Rais Samia aidhinisha Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote, sasa ni Sheria rasmi

Hao wachache mmeshindwa kuwahudumia je hao wengi itakuwaje? Report za CAG mmeweka kwapani wakati zilianinisha uozo wote kwenye malipo ya NHIF.Situmii hiyo Bima yenu na silipii bora nibaki Jubelee Au Assemble Au Strategy nijue nimefunga mkataba na bima ya Mwaka mzima kuliko sarakasi za dawa hakuna kupata rufaa mpaka Dr umlilie
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametia saini muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote na sasa imekua sheria kamili.

Novemba 2, 2023 Bunge lilipitisha muswada huo kwa asilimia 100 na kuweka historia, baada ya mkwamo uliokuwepo kwa takribani miaka mitano tangu ulipofufuliwa upya mwaka 2018.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya jana Desemba 4, 2023 imesema muswada huo sasa umeshasainiwa na Rais na kuwa sheria kamili, baada ya kutangazwa kwenye gazeti la Serikali Desemba Mosi, 2023.

Saini ya Rais katika sheria hiyo, inaipa kazi Wizara ya Afya kuanza utungaji wa kanuni kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa sheria hiyo, ambayo itawezesha kila Mtanzania kupata huduma za afya pasipo na kikwazo cha kiuchumi.

Katika kufanikisha hayo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi iliweka msisitizo wa umuhimu wa kuwa na mfuko kwa ajili ya kugharamia bima ya afya kwa watu wasio na uwezo, na Serikali iusimamie kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora za afya.

Kupitia sheria hiyo kutakuwa na utaratibu wa utambuzi na usajili wa kundi la watu wasio na uwezo, kwa lengo la kuhakikisha wanapata huduma za afya bila kikwazo cha fedha.

Kundi hilo litajumuishwa kwenye skimu ya Bima ya Afya ya Umma kwa namna itakavyoainishwa kwenye kanuni zitakazotungwa hapo baadaye, huku akibainisha vyanzo vya mapato vitakavyotumika kugharamia skimu hiyo.

Akiusoma muswada huo bungeni kwa mara ya mwisho, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema vyanzo vya mapato ya skimu hiyo ni pamoja na sehemu ya mapato yatokanayo na ushuru wa bidhaa.

"Kwenye vinywaji vyenye kaboni, vinywaji vikali, bidhaa za vipodozi, kodi ya michezo ya kubahatisha, ada ya bima za vyombo vya moto na mapato yatokanayo na ushuru wa miamala ya kielektroniki " alisema Waziri Ummy.

Aliuhakikishia umma juu ya huduma za matibabu kwa kundi la wananchi wasio na uwezo.

MWANANCHI
 
Bima ya afya kwa wote nzuri sana. Swali je wadau wote walishirikishwa? Au ndo yale ya "tunapitisha halafu tutasikiliza maoni baadae. Hapa kuna watu walitaka tu kuficha matumizi mabaya ya fedha na malipo hewa kwa mahospitali kwenye ule utaratibu wa mwanzo. Tuelezwe fedha zilivyotumika mpaka ikapelekea mfuko kufilisika siyo ku compromise afya za watoto kwa kuleta vifurushi vinavyotuwekea vipingamizi vya vipimo na dawa
 
Najinasibu kwa kuwa consistent on issues!

Kwa muda mrefu nimeulizia na kushawishi juu ya uwepo wa sheria ya bima ya afya kwa wote ...ikiwa ni mbinu ya kistratejia kufikia uhuru wa kweli na kujitegemea katika maswala yahusuyo afya.

Mchakato huu ni mrefu sana na uligubikwa na vikwazo vingi sana.kutoka ndani na nje ya nchi.

Hatimaye umekamilika hapa sasa ndipo naweka matumaini ya kuwa na afya endelevu kwa wote.

View attachment 2833872

---
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametia saini muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote na sasa imekua sheria kamili.

Novemba 2, 2023 Bunge lilipitisha muswada huo kwa asilimia 100 na kuweka historia, baada ya mkwamo uliokuwepo kwa takribani miaka mitano tangu ulipofufuliwa upya mwaka 2018.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya jana Desemba 4, 2023 imesema muswada huo sasa umeshasainiwa na Rais na kuwa sheria kamili, baada ya kutangazwa kwenye gazeti la Serikali Desemba Mosi, 2023.

Saini ya Rais katika sheria hiyo, inaipa kazi Wizara ya Afya kuanza utungaji wa kanuni kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa sheria hiyo, ambayo itawezesha kila Mtanzania kupata huduma za afya pasipo na kikwazo cha kiuchumi.

Katika kufanikisha hayo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi iliweka msisitizo wa umuhimu wa kuwa na mfuko kwa ajili ya kugharamia bima ya afya kwa watu wasio na uwezo, na Serikali iusimamie kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora za afya.

