Rais Samia afichua siri ya kuwatumbua viongozi Serikalini

Rais Samia afichua siri ya kuwatumbua viongozi Serikalini

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Akizungumza jijini Arusha wakati akifungua Mkutano wa Faragha (Retreat) wa Mawaziri na Makatibu Wakuu uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa (AICC) jijini Arusha Rais wa Jamhuri ameeleza sababu za kufanya mabadiliko ya mara kwa mara ya viongozi licha ya yeye kutokupenda kufanya hivyo.

Rais Samia Suluhu amesema kuwa hapendi na anafahamu madhara ya kufanya mabadiliko ya mara kwa mara kwani kufanya hivyo kunawafanya viongozi wafanye kazi kwa hofu na kushindwa kuwa na mipango ya muda mrefu kwa kuhofia teuzi zao kutenguliwa

HATA HIVYO RAIS SAMIA AMESEMA INGAWA SIO LENGO LAKE KUBADILI VIONGOZI MARA KWA MARA KWANI INACHUKUA MUDA MREFU KUWAJENGA LAKINI analazimika kufanya hivyo ili kuepusha madhara zaidi serikalini na kwa wananchi.

Tazama video hapa chini:


 
Kikubwa anakiri kwamba wateulowa wake ambao ni makada kindakindaki wa CCM wanafanyakazi kwa mazoea.

Kataa CCM 2025
 
Tatizo anawahamisha maeneo yao ya utendaji. Ingependeza sana kama angewaacha wakawa watazamaji maana watanzania wenye vigezo wapo tele
 
Yeye ndiye amiri jeshi mkuu nadhani anayajua mengi kuliko tunayoyaona na kuyasikia, Ni sawa kwa mustabali wa taifa
 
Haohao ndio wafujaji na wezi wa mali ya umma.
CAG anatoa ripoti kilasiku haohao ndio wakwapuaji.
Zaidi sana hapo wanagombana maana wanazidiana kwenye kukwapua.
 
Back
Top Bottom