Rais Samia akataa mwananchi kueleza shida kwenye mkutano, amtaka amfikishie kupitia mbunge

Rais Samia akataa mwananchi kueleza shida kwenye mkutano, amtaka amfikishie kupitia mbunge

Sahihi kabisa, utaratibu wa Rais kusikiliza shida za mtu mmoja mmoja barabarani haufai
Aje ikitokea Kero ya Mwananchi ni huyo mbunge mwenyewe, itafika kwa rais?
Huwezi kusikiliza wote ndio, lakini walau sampling, ingetia matumaini kwa raia na uwajibikaji kwa viongozi.
 
Naona haikuwa sahihi. Kumuona Mbunge ili kumueleza kero ni ngumu sana. Na hata kufikisha kero kwa wasaidizi wa Mh Raisi wanaweza wasifikishe hizo kero kwa Raisi. Ingekuwa ni jambo la hekima kumsikiliza huyo mtu hapo Barabarani.
 
Naona haikuwa sahihi. Kumuona Mbunge ili kumueleza kero ni ngumu sana. Na hata kufikisha kero kwa wasaidizi wa Mh Raisi wanaweza wasifikishe hizo kero kwa Raisi. Ingekuwa ni jambo la hekima kumsikiliza huyo mtu hapo Barabarani.
Na unaweza kuta hadi huyo Mbunge Mama alisha muona lakini labda msaada wa Mbunge ni mdogo sana kwa Mama,na unaweza kuta Mbunge wake ndiyo alimshauri shida yake ni Rais pekee ndiyo ataweza itatua na ndiyo maana Mama akaamua kujitosa kwenye Kadamnasi! Na utaweza kuta Mama anasumbuliwa na maswala ya kudhulumiwa Mirathi tu! Mi kulikua na kesi moja Mpelelezi wa kesi mwenyewe akanishauri niende nikalalamike kwa Katibu Mkuu Office ya Rais, baada ya kuona kuna figusi kama wakubwa zake wamesha settle na watuhumiwa ndiyo maana Jalada haliendi mbele lime stack kwenye meza zao,na yeye mpelelezi kimamlaka hawezi waauliza "Wakuu vp mbona mzigo hausongi mbele"!!??
 
Sasa alisimama kufanya nn, kimsingi alisimama kusikiliza kero za wananchi alitakiwa awasikilize hata magufuli alipooba hili jambo ni dogo alikuws anawakataa kwa kuwaelekeza watu wa chini wayamalize. Yawezekana rais alikuwa sahihi kuelekeza kero akaipeleke kwa mbunge ila angemsikiliza kwanza yawezekana anayemtuma kwake yeye ndo changamoto mwenyewe
 
Rais Samia leo September akiwa mkoani Mtwara alisimamisha msafara wake kuongea na wananchi wa eneo hilo. Moja wananchi hao aliomba kuongea jambo ambapo Rais alimwambia mambo ni mengi na Tanzania ni kubwa.

Rais Samia alimtaka mwananchi huyo ampatie jambo lake mbunge kisha amfikishie Rais au wasaidizi wake.

Mwaka 2017 Rais Magufuli akiwa anaelekea Mtwara alisimamishwa Somanga na mwananchi aliyeelezea changamoto ya zahanati katika eneo hilo kutokamilika kwa miaka mingi. Rais Magufuli alichangia na kuamrisha ikamilike.

Alipopita tena barabara hiyo miaka 3 baadae mwananchi huyo alimzawadia jogoo kama shukrani ya kutimiza ahadi ya kufanyia kazi dukuduku lake na Magufuli alimsubiri mpaka alipomkamatia na kumpa. Alipofariki, mwananchi huyo alifunga safari kumzika Rais Magufuli mwaka 2021.

Mmeanza ujinga wenu. Sasa m unge ana kazi Gani? Tofautisha udictator na uongozi unafuata sheria na miongozo sahihi. Jpm alikuwa mtu wa mizuka tu ikipanda anaamua chochote bila kujali impact yake. Ndo mana midege yake inakamatwa kila Leo Samia anasawazisha kwa uongozi thabiti.
 
Ili iweje? Rais hawezi kusikiliza kero za mtu mmoja mmoja, na hata akisikiliza hawezi kufanya maamuzi hapo kwa hapo, maana inawezekana huyo mwananchi akawa anapotosha pia. Kama yule mama wa Tanga alivyompotosha Magufuli
Kwamba katiba inakataza Rais kumsikiliza Raia mmoja?
Je. Viongozi wanaowajibika Kwa Rais hawampotoshi Rais pia?
Katika nchi hii, kati ya kiongozi na Raia wa kawaida nani ana asilimia kubwa ya kumpotosha Rais?
 
Anasimama barabarani kusalimia, au kutoa majibu ya matatizo aliyopewa na kuhusu hilo eneo na mbunge wao... Ndio maana ya representative democracy
Mbunge. Mkuu wa mkoa. Mkuu wa wilaya. Diwani.
Hai wote wangeweza Kutoa majibu
 
Hawa jamaa wa kijani waoga balaa hapo anafikiri ya bandari yataibuka
 
Hapana, Rais anatakiwa ashughulike na mambo ya kitaifa. Huyo raia unaweza kukuta analalamikia kesi ya mirathi ya familia yao au kucheleweshwa mshahara kazini kwake.
Huko kwengine nako amesema kaziba masikio na case zengine kachagua kukaa kumya.
 
Sasa alisimama kufanya nini na alifuata nini huko haswa? Si angetulia ofisini kwake apelekewe na hao wabunge na wasaidizi wake!!!
 
Hapo alisema naagiza ma RC wote nchi kusghulikia matatizo yote yanayofanana na la Mwananchi huyu mara Moja na masuala mengine ambayo ni kero kwa Wananchi. Mchezo ungisha kiukaini!
Nchi haitakiwi kuendeshwa kienyeji hivyo
 
Sahihi kabisa, utaratibu wa Rais kusikiliza shida za mtu mmoja mmoja barabarani haufai
Kwanini sasa alisimamisha msafara? Rais wa sasa anajaribu sana kuiga style ya aliyemtangulia lakini wakati huo huo akiwa hapendi.

Yeye aje na style yake tofauti kama anaona hawezi kuwasikiliza Wananchi wanaokuwa wamekusanyika huko njiani awe anapita kwa kasi na msafara wake na atoe muongozo rasmi wa namna gani atapenda kufikishiwa kero za Wananchi,vinginevyo akisimama tu njiani wananchi wanakuwa na shauku ya kuongea hapo hapo kero zao maana walizoeshwa na awamu ya tano.
 
Kinachotakiwa ni .......yule mbunge kumuweka nje ya ubunge kwa lazima........hapo tutasikilizwa na kusikilizana.......siku hazigandi
 
Uongozi Huwa ni karama.


Huyu SAMIA , ni kama tu Mwijaku, alale aamke aamue ajiunge na CCM ili mambo yake yawe sawa, kuongea ongea Mara paa anapewa UDC .


Hamna kiongozi humo
DPW inamtesa sana.....hana majibu anajua CUF wamejaa huko hataweza kuwajibu
 
Back
Top Bottom