Rais Samia aidhinisha Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote, sasa ni Sheria rasmi

Rais Samia aidhinisha Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote, sasa ni Sheria rasmi

K
Najinasibu kwa kuwa consistent on issues!

Kwa muda mrefu nimeulizia na kushawishi juu ya uwepo wa sheria ya bima ya afya kwa wote ...ikiwa ni mbinu ya kistratejia kufikia uhuru wa kweli na kujitegemea katika maswala yahusuyo afya.

Mchakato huu ni mrefu sana na uligubikwa na vikwazo vingi sana.kutoka ndani na nje ya nchi.

Hatimaye umekamilika hapa sasa ndipo naweka matumaini ya kuwa na afya endelevu kwa wote.

View attachment 2833872

---
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametia saini muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote na sasa imekua sheria kamili.

Novemba 2, 2023 Bunge lilipitisha muswada huo kwa asilimia 100 na kuweka historia, baada ya mkwamo uliokuwepo kwa takribani miaka mitano tangu ulipofufuliwa upya mwaka 2018.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya jana Desemba 4, 2023 imesema muswada huo sasa umeshasainiwa na Rais na kuwa sheria kamili, baada ya kutangazwa kwenye gazeti la Serikali Desemba Mosi, 2023.

Saini ya Rais katika sheria hiyo, inaipa kazi Wizara ya Afya kuanza utungaji wa kanuni kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa sheria hiyo, ambayo itawezesha kila Mtanzania kupata huduma za afya pasipo na kikwazo cha kiuchumi.

Katika kufanikisha hayo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi iliweka msisitizo wa umuhimu wa kuwa na mfuko kwa ajili ya kugharamia bima ya afya kwa watu wasio na uwezo, na Serikali iusimamie kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora za afya.

Kupitia sheria hiyo kutakuwa na utaratibu wa utambuzi na usajili wa kundi la watu wasio na uwezo, kwa lengo la kuhakikisha wanapata huduma za afya bila kikwazo cha fedha.

Kundi hilo litajumuishwa kwenye skimu ya Bima ya Afya ya Umma kwa namna itakavyoainishwa kwenye kanuni zitakazotungwa hapo baadaye, huku akibainisha vyanzo vya mapato vitakavyotumika kugharamia skimu hiyo.

Akiusoma muswada huo bungeni kwa mara ya mwisho, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema vyanzo vya mapato ya skimu hiyo ni pamoja na sehemu ya mapato yatokanayo na ushuru wa bidhaa.

"Kwenye vinywaji vyenye kaboni, vinywaji vikali, bidhaa za vipodozi, kodi ya michezo ya kubahatisha, ada ya bima za vyombo vya moto na mapato yatokanayo na ushuru wa miamala ya kielektroniki " alisema Waziri Ummy.

Aliuhakikishia umma juu ya huduma za matibabu kwa kundi la wananchi wasio na uwezo.

MWANANCHI

Hao wachache mmeshindwa kuwahudumia je hao wengi itakuwaje? Report za CAG mmeweka kwapani wakati zilianinisha uozo wote kwenye malipo ya NHIF.Situmii hiyo Bima yenu na silipii bora nibaki Jubelee Au Assemble Au Strategy nijue nimefunga mkataba na bima ya Mwaka mzima kuliko sarakasi za dawa hakuna kupata rufaa mpaka Dr umlilie
Kwa andiko hili unaamini kuwa utapewa bure siyo
 
Kwa Sheria hii ndio huduma ya afya inaenda kuwa ya kiwango duni kupita maelezo. Hakuna jambo lolote linaendeshwa na serekali kwa ufanisi. Utakuta kinasemwa kingine, kinatekelezwa kingine kabisa.
Wew ndo unayoilewa hiyo bima yule waziri anamdoma kama chiriku mbona atakomaa kipindi hiki
 
