PostGE2025 Rais Samia aipa Tume Huru kazi nzito: chunguzeni hata kauli za vyama vya upinzani kama vile 'Lazima Kiwake'

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Iwapo uuaji na utoweshwaji wa maiti za waliouwawa utachunguzwa,bila shaka hata kauli za ma Sheikh ubwabwa zitachunguzwa pia,hata zile kauli za kifo ni kifo,na zile za hakuna nywi nywi wala nyinyi hata zile tunyooke nao wanaowasema ccm hata kama ni wenzao ama,zile za ushindi ni kazi ya sirikali hata zile za hata mkipiga huku ushindi ni wetu na hata zile za mabao ya mkono.Mambo ni mengi muda mchache dunia subiri nishuke nimechoka mno!
 
Mbona umesahau na jeshi la polisi na kauli zao za vitisho?
 
Safi sana, hao ndio wanaongoza kuchochea ugaidi
 
Utapeli tu hapa ile tume ya Haki na jinai imeishia wapi. Watanzania na hawa watoto sio wajinga jinga tena
 
Tume gani HURU inaelekezwa namna ya kufanya kazi? Sa100 aache usanii
 
Mbona ipo predictable sana wandugu, inajulikana straight anamlenga nani! Hapo kwa kuwa kaambiwa hamna maridhiano bila uwajibikaji sasa anataka kutumia kete ya kutorture kwa vyombo vya mabavu. Huyu mama alipata division gani? Mbona mwepesi sana jamani? Karne hii ndio tunakua na rais wa hivi wazee???

So sad, naamini kuna kosa kubwa sana tulimkosea Mungu wabongo maana sio kwa adhabu hizi, left, right, back and forward dah
 
Aliposema hakutakuwa na nywi×3 alikuwa na maan ipi hasa?
Alijua atapiga risasi na kuua ? Tume ichunguze hizi kauli kweli.
 
Tume yake ya Mfukoni! Sijui ameipa muda gani mpaka ije kutoa ripoti?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…