Rais Samia afanya ziara ya Kiserikali nchini Msumbiji, ahimiza kutumia fursa za kibiashara zilizopo katika nchi hizo mbili

Rais Samia afanya ziara ya Kiserikali nchini Msumbiji, ahimiza kutumia fursa za kibiashara zilizopo katika nchi hizo mbili

Tozo zimepunguzwa na zingine kuondolewa lengo la kuondoa tozo ni kumuinua mtanzania na sio kumdidimiza na Rais Samia Suluhu kupitia hizi ziara zake anakuza diplomasia ya uchumi
Hebu nenda uko bana na diplomasia zako msitufanye wajinga hapa.!!

Kwani hizo tozo aliweka nani??
Alafu Leo uje uzitoe sijui kupunguza tuanze kukusifu??
Wakati anaweka tozo hakujua hali za watu wake??

Hizo siasa zenu msizilete kwenye mambo ya msingi ya maisha ya watu.

Unga kilo 2200 huku alafu mnaleta hadithi za diplomasia.!!!?
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika ziara ya Kiserikali nchini Msumbiji leo tarehe 21 Septemba, 2022.



Rais Samia ametaka ushirikiano wa ulinzi baina ya nchi hizi mbili hasa ule wa mipaka ulio anzishwa tangu miaka ya 1980 uendelezwe hasa kwenye kipindi hiki muhimu cha kupambana na ugaidi.

Amegusia pia jitihada za kuongeza ushirikiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Msumbiji, pia namna bora ya kutumia fursa za kibiashara zilizopo baina ya nchi hizi mbili.

Upande wa elimu wameafikiana kubadilishana wanafunzi, aidha lugha ya kiswahili kwa sasa itapewa kipaumbele nchini Msumbiji.

Kupitia safari hii, Rais Samia anaamini ukurasa mpya wa ushirikiano mwema kati ya Msumbiji na Tanzania utafunguka.

Kwani ushirikiano ulikuwa haupo?

Wales to Maputo flying across the spheres........more trips are still loading at the citizens' expense
 
Safari hii imeshindikana kupata mabilioni ya kutembeza bakuli kwa malkia, imebidi mje na gia hiyo mkiwa busy kuchoma tozo kuzurula sio!
 
Back
Top Bottom