Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais Samia ametoa agizo hilo Agosti 06, 2024 wakati akihitimisha ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro.
"Nimejionea mwenyewe wakati naenda Kilosa tofauti iliyokuwa ikionekana maeneo ambayo hayana umeme na yale yenye umeme ambayo yameshamiri kwa shughuli za biashara, hii inaonesha umuhimu wa nishati katika maeneo yote nchini," amesisitiza Dkt.Samia.
Aidha, amesisitiza kuwa uwepo wa umeme wa uhakika kutoka Bwawa la Julius Nyerere kunaufanya Mkoa wa Morogoro kuwa sehemu sahihi ya uwekezaji.
"Morogoro sasa ina umeme wa uhakika, hali inayovuta uwekezaji ndani ya Mkoa." Ameongeza Mhe.Rais
Akizungumzia kuhusu miradi ya umeme vijijini Mkoa wa Morogoro, Dkt. Samia amesema kupitia Wakala wa Nishati Vijijini Serikali imepeleka umeme kwenye Vijiji 621 kati ya Vijiji 669.