Rais Samia afanya Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa na Taasisi: Hamduni-TAKUKURU, Makala-Dar, Kafulila-Arusha, Chalamila-Mwanza, Sendiga-Iringa, Makongoro...

Rais Samia afanya Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa na Taasisi: Hamduni-TAKUKURU, Makala-Dar, Kafulila-Arusha, Chalamila-Mwanza, Sendiga-Iringa, Makongoro...

Kwa nini hakuondolewa kabisa na badala yake amefanywa kuwa mkuu wa mkoa?
Naona Mkuu wa JKT wa zamani Maj. General Charles Mbuge katolewa na kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa Kagera.

Maj. General Charles Mbuge anatakiwa ajitathmini sana utendaji wake na tabia zake za hovyo alizokuwa nazo akiwa JKT maana hiyo imekuwa ni demotion kwako.

Wakati wa utendaji wake akiwa Mkuu wa JKT Maj. Charles Mbuge alikuwa na mapungufu na natatuzo yafuatayo;

1. Kujipendekeza sana kwa mwendazake mpaka alifikia kuwadharau mabosi wake

2. Hata kupandishwa cheo kuwa Maj. General kulikuwa na walakini

3. Empties[emoji38][emoji38][emoji38] za vijana waliokuwa wanakwenda JKT na hivyo kupelekea kuwa na malipo yaliyokuwa na walakini sana. Mh. Rais apeleke team ya wakaguzi kwenye makambi yote ili kukinganisha idadi halisi ya vijana waliokuwa wanapelekwa JKT na idadi ya pesa iliyokuwa inaombwa hazina
4. Alikuwa anaoenda kuwanyanyasa wale wote waliokuwa na mawazo tofauti kuhusu kumanage rasilimali fedha na hivyo kupelekea kuwahamisha vituo kama ishara ya kuwakomoa
6. Kuna badhi ya askari alikataa kuwapanxisha vyeo mwezi wa 2 wakati walikuwa wanastahili kutokana na chuki binafsi tu.

7. Kuna askari mmoja yuko Kigoma alitakiwa apandishwe cheo mwezi wa 2 kuwa Major lakini Maj. General Mbuge alilinyofoa jina lake wakati wa kuyapeleka majina Ngome ili kumkomoa askari husika kwa chuki binafsi tu

8. Maj. General Charles Mbuge kutokana na kutojiamini na ukizingatia kuwa na shule ndogo aliwagawa wafanyakazi wa JKT

Mwisho, atakaekuja kuchukua nafasi ya Maj. General Mbuge ajaribu kuangalia weakness alizokuwa nazo Mbuge ili kujenga team work na nidhamu kwenye jeshi letu, acha mambo ya kuonea watu.

Asante!!
 
Chalamila yuko pale pale kama mkuu wa mkoa. Kelele za kina Maria Sarungi hazijasikilizwa.

Hamduni afanye kazi kitaalam, aachane na vitisho vya magwanda ya kijeshi kama ya aliemtangulia. Akumbuke PCCB ni law enforcement agency or investigative services hivyo afanye kazi kitaalam.
Kwanini watu hawa wanapopata vyeo wanapenda kuhenyesha wengine bila sababu yoyote? Ninamuombea hamduni asimame imara. Afanye kazi yake kwa weledi na uadilifu.
katika ufalme wake, asimsahau Kangi Lugola. Naye yupo ila sijui yupo katika hali gani 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂
 
Tushawajua toka mrema alipogombea mwaka 1995, yaani wale wabaguzi sana, walimharibia hata mrema, hawatapa uongozi wa nchi .Sasa waliyemfukuza chadema kaja kama mkuu wa mkoa kwenye ngome yao.Hongera Kafulila piga kazi
Arusha toka lini ikawa ngome ya Wachagga? Ngome ya wachagga ni Wilaya 4 za Kilimanjaro tu. Wanajaribu kutumia elimu na pesa zao vibaya. Arusha pia sio ngome ya CHADEMA hata kidogo. Lema alishinda kwa bahati tu ya mfarakano wa CCM Arusha. Nawashangaaga sana siku hizi wachagga wakitaka kuongelea kitu kinachowahusu wachagga, wanasema "MOSHI na ARUSHA". Najua ni mkakati lkn wakae wajue Arusha wapo Wairaq, Wameru, Waarusha na Wamasai. Wachagga wapo Arusha kibiashara kama walivyo Warangi, Wapare, Wanyaturu na Wanyiramba. Wapo Arusha kama walivyo DSM, Mwanza, Morogoro na Korogwe.
 
Amos Makalla amerudishwa ulingoni,
Mtaka sijamuona.

Karibu Dar mh Makalla
Mimi niliwahi kusoma humu kwamba Mama ni team msoga sikuamini. Pili nilisoma kwamba awamu ya sita inaongozwa na kiongozi wa awamu ya nne sikuamini lakini leo naanza kuamini kwani mkuu wa mkoa wa Dar mpya alishawahi kupigwa chini kwa mapungufu alionyesha Kilimanjaro, Mbeya na Songwe na hata ubunge uteuzi ulumtupa kando kwa vile ni team JK leo ni jiwe la pembeni kwani amepewa mkoa mkuu kuongoza. Nawasalimu kwa jina la jamhuri ya JPM na SSH
 
Kwahiyo unataka kusema kuwa marehemu alimfuta kazi Makalla kwa kuwa ni timu msoga au haukuwa na uwezo wa kuchapa kazi?
Kama kweli Magufuli alimuondoa kwa sababu hiyo tutarajie visasi kwa timu yake aliyoiacha
 
Kwanini watu hawa wanapopata vyeo wanapenda kuhenyesha wengine bila sababu yoyote? Ninamuombea hamduni asimame imara. Afanye kazi yake kwa weledi na uadilifu.
katika ufalme wake, asimsahau Kangi Lugola. Naye yupo ila sijui yupo katika hali gani [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Hilo tu ndilo linalotakiwa
 
Back
Top Bottom