Huwa nasikitika Sana wanapolaumiwa wachezaji football wa Tanzania kuwa hawajui au hawapo serious pale timu yetu ya taifa inapofanya vibaya. Vijana hawa hulaumiwa sababu kazi yao hufanyikia hadharani ambapo na mashabiki hualikwa kushuhudia matokeo ya kazi yao.
Naamini kama na watendaji wa ofisi za umma wangekuwa wanafanyia kazi zao za kitaalam ktk majukwaa ya wazi na si ktk vi ofisi tena vyenye mafaili yaliyoandikwa SIRI wallah Watanzania tungeitisha mjadala wa kitaifa kutafuta suluhu ya matatizo ya uwajibikaji kati yetu. Serikalini kuna watendaji wabovu zaidi ya hawa wacheza football tunao watukana kila uchao.
Ni watendaji hawahawa wameshindwa kutengeneza miundombinu ya kuandaa wachezaji watetezi wa taifa wa kesho. Badala yake huishia kufanya mipango ya zimamoto kutaka matokeo ambayo wenzetu wamewekeza akili, maarifa, pesa na utaalam kuyapata.