Huyu ndio rahisi pekee ambae amefanya mambo mengi yaliyopingwa na wananchi wake ktk historia ya nchi yetu.
Katiba yetu ni mbovu ndio maana imetuletea mtu mbovu.
Ni mtu asiejali raia wake wanasema nini na wanataka nini na wana uwezo gani.
68% ya Watanzania wanaishi vijijini, maisha yao ni duni mlo wa siku ni jasho la damu watamudu vipi gharama za bima?
Wabunge tunaodanganywa kuwa tunawachagua kama wawakilishi wa wananchi ni upuuzi mtupu, hawajawafikiria wananchi wa hali ya chini kwasababu siikitu kwao ilimradi wao na familia zao wapo salama.
Si amesema mwenyewe ameziba masikio .na kuamua kukaakimya
 
Kijijini mtu maskini mkulima hiyo kilimo Cha kujikimu au mtembeza Au kondakta wa daladala au dereva au muuza Genge au mama nitilie bima ya afya anachangia shilingi ngapi?
Zitatungwa kanunu, sheria ikishapata za Mhe. Rais kinachofuata ni kutunga kanuni(regulations) ambazo ndizo huweka utaratibu wa ufanisi wa sheria
 
Watu watakufa kama maji uhudumiwe bure nanani kama bima tu unayoilipia ni tabu ndio hii nj suicide mission.
Nakumbuka kauli hii Trump alimwambia Kim kuwa 'The rocket man is in suicidal mission'
ahahaha wazungu bwana!
 
Kijijini mtu maskini mkulima hiyo kilimo Cha kujikimu au mtembeza Au kondakta wa daladala au dereva au muuza Genge au mama nitilie bima ya afya anachangia shilingi ngapi?

Wewe mwenye uwezo utakuwa unamchangia asiye na uwezo...
 
Hao wachache mmeshindwa kuwahudumia je hao wengi itakuwaje? Report za CAG mmeweka kwapani wakati zilianinisha uozo wote kwenye malipo ya NHIF.Situmii hiyo Bima yenu na silipii bora nibaki Jubelee Au Assemble Au Strategy nijue nimefunga mkataba na bima ya Mwaka mzima kuliko sarakasi za dawa hakuna kupata rufaa mpaka Dr umlilie
Hiyo bima waje watuambie itatumika Hadi private? Juzi nimeenda zahanati ya serikali na bima yangu ya nhif, nimeambiwa dawa moja hawana nikanunue......na sio mara moja naambiwa hivyo......na hapo wanapita na mshahara wangu kila mwezi.
 
Watanzania tulio wengi mambo muhimu kama haya hatuyapi attention ila ngoja usikie V8 la Mh. Waziri limepata ajali usiku wa kuamkia leo ndio utaelewa vizuri.
 
Wazee hii sheria nilikuwa Sijaisoma ni ngumu sana...
Watu watafungwa sana...Naanza kukumbuka miaka ya 80 na 90 mwanzoni kodi ya Kichwa...
So sad isome vizuri..
Soma Kifungu cha 37 ,38 na 39...

Kwakuwa ni lazima Hakuna mtu hatatakiwa kutojiunga na usipojiunga utakamatwa na utalipa faini si chini ya laki sita na Utalipa Riba ya 10%
 
Hilo zoezi haliwezi kufanikiwa kamwe,kwanza wameaza tayari ubaguzi kati ya walionacho na wasionacho
 
Hiyo bima waje watuambie itatumika Hadi private? Juzi nimeenda zahanati ya serikali na bima yangu ya nhif, nimeambiwa dawa moja hawana nikanunue......na sio mara moja naambiwa hivyo......na hapo wanapita na mshahara wangu kila mwezi.
NHIF haipo limited kwa vituo vya serikari, inafanya kazi hadi kwa private provided ameingia mkataba nao.
 
Hilo zoezi haliwezi kufanikiwa kamwe,kwanza wameaza tayari ubaguzi kati ya walionacho na wasionacho
Probably kwasababu wameruka sana vitu vingi kuharakisha kitu ambacho hawakiwezi. Mfano mzuri ni misamaha, inaua vituo vya afya vingi chakustaajabisha serikari hailipii cost zinazotokana na misamaha. Wameruka sana stage nyingi. Sijajua wanapapara gani.
 
Back
Top Bottom