Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Rais Samia ametoa agizo hilo Agosti 08, 2026 wakati kufunga rasmi Maonesho ya Nane Nane Kitaifa na Kimataifa yaliyofanyika katika Viwanja vya Dkt. John Samuel Malecela jijini Dodoma.
Amesisitiza kuwa makundi hayo yote mawili yana umuhimu mkubwa katika uzalishaji na ukuaji wa uchumi wa nchi, hivyo ni muhimu kuweka mazingira yatakayowawezesha kufanya shughuli zao kwa amani na tija.
Katika hatua nyingine, Naibu Katibu OWM-TAMISEMI, anayeshughulikia masuala ya Afya, Prof. Tumaini Nagu, amesema Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wananchi kuongeza uzalishaji na kuboresha maisha yao, hususan kupitia fursa zinazotolewa na Serikali za Mitaa.
Aidha, Prof. Nagu amesema kuongeza tija katika kilimo hakupaswi kuishia katika uzalishaji wa mazao pekee, bali kunapaswa kuhusisha hatua zote za mnyororo wa thamani, ikiwemo uzalishaji, uchakataji, uhifadhi, usafirishaji na upatikanaji wa masoko.
Amesema Maonesho ya Nane Nane yameendelea kuwa jukwaa muhimu la kuwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo, kutoa elimu, kuonesha teknolojia na ubunifu katika uzalishaji, pamoja na kujadili fursa zinazoweza kuongeza tija na thamani katika sekta ya kilimo.