Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema Tume ya Uchunguzi ya masuala ya vurugu za uchaguzi haitachunguza tu matukio ya uvunjifu wa amani, bali pia kauli na matamshi yaliyotolewa na baadhi ya vyama vya upinzani kabla na wakati wa uchaguzi.
Amesema hatua hiyo inalenga kupata picha kamili ya chanzo cha kilichojitokeza, hususan pale viongozi wa vyama hivyo walipotoa kauli za kuchochea taharuki kama vile
“lazima kiwake”, “hapakaliki”, “lazima aondoke”, “uchaguzi hautafanyika.”
Akizungumza leo jijini Dodoma, Ikulu ya Chamwino, wakati akizindua rasmi Tume Huru ya Uchunguzi wa matukio ya vurugu wakati na baada ya uchaguzi mkuu, Samia amesema: