Rais Samia aingia amependeza Kikaoni kuwahi kutokea, wengi watamani Ushonaji wake wa Nguo uigwe kwenye vazi la Taifa

Rais Samia aingia amependeza Kikaoni kuwahi kutokea, wengi watamani Ushonaji wake wa Nguo uigwe kwenye vazi la Taifa

Ila Mkuu wewe sio Chawa Tu... Wewe ni FUNZA kabisa Mkuu...😀😀👋👋
Subiri Maandiko ya kumsifia Wasira yatakavyomiminika hapa jukwaani Ndio utajua kwamba mashuleni 21centiry skills zinafaa kufundishwa
 
Wote akili zenu sawa na huyo mama yako hata sishangai kwanini mlipata division 0 form four.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa hakika ikiwa upo mbali na Tv yako basi nenda hata migawahani au vibanda umiza au hata kwa jirani mwenye Tv ushuhudie kinachoendelea Dodoma. kwa sababu ikiwa upo mbali na Tv au matangazo ya moja kwa moja kutoka Dodoma . Basi utakuwa unakosa Mambo mengi sana hapa Duniani.

Rais Samia ameingia Leo kikaoni kibabe kwelikweli.
ameingia akiwa Amependeza kuwahi kutokea au kushuhudiwa kwa kiongozi yeyote yule wa ngazi ya juu kuwahi kuingoza au kushika nafasi yoyote ile ya kiserikali mahali popote pale Duniani na kwenye vikao vyovyote vile Kuwahi kufanyika.

Walio kuwa wanamuona akiingia wengine walishindwa kumtambua kwa haraka haraka. kwa hakika tumepata Rais kwelikweli. Rais Wa viwango ,Rais mwenye utimamu wa Mwili na akili, Rais shupavu ,hodari, madhubuti,imara na makini kwelikweli.Rais anayejua ukubwa na umuhimu wa nafasi yake.

Unajua Ipo hivi. Rais na Mkuu wa Nchi ni kioo cha Nchi au Taifa. ni Nembo yetu sisi watanzania.Ni taswira ya Nchi,Mtu akitaka kutujua watanzania vyema akili zetu zilivyo anaweza kumuangalia RAIS wetu alivyo na viongozi waliomzunguka.

.Ni aibu na inakuwa aibu kwa Taifa zima ikiwa mnakuwa na kiongozi mkuu wa Nchi mshamba mshamba na asiye na mpangilio hata wa mavazi yake tu. Haelewi avae vipi na wakati gani na kwa mazingira gani na kwa matukio gani na eneo lipi na kwa hali ya hewa ipi na ukanda upi.

Siyo mna Rais anatoka na anaingia kikaoni amevaa zake masweta mazito utafikiri watalii wanao jiandaa kupanda mlima Kilimanjaro huku akijua yupo eneo na mkoa wa joto kali kama Dar es salaam. matokeo yake muda wote anajikuta anatokwa na jasho tu uso mzima utafikiri anachoma au anaopoa mkaa Juani au anachoma tanuri la matofali kule maeneo ya Mbozi mbugani.

Rais Samia kiukweli anatufanya watanzania tujisikie fahari sana kuwa Naye madarakani. mpaka inafikia Watanzania wanatamani aina ya ushonaji wake wanguo ungeigwa katika vazi la Taifa .View attachment 3204382

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Rubbish
 
Nimecheka na natamani niijue maana ya mbwira! Kwamba kijana aliyesoma Kwa Kodi za watanzania anaona kwenye mkutano wa chama chenye madaraka ya kuongoza nchi ni kumsifia mtu Kwa namna alivyovaa na jinsi mshono ulivyopendeza badala ya kuzungumzia ajenda zenye matokeo chanya Kwa Taifa mathalani
1. Ukosefu wa usalama
2. Demokrasia
3. Rushwa
4. Ukosefu wa huduma Bora za afya na Bima ya afya kwa wote
5. Miundombinu duni
6. Ukosefu wa Ajira
7. Elimu isiyokidhi matakwa ya sasa kitaifa na kimataifa
8. Namna Gani rasimlimali watu na asili zinavyoweza kutumika kuleta maendeleao endelevu
9. Mabadiliko ya Tabia nchi na athari zake kiuchumi na kijamii!

Hili toto ni Mbwira kweli!

“Mbwira “ - Mjumuisho wa Tabia zake za hovyo
 
Hayo uliyoyaandika yametekelezwa vyema sana na serikali yetu chini ya uongozi shupavu, imara na madhubuti wa Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan
 
Mimi siwezi kujitekenya unayejitekenya ni wewe kunguni unayeacha kujadili mambo ya kitaifa na kuangalia trivial issue kama vazi la kiongozi.
Mambo ya kitaifa yapo vyema na yanaendelea vizuri .hili ni la kitaifa zaidi kuliko hata hayo mengine
 
Mambo ya kitaifa yapo vyema na yanaendelea vizuri .hili ni la kitaifa zaidi kuliko hata hayo mengine
Zero ya kwenye vyeti haiwezi kukosewa hadi kwenye kufikiri katika uhalisia tutajikuta tu tumekujua uwezo wako na ulichopata shuleni.

Kwakuwa wewe ulienda kusindikiza wenzio basi endelea kulamba buku 7 kutetea uongo humu.
images (91).jpeg
 
Back
Top Bottom