Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani katika viwanja vya llulu Mkoani Lindi leo Disemba 1, 2022
Hotuba ya Rais Samia Suluhu
Tunapozungumza magonjwa ya UKIMWI na VVU tunazungumza muda wa miaka 30 tangu yalipoonekana kwetu kufika mwakani itakuwa mwaka wa 30 tangu mwaka 1983 ulipogunduliwa nchini ninaposimama hapa ni mwaka wa 29.
Dunia imedhamiria kukomesha majanga haya ya UKIMWI ifikapo mwaka 2030 na dunia inapigania usawa wa kijinsia katika kutokemeza janga hili la UKIMWI.
Napoongelea usawa namaanisha kuwa UKIMWI upo dunia nzima kama UVIKO hivyo kupata Usawa kwenye matibabu kwenye magonjwa yaliyo dunia nzima ni kazi sana ila tunashukuru tumepata misaada kwenye UVIKO na kwenye UKIMWI pia.
Mafanikio mliyoyafikia kupunguza vifo kupunguza maambukizi ni kwa sababu tulipata misaada kutoka kwa wahisani na niwashukuru sana ila bado wanasema jambo la unyanyapaa hatujalifanya vizuri bado kuna unyanyapaa na sisi tunasema tumejipanga vizuri na tuna mikakati ya kufikia 000, yaani 0 ya vifo, 0 ya maambukizi na 0 ya unyanyapaa na hiyo tunataka ikamilike 2030.
Kupitia hili tumejifunza kwamba kufanya kazi kwa ushirikiano kunaleta tija kubwa, hivyo inabidi tushirikiane katika kutokomeza hili kila mmoja afanye jukumu lake, kila mtu ajilinde, wanaotoa elimu watoe na walioambukizwa wasiambukize wengine, katika ushirikiano huu tutavuka na kufikia lengo.