Rais Samia akagua Daraja la Kigongo-Busisi Mkoani Mwanza, leo Juni 14, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua daraja la Kigongo - Busisi mkoani Mwanza leo tarehe 14 Juni, 2023.




Muonekano wa Daraja la Daraja la JP Magufuli (Kigongo-Busisi km 3) linalounganisha Wilaya za Misungwi na Sengerema Mkoani Mwanza ambalo Ujenzi wake umefikia asilimia 75 na unatarajiwa kukamilika mwezi Februari, 2024.​

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Wananchi wa Buhongwa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza alipokuwa njiani akielekea Busisi kwa ajili ya kukagua Maendeleo ya Ujenzi wa Daraja tarehe 14 Juni, 2023.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mama Mzazi wa Mama Janeth Magufuli (Juliana Stephano Kidaso) mara baada ya kuwasili Sengerema Mkoani Mwanza tarehe 14 Juni, 2023.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS ) Eng. Pascal Ambrose wakati akikagua Daraja la JP Magufuli (Kigongo-Busisi km 3) ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 75. Mhe. Rais Samia amekagua Daraja hilo ambalo Ujenzi wake unatarajiwa kukamilika Februari, 2024.

Viongozi mbalimbali wa Serikali wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati alipokuwa akiwasalimia Wananchi wa Sengerema na Buchosa Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza tarehe 14 Juni, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza mmoja wa Wataalamu wa Ujenzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo-Busisi km 3) Eng. Abdulkarim Majuto wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wake Mkoani Mwanza.
 
Ile ripoti ya CAG ilibainisha wizi mkubwa mkubwa TANROADS.
 
 
huku tumezuiliwa Ili tuonekane tupo wengi kwenye mkutano wao .hakuna abiria kuvuka
Nakusihi usihadae watu.
Nakumbuka mambo haya ya kuzuia watu kwa muda mrefu, Makamu wa Rais aliyazuia akiwa huko huko Kwanza.
 
Nakusihi usihadae watu.
Nakumbuka mambo haya ya kuzuia watu kwa muda mrefu, Makamu wa Rais aliyazuia akiwa huko huko Kwanza.
tumelalamika sana .ferry 2 zimezuiliwa kuondoka mpaka mwenye nchi amalize hotuba yake na kuondoka ndio turuhusiwe.hii nchi ngumu sana.wao wanatumia daraja la dharula sisi tunatumia ferry ila imekuwa nogwa sisi tukienda maana wanaona watabaki wenyewe hapa busisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…