Rais Samia afanya Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa na Taasisi: Hamduni-TAKUKURU, Makala-Dar, Kafulila-Arusha, Chalamila-Mwanza, Sendiga-Iringa, Makongoro...

lakini si kuna watendaji wengi ambao ni wataalam mikoani na wilayani? Naona kazi yao ni ya kisiasa zaidi.
 
Kwa mej general mbughe cheo kimeshuka amekua Brig general, wakati Brig Marco Gaguti naona amekua Mej general kuna nini hapo au tusubiri tuone
 
Ulitaka wasipige fedha ya uhamisho+nights+ontransit+wategemezi?
 
Kigogo2014 mkuu ni lipumbavu! Lilikuwaga linajidai kutoa mabrekingi nyuzi sasa hivi linaugulia maumivu limekuwa ka taahira vile linavyojisemeshasemesha!
Yule jamaa wakati jina lake liko juu siku alipojuwa kuwa ile mianya imefungwa angekaa kimyaa na kutweet mara moja moja kama breaking news tena habari za uhakika ila anataka kubaki kulekule wakati info hana akarudi badala ya kutoa habari akawa mchambaji baada ya habari. kapotea JPM alimpaisha na JPM alikuwa mropokaji hana siri na wapambe ndio wasambaza habari.
 
Wanamwanza wamepelekewa wanachokipenda. Ngoja akawape haki yao ya viboko.
 
Makalla mkuu wa Mikia wa Dar...naona wenye ccm yao wanarudi kwa kasi ya ajabu.
 
Natamani kujua kwanini mkoa wa Kagera wakuu wa mkoa huo mara nyingi wanapelekwa wanajeshi?
Mikoa ya mipakani(Ukiacha mipaka ya Kenya,Malawi,Zambia) huwa kunakua na chokochoko na machafuko ya chini kwa chini ugaidi/ujambazi

Ndio maana Kigoma na Kagera huwa ni gwanda mara kwa mara

Sasa hivi na Mtwara na Ruvuma tumeanza kuvisha bakabaka kwaajili ya Changamoto ya Cabo Delgado
 
Sijaona jina la Mkonda au nimepitia haraka haraka huu waraka.,
 
Nakuhakikishia huyu chalamila utakayemuona Mwanza hawezi kuwa yule wa Mbeya. Yule wa Mbeya alikuwa na awamu 5 ilhali huyu wa Mwanza ana awamu 6
Mwaka huu mtajinyonga.

Ukiwauliza watu Chalamila kosa lake ni nini hawana majibu ila wanataka tu atoke, chuki binafsi.
 
Mama hafanyi kazi kwa kuelekezwa na wanharakati.waendelee kupiga kelele.mbona watumishi hawawatetei!
 
Ile ilikuwa amri kutoka juu lakini Makalla hakutaka ile kitu ndio chanzo ya mengine kumpiga fitna mpaka kura za maoni ubunge alipita wakamkata huko ila nazani Mama anajuwa story hii anajuwa jamaa hana makosa.
Kama ilikuwa ni amri kutoka juu basi hii dhambi haitamuandama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…