Kumbe hata kusoma napo ni tatizo.Sasa gazeti hili lanini hapa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kumbe hata kusoma napo ni tatizo.Sasa gazeti hili lanini hapa.
Dada Lucy wewe umeshashona nguo kama ya Samia?Ndugu zangu Watanzania,
Kwa hakika ikiwa upo mbali na Tv yako basi nenda hata migawahani au vibanda umiza au hata kwa jirani mwenye Tv ushuhudie kinachoendelea Dodoma. kwa sababu ikiwa upo mbali na Tv au matangazo ya moja kwa moja kutoka Dodoma . Basi utakuwa unakosa Mambo mengi sana hapa Duniani.
Rais Samia ameingia Leo kikaoni kibabe kwelikweli.
ameingia akiwa Amependeza kuwahi kutokea au kushuhudiwa kwa kiongozi yeyote yule wa ngazi ya juu kuwahi kuingoza au kushika nafasi yoyote ile ya kiserikali mahali popote pale Duniani na kwenye vikao vyovyote vile Kuwahi kufanyika.
Walio kuwa wanamuona akiingia wengine walishindwa kumtambua kwa haraka haraka. kwa hakika tumepata Rais kwelikweli. Rais Wa viwango ,Rais mwenye utimamu wa Mwili na akili, Rais shupavu ,hodari, madhubuti,imara na makini kwelikweli.Rais anayejua ukubwa na umuhimu wa nafasi yake.
Unajua Ipo hivi. Rais na Mkuu wa Nchi ni kioo cha Nchi au Taifa. ni Nembo yetu sisi watanzania.Ni taswira ya Nchi,Mtu akitaka kutujua watanzania vyema akili zetu zilivyo anaweza kumuangalia RAIS wetu alivyo na viongozi waliomzunguka.
.Ni aibu na inakuwa aibu kwa Taifa zima ikiwa mnakuwa na kiongozi mkuu wa Nchi mshamba mshamba na asiye na mpangilio hata wa mavazi yake tu. Haelewi avae vipi na wakati gani na kwa mazingira gani na kwa matukio gani na eneo lipi na kwa hali ya hewa ipi na ukanda upi.
Siyo mna Rais anatoka na anaingia kikaoni amevaa zake masweta mazito utafikiri watalii wanao jiandaa kupanda mlima Kilimanjaro huku akijua yupo eneo na mkoa wa joto kali kama Dar es salaam. matokeo yake muda wote anajikuta anatokwa na jasho tu uso mzima utafikiri anachoma au anaopoa mkaa Juani au anachoma tanuri la matofali kule maeneo ya Mbozi mbugani.
Rais Samia kiukweli anatufanya watanzania tujisikie fahari sana kuwa Naye madarakani. mpaka inafikia Watanzania wanatamani aina ya ushonaji wake wanguo ungeigwa katika vazi la Taifa .View attachment 3204382
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Ni funza wale matekenya kabisaIla Mkuu wewe sio Chawa Tu... Wewe ni FUNZA kabisa Mkuu...😀😀👋👋
Uwe na adabu kwa kaka zakoDada Lucy wewe umeshashona nguo kama ya Samia?
Tuna watu wengi wa sampuli ya Mwashambwa ndiyo maana hii nchi imebaki nyuma sana kwenye kila kitu, wanajua watu kumbe wanashindwa kununua TV ili waangalie mama Abdul alivyovaa. Aliyeleta mada anajua kuwa watanzania zaidi ya asilimia 75 hawana umeme na walio na umeme unakatikakatika halafu yeye anasherekea mama kuvaa dera za kijani? Hivi ufikiri wetu watanzania upoje, hii mada ingekuwa nchi nyingine mtoto wa miaka mitano angeidharau. Nchi hii ilikuwa na mkuu wa mkoa aliyesema Mungu amshukuru Magufuli kwa aliyoyafanya. Jamani, what do these people have in their brains?
Inuka na uangaze utazame namna Tanzania ilivyoendelea na kupata maendeleoTuna watu wengi wa sampuli ya Mwashambwa ndiyo maana hii nchi imebaki nyuma sana kwenye kila kitu, wanajua watu kumbe wanashindwa kununua TV ili waangalie mama Abdul alivyovaa. Aliyeleta mada anajua kuwa watanzania zaidi ya asilimia 75 hawana umeme na walio na umeme unakatikakatika halafu yeye anasherekea mama kuvaa dera za kijani? Hivi ufikiri wetu watanzania upoje, hii mada ingekuwa nchi nyingine mtoto wa miaka mitano angeidharau. Nchi hii ilikuwa na mkuu wa mkoa aliyesema Mungu amshukuru Magufuli kwa aliyoyafanya. Jamani, what do these people have in their brains?
Muoneni mjumbe wa CCM huyuAcha kuropoka ropoka Hovyo hovyo tu
Unamuonea wivu mjinga kweli?Acha wivu