Kupitia sheria hiyo kutakuwa na utaratibu wa utambuzi na usajili wa kundi la watu wasio na uwezo, kwa lengo la kuhakikisha wanapata huduma za afya bila kikwazo cha fedha.

Kundi hilo litajumuishwa kwenye skimu ya Bima ya Afya ya Umma kwa namna itakavyoainishwa kwenye kanuni zitakazotungwa hapo baadaye, huku akibainisha vyanzo vya mapato vitakavyotumika kugharamia skimu hiyo.

Akiusoma muswada huo bungeni kwa mara ya mwisho, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema vyanzo vya mapato ya skimu hiyo ni pamoja na sehemu ya mapato yatokanayo na ushuru wa bidhaa.

"Kwenye vinywaji vyenye kaboni, vinywaji vikali, bidhaa za vipodozi, kodi ya michezo ya kubahatisha, ada ya bima za vyombo vya moto na mapato yatokanayo na ushuru wa miamala ya kielektroniki " alisema Waziri Ummy.

Aliuhakikishia umma juu ya huduma za matibabu kwa kundi la wananchi wasio na uwezo.

MWANANCHI
Upigaji uendelee, chaka jipya limeibuka.
 
Wazee,wajawazito na watoto below five waliahidiwa watapata hudumu za afya bure,mpaka leo hawajapata,sembuse wote wasio na uwezo!Tusubiri,ila naamini huu ni usanii mwinginene tunapoelekea uchaguzi mkuu.Wadanganyeni wadanganyika,wengine hatudanganyiki.
 
Najinasibu kwa kuwa consistent on issues!

Kwa muda mrefu nimeulizia na kushawishi juu ya uwepo wa sheria ya bima ya afya kwa wote ...ikiwa ni mbinu ya kistratejia kufikia uhuru wa kweli na kujitegemea katika maswala yahusuyo afya.

Mchakato huu ni mrefu sana na uligubikwa na vikwazo vingi sana.kutoka ndani na nje ya nchi.

Hatimaye umekamilika hapa sasa ndipo naweka matumaini ya kuwa na afya endelevu kwa wote.

View attachment 2833872

---
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametia saini muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote na sasa imekua sheria kamili.

Novemba 2, 2023 Bunge lilipitisha muswada huo kwa asilimia 100 na kuweka historia, baada ya mkwamo uliokuwepo kwa takribani miaka mitano tangu ulipofufuliwa upya mwaka 2018.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya jana Desemba 4, 2023 imesema muswada huo sasa umeshasainiwa na Rais na kuwa sheria kamili, baada ya kutangazwa kwenye gazeti la Serikali Desemba Mosi, 2023.

Saini ya Rais katika sheria hiyo, inaipa kazi Wizara ya Afya kuanza utungaji wa kanuni kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa sheria hiyo, ambayo itawezesha kila Mtanzania kupata huduma za afya pasipo na kikwazo cha kiuchumi.

Katika kufanikisha hayo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi iliweka msisitizo wa umuhimu wa kuwa na mfuko kwa ajili ya kugharamia bima ya afya kwa watu wasio na uwezo, na Serikali iusimamie kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora za afya.

Kupitia sheria hiyo kutakuwa na utaratibu wa utambuzi na usajili wa kundi la watu wasio na uwezo, kwa lengo la kuhakikisha wanapata huduma za afya bila kikwazo cha fedha.

Kundi hilo litajumuishwa kwenye skimu ya Bima ya Afya ya Umma kwa namna itakavyoainishwa kwenye kanuni zitakazotungwa hapo baadaye, huku akibainisha vyanzo vya mapato vitakavyotumika kugharamia skimu hiyo.

Akiusoma muswada huo bungeni kwa mara ya mwisho, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema vyanzo vya mapato ya skimu hiyo ni pamoja na sehemu ya mapato yatokanayo na ushuru wa bidhaa.

"Kwenye vinywaji vyenye kaboni, vinywaji vikali, bidhaa za vipodozi, kodi ya michezo ya kubahatisha, ada ya bima za vyombo vya moto na mapato yatokanayo na ushuru wa miamala ya kielektroniki " alisema Waziri Ummy.

Aliuhakikishia umma juu ya huduma za matibabu kwa kundi la wananchi wasio na uwezo.

MWANANCHI
Kwahiyo wanafikiri watanzania ni wazungu kisa USA walipitisha bima ya afya kwa wote!
Ni heri mngeleta Kodi ieleweke kuliko haya manyanyaso ya dawa hizi hazipo kwenye bima!
Bima inayotibu malaria na kichwa... Hapo hamna kitu
 
Kwa Sheria hii ndio huduma ya afya inaenda kuwa ya kiwango duni kupita maelezo. Hakuna jambo lolote linaendeshwa na serekali kwa ufanisi. Utakuta kinasemwa kingine, kinatekelezwa kingine kabisa.
 
