Wakuu barabara ya kutoka Kibaha maili moja hadi Morogoro ni kelo Sana, maroli ni mengi sana hii barabara imezidiwa Sana.
Unaweza ukatoka mkoani huko vzr tu unakuja kupoteza muda kipande hicho.
Mimi mheshimiwa Rais Samia akiipanua tu hii barabara kuwa njia sita kuanzia alipoishia Magufuli pale Kibaha maili moja hadi Morogoro kuwa njia sita mi nitaanza kumpigia debe rasmi mitano tenaaaa
Binafsi hata mimi sielewi Marais wanaofuatia kwa nini wasiongeze njia nyingine kwa barabara kuu hizi.
Ok kuna mpango wa bandari kavu kule Kwara Pwani Mlandiz lakin bado naona haitaweza kutatua shida za jam zilizopo.
Leo kujenga barabara kiwango cha lami kinafikia 1b hadi 1.5b sasa tunaweza kuweka mkakati tu wa miaka 30 ivi mwaka huu barabara ya Mwanza next Arusha nk.
Kama Marais waliopita walizijenga hiz barabara kuu kwenda na kurudi kwa nn Marais wanaofuatia washindwe wakati matumiz ya barabara na huduma zingine zimeongezeka leo tupo 60m kila nyanja imeongezeka
1. Dar to Mtwara
2.Dar to Arusha na Tanga/namanga
3.Dar to Mbeya/tunduma
4.Dar to Songea/mtwara
5.Dar to Mwanza/Kagera/mtukura/Rwanda
6.Dar to Kigoma na Tabora/burundi
Hiz barabara zilianza kuboreshwa kipindi cha Mh.Mkapa sasa tukiweka Mkakati wa taifa wa miaka 20 au zaidi kweli tusingesimaliza.
Kama tunakopa kwa ajili ya maendeleo kwa nini tusikope fedha kuboresha barabara hizi ambazo kiuchumi zinalipa sana nje na ndani ya nchi
Na kizuri barabara zote zinaenda nchi jirani
ukiweka
Nimesikia kuna trion 7 zinakopwa au sijui msaada kwa nini tusifanye kitu tukamaliza jambo fulani la kimkakati then tuje na jambo lingine
Kukopa kwa ajili ya maendeleo/biashara ni jambo jema endapo mkopo huo utatumika kwenye malengo yaliyokusudiwa
Mh. Rais Samia ameanza vizur tunamaliza jambo fulan tunaenda jambo jingine mfano madarasa, madawati,mashine za mahospitali nk. na fedha za uviko 19 zitaleta picha nzuri Wizara za maji,utalii,afya,elimu,tamisemi
Kuna mwaka nilienda Nyasa mbambabay kuna bonde linamwaga maji ziwa Nyasa ni kubwa sana nikamuliza mwenyeji wangu vipi kwa nini msifanye kilimo cha umwagiliji kwa kutumia maji ya ziwa Nyasa sikupata jibu
NB.
Nchi iwe na Sera na mikakati ambayo haibadiliki hasa kwenye issues za kitaifa
Sio leo Rais akiingia sitak bandari au hiki ok kama kinamapungufu ndio muda wa kurekebisha kasoro zote mradi uendelee