Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Rais Samia Suluhu Hassan siku ya leo ameidhinisha kupandishwa hadhi kwa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji kuwa Halmashauri ya Mji, na Halmashauri ya Mji wa Geita kuwa Manispaa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa, alitoa taarifa hiyo leo, Disemba 13, 2024, wakati wa hotuba yake kwa wananchi wa Rufiji.
Tukio hilo lilifanyika katika uwanja wa Ujamaa, Ikwiriri, ambapo mamia ya wananchi walikusanyika kushuhudia uzinduzi wa Tamasha la Bibi Titi Mohamed.
"Bibi Titi Mohamed huko aliko atakuwa anafurahia sana maendeleo ya Rufiji maana ndiye Mbunge wa kwanza aliyeasisi jimbo hili alifanya kazi kubwa sana na mimi Mbunge wa tisa naendeleza kazi aliyoianza Hayati Bibi Titi na pia Mhe. Rais amefanya kazi kubwa kwa kuleta miradi mingi katika Wilaya yetu na sasa ameipandisha hadhi kuwa Halmashauri ya Mji." amesema Mchengerwa
Ameeleza kuwa Rufiji kuwa halmashauri ya mji kutawezesha ufadhili wa miradi mikubwa ya Benki ya Dunia, kuharakisha maendeleo, kujenga masoko, kuboresha huduma za afya, na kuimarisha sekta ya elimu.
"Hivyo tunamshkuru Mhe. Rais kwa kuiona Rufiji na kuipa hadhi ya kuwa Mji na sasa maendeleo katika Wilaya hii katika nyanja zote yataenda kwa kasi zaidi." ameongeza Mchengerwa
Source: Jambo TV