Uwepo wa sheria ni jambo moja na utekelezaji ni jingine. Hasa utekelezaji kwa weledi na ufanisi
Sheria zipo nyingi sana ambazo kama zingetekelezwa kwa weledi ili lengo litimie, tungekuwa mbali kimaendeleo.
Bima kwa wote bila madaktari, wahudimu na madawa ya kutosha lengo halitatimia. Hivyo maboresho yaende sambamba na hilo.
Hata hivyo, adui mwingine ni matumizi mabaya ya fedha itakayotengwa (ufisadi).
 
Najinasibu kwa kuwa consistent on issues!

Kwa muda mrefu nimeulizia na kushawishi juu ya uwepo wa sheria ya bima ya afya kwa wote ...ikiwa ni mbinu ya kistratejia kufikia uhuru wa kweli na kujitegemea katika maswala yahusuyo afya.

Mchakato huu ni mrefu sana na uligubikwa na vikwazo vingi sana.kutoka ndani na nje ya nchi.

Hatimaye umekamilika hapa sasa ndipo naweka matumaini ya kuwa na afya endelevu kwa wote.

View attachment 2833872

---
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametia saini muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote na sasa imekua sheria kamili.

Novemba 2, 2023 Bunge lilipitisha muswada huo kwa asilimia 100 na kuweka historia, baada ya mkwamo uliokuwepo kwa takribani miaka mitano tangu ulipofufuliwa upya mwaka 2018.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya jana Desemba 4, 2023 imesema muswada huo sasa umeshasainiwa na Rais na kuwa sheria kamili, baada ya kutangazwa kwenye gazeti la Serikali Desemba Mosi, 2023.

Saini ya Rais katika sheria hiyo, inaipa kazi Wizara ya Afya kuanza utungaji wa kanuni kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa sheria hiyo, ambayo itawezesha kila Mtanzania kupata huduma za afya pasipo na kikwazo cha kiuchumi.

Katika kufanikisha hayo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi iliweka msisitizo wa umuhimu wa kuwa na mfuko kwa ajili ya kugharamia bima ya afya kwa watu wasio na uwezo, na Serikali iusimamie kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora za afya.

Kupitia sheria hiyo kutakuwa na utaratibu wa utambuzi na usajili wa kundi la watu wasio na uwezo, kwa lengo la kuhakikisha wanapata huduma za afya bila kikwazo cha fedha.

Kundi hilo litajumuishwa kwenye skimu ya Bima ya Afya ya Umma kwa namna itakavyoainishwa kwenye kanuni zitakazotungwa hapo baadaye, huku akibainisha vyanzo vya mapato vitakavyotumika kugharamia skimu hiyo.

Akiusoma muswada huo bungeni kwa mara ya mwisho, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema vyanzo vya mapato ya skimu hiyo ni pamoja na sehemu ya mapato yatokanayo na ushuru wa bidhaa.

"Kwenye vinywaji vyenye kaboni, vinywaji vikali, bidhaa za vipodozi, kodi ya michezo ya kubahatisha, ada ya bima za vyombo vya moto na mapato yatokanayo na ushuru wa miamala ya kielektroniki " alisema Waziri Ummy.

Aliuhakikishia umma juu ya huduma za matibabu kwa kundi la wananchi wasio na uwezo.

MWANANCHI
Vigezo gani vitatumika kusema hawa hawana uwezo na hawa wana uwezo?

Kwenye Taifa la watu milioni 60 wenye uwezo si inafahamika ni wachache sana? Na wengi ni masikini wengine wenye umasikini wa kutupwa?

Tufahamu kwanza vigezo gani vinatumika. Maana gharama za matibabu zinafahamika.

Kama kweli itakuwa “universal healthcare”, tufahamu how it’s going to work.
 
Huyu ndio rahisi pekee ambae amefanya mambo mengi yaliyopingwa na wananchi wake ktk historia ya nchi yetu.
Katiba yetu ni mbovu ndio maana imetuletea mtu mbovu.
Ni mtu asiejali raia wake wanasema nini na wanataka nini na wana uwezo gani.
68% ya Watanzania wanaishi vijijini, maisha yao ni duni mlo wa siku ni jasho la damu watamudu vipi gharama za bima?
Wabunge tunaodanganywa kuwa tunawachagua kama wawakilishi wa wananchi ni upuuzi mtupu, hawajawafikiria wananchi wa hali ya chini kwasababu siikitu kwao ilimradi wao na familia zao wapo salama.
 
Back
Top Bottom