Rais Samia aitisha na kuongoza kikao cha Baraza la Mawaziri Ikulu Chamwino

Kwakuwa Nape & Makamba bado hawajakabidhi ofisi I hope walikuwemo.
Naona wa Zenji wamepata wa kuwawakirisha mambo ya nje!
R.I.P Mzee Thabiti Kombo. Tulikuwa tunamsoma saaana kwenye somo la Siasa, mashuleni miaka ileeee! Nikabahatika kumuona LIVE mara moja tu,(nilikuwa ninamfahamu kupitia picha kwenye magazeti ya Uhuru/Mzalendo.)alipokuja kufungua JUMBA LA MAENDELEO (hall) la kiwanda cha nguo cha URAFIKI!
Mwanae, anazidi kusogea tu! Wa Mwalimu JK, aaaaaaaaa!!!!
 
Baba ukitaka kuandamana kesho yake unasahau au kuamka unaumwa kichwa haswa
Hakuna uchawi mbele ya nguvu ya umma..ni sauti ya Mungu.: Uchawi wanao..sawa..Niliwahi kukabiliana na CCM kwenye by election-2013 ya Mwenyekiti wa Kijiji kinaitwa KABIGA-huko Nyangh' wale mpakani mwa Mkoa wa Mwanza na Geita nikiwa CHADEMA,ilikuwa wiki moja ya kampeni za kufa na kupona..CCM wametuchangia wa Mwanza na Geita.Tumetoka Geita Mjini tukiwa 5 tu, Dada 1 wa Bawacha na siye MME 4 na mkweche wetu wa Lover wao na Cruser mpyaaa.Poli-CCM wakawazila CCM kwamba hawana mafuta ya Difenda..Tulitawala Kijiji jombaa chini ya Red-brigade. :Usiku wa kuamukia siku ya kupiga kura tuliwakamata CCM wakiwa wanamwaga dawa za kienyeji walahi kwenye kisima cha wazi cha maji ya kunywa wana kijiji.Sikuamini macho yangu..wakatimuka na kuacha baadhi ya tunguli pale...Lakini kesho yake Mgombea wetu wa CHADEMA alishinda kwa kishindo cha kutisha.
 

Magufuli alishamuwekea msingi mzuri .... Haya MaCCM ni kuyatia woga tu, kazi imeisha. Baada ya hapo utaiendesha nchi kwa kadri unavyopenda mwenyewe .... Hata ukitaka kuchagua Mweza wako kuwa Waziri au Balozi hilo linawezekana pia.
 
Katika hatua za mwisho mwisho kuandaa maandamano ya kupinga president mtarajiwa kudhalilishwa.
 
Hivi hauelewi maana ya kutenguliwa?
Kutenguliwa ni lugha ya staha, lakini kiuhalisia ni kufukuzwa.
Kwa mfano Ruto alipovunja baraza la mawaziri na kuwatwua tena wale wale je hiyo utasema walifukuzwa? Huko ni kumbadili unafukuzwa ikiwa umemsikiliza mtu na hukukubaliana na utetezi wake na ukasema nakufukuza lakini hii discretional power watu hawafukuzwi bali wanabadilishwa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…