Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais Samia akishiriki Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Machi 8, 2025 Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda akitoa salamu za mkoa
"Mhe. Rais, sherehe zetu zilihitimishwa jana na ulaji wa nyama... Nyama ya Mkoa wa Arusha haina uhusiano na mafundisho ya Dkt. Janabi. Sisi Wamaasi tunaendelea kula nyama miaka yote kwa kweli, nyama ni sehemu ya utamaduni wetu, nyama ni sehemu ya tiba yetu. Na tunakuomba Mheshimiwa Rais, baada ya futari basi ile nyama tuliyoionja jana, swala pamoja na wanyama wengine, tukukaribishe na wewe,”
RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZIA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE
"Mwaka huu tunaadhimisha siku ya mwanamke duniani ikiwa tu sio miaka 30 tangu kutolewa kwa tamko la umoja wa mataifa kule Beijing lililoweka misingi ya utekelezaji wa haki kwa mwanamke na mtoto wa kike bali pia tukitimiza miaka 10 ya uwepo wa maendeleo endelevu na miaka mitano ya jukwaa la kizazi chenye usawa hivyo hii ni fursa ya kutathmini mafanikio tuliyoyapata, hatua zaidi zinapaswa kuchukuliwa ili kuhakikisha kwamba kila msichana na mwanamke hapa nchini anapata nafasi ya kufikia ndoto zake. Ni vema tukawe pamoja katika kuhakikisha kwamba mabadiliko tunayoyahitaji yanapatikana"
"Binafsi nilipata nafasi ya kushiriki mkutano ule na nilivutiwa sana kusikia kwa wakati ule kuwa mkutano wa kihistoria unaongozwa na mwanamama shupavu kutoka Tanzania Balozi Getrude Mongela kupitia uongozi wake Tanzania ilitoa mchango stahiki na kuwasha mwenge wa matumaini ulioleta mageuzi makubwa kwenye haki za wanawake na mtoto wa kike kote ulimwenguni"
"Hatua mbalimbali za kisera na kisheria zimechukuliwa na zinaendelea kuchukuliwa katika kupambana na mila kandamizi kwa mwanamke na mtoto wa kike. Kaulimbiu ya maadhimisho haya ina mnasaba sana na matamko yale ya kimataifa, kaulimbiu yetu inasema WANAWAKE NA WASICHANA 2025 TUIMARISHE HAKI USAWA NA UWEZESHAJI"
"Kwa upande wetu Tanzania mpaka tunafanya tahmini ya mpango wa tatu wa maendeleo katika vision yetu kubwa ya miaka 25 tayari tulishapunguza umasikini kwa kiwango cha asilimia 26, pamoja na jitihada zilizochukuliwa leo hatushuki kwenye asilimia 30."
"Kwa upande wa kuondoa njaa Tanzania kitaifa tumeshaondoa njaa kwa asilimia 100, na katika lengo la kujitegemea kwa chakula, Tanzania tunajitegemea kwa chakula kwa asilimia 128 sasa kilichobaki ni mtu mmojammoja kuhakikisha kwamba habaki na njaa ama halali na njaa"
"Kwa upande wa swala la afya tumepiga hatua kubwa sana hasa kwenye maendeleo ya miundombinu, nyinyi mnatambua kwamba serikali yenu imejitahidi kujenga miundombinu ya afya nchi nzima katika kila ngazi kuanzia zahanati, hospitali za kata, wilaya, mikoa na hospitali za rufaa lakini sio tu kujenga miundombinu pamoja na miundombinu au vifaa vya matibabu na vifaa vingine vinavyotakiwa"
"Tumeweza kupunguza vifo vya wanawake wakati wa kujifungua wakati tunakwenda Beijing vifo vya wanawake wakati wa kujifungua ilikuwa vifo 1500 kwa vizazi hai laki moja leo tunapozungumza ni 104 kwa vizazi hai laki moja"
Aidha katika hotuba yake, Rais Samia ametangaza kuwa maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Wanawake yatafanyika kila baada ya miaka mitano, huku maadhimisho ya kila mwaka yakifanyika katika ngazi ya mikoa. Kwa mujibu wa utaratibu huo, maadhimisho mengine ya kitaifa yatafanyika mwaka 2030