Rais Samia afanya Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa na Taasisi: Hamduni-TAKUKURU, Makala-Dar, Kafulila-Arusha, Chalamila-Mwanza, Sendiga-Iringa, Makongoro...

Kwa nini hakuondolewa kabisa na badala yake amefanywa kuwa mkuu wa mkoa?
 
Kwanini watu hawa wanapopata vyeo wanapenda kuhenyesha wengine bila sababu yoyote? Ninamuombea hamduni asimame imara. Afanye kazi yake kwa weledi na uadilifu.
katika ufalme wake, asimsahau Kangi Lugola. Naye yupo ila sijui yupo katika hali gani 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂
 
Tushawajua toka mrema alipogombea mwaka 1995, yaani wale wabaguzi sana, walimharibia hata mrema, hawatapa uongozi wa nchi .Sasa waliyemfukuza chadema kaja kama mkuu wa mkoa kwenye ngome yao.Hongera Kafulila piga kazi
Arusha toka lini ikawa ngome ya Wachagga? Ngome ya wachagga ni Wilaya 4 za Kilimanjaro tu. Wanajaribu kutumia elimu na pesa zao vibaya. Arusha pia sio ngome ya CHADEMA hata kidogo. Lema alishinda kwa bahati tu ya mfarakano wa CCM Arusha. Nawashangaaga sana siku hizi wachagga wakitaka kuongelea kitu kinachowahusu wachagga, wanasema "MOSHI na ARUSHA". Najua ni mkakati lkn wakae wajue Arusha wapo Wairaq, Wameru, Waarusha na Wamasai. Wachagga wapo Arusha kibiashara kama walivyo Warangi, Wapare, Wanyaturu na Wanyiramba. Wapo Arusha kama walivyo DSM, Mwanza, Morogoro na Korogwe.
 
Amos Makalla amerudishwa ulingoni,
Mtaka sijamuona.


Karibu Dar mh Makalla
Mimi niliwahi kusoma humu kwamba Mama ni team msoga sikuamini. Pili nilisoma kwamba awamu ya sita inaongozwa na kiongozi wa awamu ya nne sikuamini lakini leo naanza kuamini kwani mkuu wa mkoa wa Dar mpya alishawahi kupigwa chini kwa mapungufu alionyesha Kilimanjaro, Mbeya na Songwe na hata ubunge uteuzi ulumtupa kando kwa vile ni team JK leo ni jiwe la pembeni kwani amepewa mkoa mkuu kuongoza. Nawasalimu kwa jina la jamhuri ya JPM na SSH
 
Kwahiyo unataka kusema kuwa marehemu alimfuta kazi Makalla kwa kuwa ni timu msoga au haukuwa na uwezo wa kuchapa kazi?
Kama kweli Magufuli alimuondoa kwa sababu hiyo tutarajie visasi kwa timu yake aliyoiacha
 
Hilo tu ndilo linalotakiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…