PostGE2025 Rais Samia aipa Tume Huru kazi nzito: chunguzeni hata kauli za vyama vya upinzani kama vile 'Lazima Kiwake'

PostGE2025 Rais Samia aipa Tume Huru kazi nzito: chunguzeni hata kauli za vyama vya upinzani kama vile 'Lazima Kiwake'

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
mbona unaangalia upande mmoja , wapo waliosema wataua watakaoandamana , je hawa tuwapuuze mpk sku wakikuua ww ?wapo waliosema watavunja watu miguu je hawa tuwapuuze mpk wakikuvunja ?

Pia za chini chini ni kuwa walioiba maduka ya watu kuanzia trh 30 ni polisi wenu maana raia walikuwa ndan
Hili nilisema mapema yaani tukitaka tuguse kila pande kwa haki na watu wa wajibishwe basi hii list lazima ichunguzwe hawa, kinyume chake ni ushabiki tu na kuweka hisia

1)Samia kama mkuu wa Nchi

2)Lissu/Heche viongozi wa upinzani na kwa mujibu wa kauli zao hasa kabla ya uchaguzi na bahati kuna kumbukumbu ya video/picha mjongeo za matamshi yao

3)Gwajima kwa sababu ya matamshi yake kabla ya uchaguzi

4)Wanaharakti na hasa hao wanaotokea nje na hasa Mange na Maria

Hawa ni kwa uchache ktk wengi wao wanao takiwa kuchunguzwa kwa shida hii

TEC/Bakwata nao wahusishwe na ijulikane hasa dhamira zao na ushiriki wao na hasa hasa hawa TEC nao ndo wana complicity the issue hii pia
 
Tume inaelekezwa ikachunguze kile na hapo bado unaiita tume huru.Au ndiyo uwezo mdogo wa kushindwa kuelewa maan ya neno huru
Tume inaelekeZwa cha kuchunguza halafu mnaita tume huru, kwanini hajasema wakachunguze na wanaoteka watanzania na kuwaua.?
 
Kuna mtu ameshachanganyikiwa. Hakika amechagua ngumu sana ya kupita. Huku anakotaka kwenda ndiyo kubaya zaidi kwa sababu atazidi tu kujiharibia Kuwaletea ubabe watu waliokata tamaa! Na ambao hawana kitu cha kupoteza; ni balaa lingine kabisa.

Gen Z, kazi kwenu vijana wangu. Mtu wenu huyo hapo nawakabidhi kwa ajili ya D9. 🙌
 
Mbona umesahau na jeshi la polisi na kauli zao za vitisho?
Mkuu nimesema hapo kama uchunguzi usiwe kwa upande wa dola tu (Rais akiwa muwakilishi dola na labda hata hajatoa amri yoyote kwa lolote) na hapo kuna taasisi nyingi chini yake zinaingia na hao uliowataja

Lakini uchunguzi utakuwa batili kama hautaangazia hao wengine walio tengeneza mazingira ya ku provoke, kwahiyo wapinzani wachunguzwe, wana harakati pia na baadhi ya viongozi wa dini na wengine kuna video zao wakisema watakinukisha mara nchi haitatawalika nao hao wapate haki yao ya hukumu kwa kuhamasisha vurugu na mauaji

Kwahiyo uchunguzi ni suala moja na baada ya uchunguzi ni nani amehusika kabisa ndo wataona wao inavyo faa. Uchunguzi wa haki ubebe wote hao usiegemee upande wa dola tu
 
mbona unaangalia upande mmoja , wapo waliosema wataua watakaoandamana , je hawa tuwapuuze mpk sku wakikuua ww ?wapo waliosema watavunja watu miguu je hawa tuwapuuze mpk wakikuvunja ?

Pia za chini chini ni kuwa walioiba maduka ya watu kuanzia trh 30 ni polisi wenu maana raia walikuwa ndan
Ukisema polisi wenu /wangu una maana ipi? Polisi ni chombo kilichopo kwa mujibu wa sheria, sasa kama unaona kuna mapungufu kwa uwepo wao sio tatizo langu ni lako na kwangu sina ufumbuzi wa tatizo lako hilo

Kama kuna kauli zilitoka kwa upande wowote, ndo maana tume ya uchunguzi itasema ikikamilisha kazi yake
Ninachopinga kuonyesha ni tatizo la dola tu hili wakati kuna hao wapinzani,baadhi ya viongozi wa dini na wana harakati baadhi nao ndo wametufikisha hapa tulipo

Hivi kusema tutakinukisha,nchi haitatawalika, tunaleta uasi unaona ni maneno madogo hayo mkuu wangu?

Au waraka uliotoka wa baadhi ya madhehebu ya dini na kuzidi kuamsha moto badala kupunguza au kuuzima na mbaya inatoka kwa viongozi wa dini/kiroho
Unajiuliza kuna agenda zipi haya makundi yana zi sukuma kwa mgongo wa damu(tena wengi vijana wadogo wa ki masikini na wasio na elimu kubwa na hata exposure) achia mbali uharibifu wa mali na miundo mbinu yetu

Mie nipo kundi kubwa la watu ambao hatuna upande lkn kuna nyie wa pande zote mbili mna inajisi nchi yetu nzuri
 
Back
Top Bottom