Rais Samia afanyiwa Ibada Maalumu nzito Vatican

Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania amefanyiwa ibada Maalumu nzito sana VATICAN. Ibada ambayo imefanywa na kuongozwa na jumuiya ya watanzania wakatoliki walioko huko VATICAN. Ambapo ni ibada maalumu ya kufunga mwaka wa masomo VATICAN.

Jumuiya hiyo ya kikatoliki inaundwa na Watumishi wa Mungu wapatao 302, Wakiwemo Mapadre,Mashemasi,Watawa na Mafrateri. Ambao wanapata Elimu katika vyuo vikuu vya VATICAN.

Ibada hiyo maalumu iliambatana na hafla ya kuwaaga na kuwakaribisha wanafunzi wengine kutoka Tanzania. Ibada hiyo pia ilihudhuriwa na Mheshimiwa Hassan Iddi Mwamweta ambaye ni mlezi wa jumuiya hiyo na mwenye makazi yake Nchini Ujerumani.

Pia alikuwepo Balozi Mahmoud Kombo Balozi wa Tanzania Nchini Italia. Itakumbukwa pia ya kuwa mnamo Tarehe 12-2-2024 Rais wetu mpendwa Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan alipofanya ziara ya kikazi kwa mualiko maalum wa papa Fransis VATICAN aliweza kuonana na jumuiya hii na Diaspora wengine na kufanya nao mazungumzo.

Kilichopatikana kwa Maombi hulindwa kwa Maombi. Kilichoinuliwa na Mungu ni lazima kiombewe nguvu ya ulinzi kutoka kwa Mungu Mwenyewe. Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Mama Samia Ni Mpango wa Mungu Mwenyewe aliyemuinua kwa mkono wake .ndio maana watu wanaendelea kumuombea dua njema ndani na nje ya nchi.kwa kuwa wanaona kazi kubwa inayofanywa na Rais wetu mpendwa kwa uzalendo na hofu ya Mungu ndani yake. Ndio maana amekuwa kipenzi cha viongozi mbalimbali wa Dini na madhehebu yote hapa Nchini.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Kichekesho, Muislamu na Mkatoliki wapi na wapi?
 
Kinachoitwa uchaguzi uliofanyika 2020 ni uhayawani wa kiwango kikubwa mno ndiyo maana yule mhusika mkuu hakuchukua round akasukumiziwa kuzimu.
Jambo ambalo ningependa kusema ni kuwa suala la mtu kufa na kuishi lipo na linabakia mikononi mwa Mungu mwenyewe ,ambaye anafahamu njia ya kuondokea kila mmoja wetu hapa Duniani..
 
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania amefanyiwa ibada Maalumu nzito sana VATICAN. Ibada ambayo imefanywa na kuongozwa na jumuiya ya watanzania wakatoliki walioko huko VATICAN. Ambapo ni ibada maalumu ya kufunga mwaka wa masomo VATICAN.

Jumuiya hiyo ya kikatoliki inaundwa na Watumishi wa Mungu wapatao 302, Wakiwemo Mapadre,Mashemasi,Watawa na Mafrateri. Ambao wanapata Elimu katika vyuo vikuu vya VATICAN.

Ibada hiyo maalumu iliambatana na hafla ya kuwaaga na kuwakaribisha wanafunzi wengine kutoka Tanzania. Ibada hiyo pia ilihudhuriwa na Mheshimiwa Hassan Iddi Mwamweta ambaye ni mlezi wa jumuiya hiyo na mwenye makazi yake Nchini Ujerumani.

Pia alikuwepo Balozi Mahmoud Kombo Balozi wa Tanzania Nchini Italia. Itakumbukwa pia ya kuwa mnamo Tarehe 12-2-2024 Rais wetu mpendwa Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan alipofanya ziara ya kikazi kwa mualiko maalum wa papa Fransis VATICAN aliweza kuonana na jumuiya hii na Diaspora wengine na kufanya nao mazungumzo.

Kilichopatikana kwa Maombi hulindwa kwa Maombi. Kilichoinuliwa na Mungu ni lazima kiombewe nguvu ya ulinzi kutoka kwa Mungu Mwenyewe. Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Mama Samia Ni Mpango wa Mungu Mwenyewe aliyemuinua kwa mkono wake .ndio maana watu wanaendelea kumuombea dua njema ndani na nje ya nchi.kwa kuwa wanaona kazi kubwa inayofanywa na Rais wetu mpendwa kwa uzalendo na hofu ya Mungu ndani yake. Ndio maana amekuwa kipenzi cha viongozi mbalimbali wa Dini na madhehebu yote hapa Nchini.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Samia ni Mkombozi wa taifa
 
Ndugu mwandishi. Nakujibu nikiwa mmojawapo wa washiriki wa Ibada hiyo. Unakosea haki wahusika unapotoa taarifa ya uwongo. Ibada iliyofanyika, ilikuwa na lengo moja tu, kuwaaga wahitimu. Kisha ndani yake, liliombewa Taifa, Rais na viongozi wake. Hakukuwa na Ibada nzito iliyoandaliwa kwa ajili ya kumwombea Rais. Mabalozi walishiriki kama viongozi walezi wa Jumuiya za Diaspora. Na kisha, hakuna hata mmoja wawanafunzi anayeishi Vatican, bali huishi Italy. Hakiki taarifa na kuripoti kilicho sahihi. Aliyekufikishia taarifa angeweza kukuunganisha na viongozi husika, kupata habari kamili. Habari hii itarushwa Radio Vatican Swahili, na Radio Maria Tanzania, na itakuwa na Vichwa vya habari tofauti na vyenu.
 
Kabisa,tuendelee kutangaza kazi za chama bila kuchoka,hongera kwako kaka.
Hilo ndio jambo kubwa sana kqetu sisi kuendelea bila kuchoka kutangaza kazi zinazofanywa na serikali ya Rais Samia. Ili kuondosha upotoshaji ambao umekuwa ukifanywa na wapinzani wachache kama wale wa CHADEMA waliofirisika kisera.
 
Ndugu mwandishi. Nakujibu nikiwa mmojawapo wa washiriki wa Ibada hiyo. Unakosea haki wahusika unapotoa taarifa ya uwongo. Ibada iliyofanyika, ilikuwa na lengo moja tu, kuwaaga wahitimu. Kisha ndani yake, liliombewa Taifa, Rais na viongozi wake. Hakukuwa na Ibada nzito iliyoandaliwa kwa ajili ya kumwombea Rais. Mabalozi walishiriki kama viongozi walezi wa Jumuiya za Diaspora. Na kisha, hakuna hata mmoja wawanafunzi anayeishi Vatican, bali huishi Italy. Hakiki taarifa na kuripoti kilicho sahihi. Aliyekufikishia taarifa angeweza kukuunganisha na viongozi husika, kupata habari kamili. Habari hii itarushwa Radio Vatican Swahili, na Radio Maria Tanzania, na itakuwa na Vichwa vya habari tofauti na vyenu.
Acha kujichanganya ndugu yangu sasa hapo kipi nilichopotosha? Maana ningekuwa nimepotosha kama kusingekuwa na ibada hiyo wala maombezi kwa Mheshimiwa Rais.lakini wewe mwenyewe umekili kuwa ilikuwepo na Mheshimiwa Rais aliombewa. Sasa unakataa kipi na kuunga kipi.?Mbona habari na taarifa yangu ipo wazi na imenyooka kabisa? Au ilimradi tu upinge?
 
Hilo ndio jambo kubwa sana kqetu sisi kuendelea bila kuchoka kutangaza kazi zinazofanywa na serikali ya Rais Samia. Ili kuondosha upotoshaji ambao umekuwa ukifanywa na wapinzani wachache kama wale wa CHADEMA waliofirisika kisera.
Kabisa mkuu,na ukweli ni kuwa tumewazidi kwa hoja,usiku na mchana tuendelee kuutetea serikali yetu na chama chetu.
 
Yupo Vatican?
Soma tena habari ndugu yangu maana imenyooka .ok kwa kukusaidia tu ni kuwa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan hayupo VATICAN ,bali kule VATICAN yamefanyika au kumefanyika ibada maalum ya kumuombea.ambayo imefanywa na jumuiya ya wanafunzi wanaosoma katika vyuo vya VATICAN . ambapo ni katika tukio hilo kulifanyika hafla ya kuwaaga wanaomaliza masomo yao na kuwakaribisha wengine kutoka Tanzania.
 
Hakuna dhambi kubwa kama kuiba kura kwa hilo na waombezi wote moto unawangoja jumla. Hatuwahukumu lakini ndiyo ukweli. Duniani tunapita na madaraka tutayaacha
 
Hakuna dhambi kubwa kama kuiba kura kwa hilo na waombezi moto unawangoja jumla.
CCM ipo madarakani na itaendelea kusalia madarakani kwa muda mrefu sana kwa kadri ya uhai wa Taifa letu,kutokana na sera na ajenda zake zinazogusa maisha ya watu pamoja na kwenda na mahitaji ya watu na wakati. Ni upendo wa watu kwa CCM Ndio huiweka CCM Madarakani kwa kura zao za kishindoo za ndio.
 
Mama anatosha.
Atafanyiwa sana hizo,(mqpepo) hazina maana yoyote, umeishawahi kuona Biden, au Trump, anaenda kuombewa kanisani? Ila hutaona akialikwa white house kama Ruto, au siasa, za, CCM na uchaguzi, zikijadiliwa kwenye vyombo vya habari vya kimataifa, Leo Al Jazeera katika inside story walikua wanajadili Uchaguzi unaokuja South Africa.
Sasa uchafu wa CCM hauwezi, kijadiliwa popote labda Lumumba,
Nikiwaza, Hapa kinana, au Makonda, au, Makala,waalikwe Al Jazeera wahojiwe kuhusu mafanikio ya CCM na nchi tangu Uhuru, upande wa pili Awepo Lisu, Mnyika, au Wenje! Tunajua ma CCM yatakimbia mkia yameweka katikati ya makalio!
 
Jambo ambalo ningependa kusema ni kuwa suala la mtu kufa na kuishi lipo na linabakia mikononi mwa Mungu mwenyewe ,ambaye anafahamu njia ya kuondokea kila mmoja wetu hapa Duniani..
Sizungumzii kufa kwani wote tutakufa nazungumzia hukumu. Ukitenda uovu ujue kuna hukumu,na uovu wako ukizidi hata siku zako za kuishi duniani zinakatishwa ili usiendelee kuumiza wengine.
 
Back
Top Bottom