Rais Samia akataa mwananchi kueleza shida kwenye mkutano, amtaka amfikishie kupitia mbunge

Kuna pahala pengine (sikumbuki ni wapi). Aliamuru mwananchi awekwe ndani baada ya jiwe kutwangwa na changamoto ngumu.

Jiwe alikuwa siyo mtu. Afe tena huko alaliko.
Hii ilikuwa bukoba nilikuwemo
 
Tatizo ni wasaidizi wa rais. Inakuwaje hawajutafuta hizo info mapema. Clip kama hizi zitammaliza rais Dkt Samia 2025. Maana kauli ka hiyo inaonesha ukaidi. Jamani hakika Dkt Samia anahujumiwa.
haujumiwi anajihujumu mwenyewe mimi naona huyu mama hatagombea 2025 kaishachoka sana
 
Kuna watu ambao haki zao ziliminywa kwa kila kitu na walijaribu kufuata kila hatua lakini hawakusikilizwa, ila kupitia safari kama hizi za mtangulizi wa nafasi hiyo, wapo wengi walipata haki yao kwenye vitu ambavyo kote kwenye mamlaka za uamuzi ilishindikana.

Ni uamuzi wake kama ilivyo kwako wewe na wengineo kuukubali ama kuukataa utaratibu huo.

Ila kwa upande wangu naona ni sawa tu, ukisikiliza wananchi wawili au watatu sio mbaya, katika nchi ambayo kupata nafasi hiyo adhimu ambayo ni adimu sana, sidhani kama kuna kitu ambacho kwa nafasi yake hawezi kutoa uamuzi wala maelekezo.
 
Huyu ndio mtu mnasema tatizo lake ni amezungukwa na watu wabaya 🙂 🙂 🙂 🙂, what a joke
 
Hapana, Rais anatakiwa ashughulike na mambo ya kitaifa. Huyo raia unaweza kukuta analalamikia kesi ya mirathi ya familia yao au kucheleweshwa mshahara kazini kwake.
Umejuaje swali alilokuwa anataka kuuliza. Kuna muda inabidi Raisi awe humble tu kusikiliza kero za wananchi direct hasa anapokiwa na msafara kama hapo. Kuna cases nyingine huwa watu wanahangaika na kudhulumiwa haki zao, chance kama hiyo ndio anaona tatizo lake litapata suluhu.
 
wagombea urais muwe mnachagua makamu wenu vizuri. hili nalo sijui liingizwe kwenye katiba?
 
I don't support her regine, ila kwa hilo amefanya sahihi. hatakiwi kuwa yule mtu anasikiliza kila mwananchi, halafu anajikuta amefanya maamuzi ya haraka kwa kusukumwa na kadamnasi ya watu bila kusikiliza upande wa pili, au niseme tu hatakiwi kuwa kama magufuli aliyekuwa anatoa hukumu bila uchunguzi tena mbele za watu.
 
kilichomsimamisha hapo ni nini kama hataki kusikiliza watu?? amalize muda wake aondoke hatumtaki huyu mwarabu koko
 
Mbunge naye anaweza kataa akasema akamueleze shida zake mwenyekiti wa kijiji. Huwenda kero ya huyo mwananchi inasababishwa na huyo huyo mbunge wao.
 
Kuwa rais wa watu ni pamoja na kuwasikiliza wananchi wako shida zao. Wabunge wapo ila hawana rekodi ya kusikiliza shida za mtu mmojamoja. Rais angeiga tu style ya mtangulizi wake alivyoonekana kuwajali wanyonge
 
Hata kwa katiba hii ya sasa yapo ambayo kwa nafasi yake Rais bado hawezi kutoa uamuzi.
 
Mbunge naye anaweza kataa akasema akamueleze shida zake mwenyekiti wa kijiji. Huwenda kero ya huyo mwananchi inasababishwa na huyo huyo mbunge wao.
Kama ni kero binafsi anaweza kwenda polisi au mahakamani, kama ni kero ya wananchi wengi mwenyekiti wao wa mtaa, kijiji au diwani ndio mtu sahihi.
Tatizo leni mmefanya Rais kuwa mtenda miujiza na mnataka viongozi na watendaji wengine wawe wanalipwa tu bila kufanya majukumu yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…