Rais Samia akizungumza leo Juni 12, 2026, wakati akihutubia katika Maadhimisho ya Miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), yaliyofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
"Nipongeze Benki Kuu kwa mpango wa ununuzi wa dhahabu ya ndani. Hadi kufikia mwezi Mei mwaka huu, kama alivyosema mwenyewe Gavana, akiba yetu—rasilimali yetu ya dhahabu tuliyoikusanya—ni tani 27.5, yenye thamani ya shilingi trilioni 10 za Kitanzania. Hapa tulipofika, si haba.
Kuanzia sifuri, na ndani ya miezi mingapi? Mwaka... mwaka mmoja na nusu, tuna tani 27,000 (ishirini na saba) na huenda tukawapita wale walioanza kabla ya sisi ndani ya bara letu la Afrika. Huu ni mfano mzuri wa kutumia rasilimali za ndani kuimarisha uthabiti wa kifedha wa taifa letu."
Pia soma:
BoT yasitisha kuuza akiba ya dhahabu kufuatia kushuka kwa bei katika soko la dunia