Rais Samia akataa mwananchi kueleza shida kwenye mkutano, amtaka amfikishie kupitia mbunge

Tatizo ni wasaidizi wa rais. Inakuwaje hawajutafuta hizo info mapema. Clip kama hizi zitammaliza rais Dkt Samia 2025. Maana kauli ka hiyo inaonesha ukaidi. Jamani hakika Dkt Samia anahujumiwa.
Anahujumiwa na nani? Alishasema mabango ya malalamiko hataki! Anataka mabango yale ",Unaupiga mwingi, Umeunganisha Taifa" na hataki ata kusikia wananchi wake wanasemaje! Ila kusaini mikataba ya ovyo na kuja kuitetea aaanhh hapo ndo pake.
 
Halafu 2025 mnaanza kupita nyumba kwa nyumba kumwombea kura sio?
 
Wtf
 
Ili iweje? Rais hawezi kusikiliza kero za mtu mmoja mmoja, na hata akisikiliza hawezi kufanya maamuzi hapo kwa hapo, maana inawezekana huyo mwananchi akawa anapotosha pia. Kama yule mama wa Tanga alivyompotosha Magufuli
Subiri apotoshe ndipo useme amepotosha kusikilizwa ni lazima. Na mtu sahihi wa kusema atamletea alikuwa ni mkuu wa wilaya, mbunge anaweza asifikishe malalamiko kwa kwa rais kwani anajua 2025 sirudi tena bungeni ya nini kuangaika na hawa wananchi.
 
Pamoja na mazuri na mabaya ya the late JPM,
Tulipata rais wa aina yake na alikua raisi na mtetezi wa wanyonge.....

Magufuri alikulia maisha ya kimasikini masikini udogoni mpaka alikua anasemaga aliwai kuuza NTALALI NA NS'UNGWI na NFULU wasukuma wanaelewa......

Hata kuja kupatikana kama JPM yaan hakuwa anajitenga na watu alikua ni msikivu na katili sometimes.........

Najua hata nisipo kuja kua kiongozi au Rais wa JMT ila moyo wangu una amani sababu Kuna mtu ameishi maono yangu Mimi ni kama JPM tunafanana kwenye misimamo, kuongoza, udikteta, kusimamia nacho amini...

JPM nilitofautiana nae kwenye mengi kimtazamo sometimes ila namkubali sana Huyu BABA angu mdogo JPM

RIP JPM
 
Akili ndogo sana hii
 
Tatizo ni wasaidizi wa rais. Inakuwaje hawajutafuta hizo info mapema. Clip kama hizi zitammaliza rais Dkt Samia 2025. Maana kauli ka hiyo inaonesha ukaidi. Jamani hakika Dkt Samia anahujumiwa.
Anajihujumu.
Angesikiliza kisha maamuzi yangetolewa baadae. Hii ingeonesha anajali.
 
Anahujumiwa na nani? Alishasema mabango ya malalamiko hataki! Anataka mabango yale ",Unaupiga mwingi, Umeunganisha Taifa" na hataki ata kusikia wananchi wake wanasemaje! Ila kusaini mikataba ya ovyo na kuja kuitetea aaanhh hapo ndo pake.
Kuna wakati mambo haya yanatia kichefu chefu.
Unatia saini mkataba wa hovyo pili unatoa pesa mkataba ukatetewe kumbafu sana
 
Amesimama kuwasalimia wananchi
,malalamiko na shida zao zina mifumo yake ya kupokelewa.
 
Tatizo walijazwa upepo na yule mwigizaji au bwana yule
Yule mhuni alikuwa comedian pro max. Alikuwa anaandaa wauliza maswali na anakuwa ameandaa script ya namna ya kutatua "changamoto" fake anayopewa.

Kuthibitisha hili, angalia majibu ya mhuni huyu alipokuwa anakutana na changamoto halisi. Mfano pale Mbezi stendi kuna mwananchi alilalamikia gharama kubwa ya kulipia choo (sh 500/=). Mhuni alimfurishia matusi mwananchi yule mbele ya kamera huku TV zote zikiwa live. Alisema "kama unaona kubwa beba mavi yako peleka nyumbani".

Kuna pahala pengine (sikumbuki ni wapi). Aliamuru mwananchi awekwe ndani baada ya jiwe kutwangwa na changamoto ngumu.

Jiwe alikuwa siyo mtu. Afe tena huko aliko.
 
Rais hajatokana na kura za wananchi ili kuwa rais hivyo hawezi kujua shida za wananchi zikoje.
 
Anasimama barabarani kusalimia, au kutoa majibu ya matatizo aliyopewa na kuhusu hilo eneo na mbunge wao... Ndio maana ya representative democracy
Kama ni hivyo huyo mbunge si ndio angepeleka hayo majibu? Au ni mambo ya kujimix?
 
Umechanganyikiwa
 
Dalili za moyo kukata tamaa.

Hivi wale wazee wa ule moshi wa wakati ule ni kweli wote walikimbilia malawi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…