifanya vizuri kumleta Morogoro yule Masai maana anajua matatizo ya wakulima na wafugaji
Exactly Magufuli alikuwa anaweka watu kwa sababu wanayajua hayo maeneo au kwenda kutatua changamoto sugu kutokana na skills zao.
 
Hongera Mama kwa Kuizindua Ikulu ya Jamuhuri ya Muungano Tunguu Zanzibar.
Hakuna Raisi yeyote aliyewahi kuifanyia kazi Ikuluhii kwa Uteuzi mkubwa kama Huu.
Edi Mubaarak Raisi wangu Mzalendo Mwana wa Zanzibari
Karibu Urojo na Vileja Hapa Mwembe Tanga.

Shurba pia ipo leo jioni wenye futari ya mfungo wa Sita.
Ukiniahidi kujanitakuchinjia Mbuzi wawili wa Mtibe nyama Laini.
From Chato to Tunguu.....
kweli vindu vichenjaga
 
Back
Top Bottom